Tuesday, February 19, 2013
OLD BAGAMOYO ROAD KUITWA MWAI KIBAKI ROAD KUANZIA KESHO
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik, barabara
hiyo yenye urefu wa kilomita 10.1 ni kuaniza kwenye mataa ya Moroccco
karibu na makao makuu ya Airtel hadi mzunguko wa kuelekea Africana kule
Mbezi Beach, mkabara na uwanja wa kulenga shabaha wa JWTZ.
Akiongea usiku huu, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Rais Kibaki anatarajiwa kuwasili kesho saa 9 alasiri na kupkewa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo usiku atamwandalia dhifa ya kitaifa Ikulu. Keshokutwa. Alhamisi, Rais Kibaki ataongea na wazee wa Dar es salaam katika ukumbi wa PTA ulioko viwanja vya SabaSaba barabara ya Kilwa Road. Pia atatembelea sehemu mbalimbali atazopangiwa katika ziara yake hiyo ambayo pia ataitumia kuwaaga Watanzania kwani muhula wake wa uongozi utafikia kikomo baadaye mwaka huu.

JERRY MURO KUENDELEA KUWA HURU
UPANDE wa Mashitaka katika rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa Aliyekuwa
Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji (TBC) Jerry Murro aliyekuwa
anakabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 10 umeiomba
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kuamuru kesi hiyo isikilizwe upya.
Mawakili wa wa Serikali walidai hayo jana mbele ya Jaji Fauz Twaib kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikosea kisheria katika kuweka kumbukumbu ya Mwenendo wa
kesi hiyo jambo lililosababisha kutoa uamuzi usio wa haki.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Novemba 30 mwaka juzi na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Frank Moshi, ambayo ilimuachilia huru Murro, Deogratius Mgasa na Edmund Kapama waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka hayo.
Katika rufaa hiyo, Wakili wa Serikali Awamu Mbagwa alidai kuwa mahakama haikuandika vizuri kumbukumbu za ushahidi na vielelezo katika Mwenendo wa kesi ambapo kuna baadhi ya
ushahidi haueleweki unamaanisha nini jambo lililosababisha Hakimu kufikia uamuzi usio wa haki.
Aidha alidai kuwa kuna baadhi ya vielelezo na ushahidi haupo kwenye mwenendo wa kesi, ikiwemo maelezo ya onyo yaliyotolewa na Murro katika kituo cha polisi na kitabu cha wageni waliofika katika hoteli ya Sea Cliff ambayo wajibu rufaa wanadaiwa kuomba rushwa.
Aliieleza mahakama kuwa, kitabu cha wageni kilikataliwa kupokelewa mahakamani kama kielelezo lakini katika Mwenendo wa kesi haijaandikwa na hata uamuzi wa pingamizi la kielelezo hicho haukutolewa na kudai kuwa kukosekana kwa uamuzi huo kumesababisha Hakimu kutofikia uamuzi wa haki.
Aidha katika mwenendo wa kesi hakuna kumbukumbu za wao kuwasilisha Mkanda wa kamera inayonasa matukio (CCTV) ulioonesha wajibu rufaa walipokwenda kufanya
makubaliano ya kupokea rushwa, lakini walishindwa kuuangalia na baadaye wakaamua kutumia picha za kawaida.
Aliongeza kuwa kesi hiyo awali ilikuwa inasilizwa na Hakimu Gabriel Mirunde lakini Hakimu Frank Moshi ndiye aliyetoa hukumu hivyo kutokana na kuandikwa vibaya kwa mwenendo wa kesi hiyo Hakimu Moshi alishindwa kuelewa ushahidi na utoa uamuzi usio wa haki.
Akijibu hoja wakili wa Murro, Richard Rweyongeza aliiomba mahakama kutupilia mbali hoja hiyo kwa uwa haina misingi kisheria pia wakata rufaa hawajaeleza ni vipi kukosewa kwa mwenendo wa kesi hiyo kumesababisha kufikia uamuzi usi sahihi.
Naye Wakili wa wajibu rufaa wengine, Majura Magafu alidai kuwa wakata rufaa hawajalalamika kuhusu hukumu iliyotolewa bali maandishi katika mwenendo wa kesi na katika hukumu hiyo hakuna sehemu ambayo Hakimu alilalamika kuwa alipata shida kusoma mwenendo wa kesi hiyo.
Alidai endapo mahakama itamua kesi hiyo isikilizwe upya itakuwa ni sawa na kufanyabiashara ya kuchagua mahakimu kuwa kama wameshindwa kwa hakimu huyo wajaribu kwa mwingine jambo ambalo haliruhusiwi kisheria.
Warufani walikuwa na sababu nne lakini imesikilizwa sababu moja ambapo baada ya kusikiliza hoja hizo Jaji Twaib aliahirisha shauri hilo hadi Aprili 29 mwaka huu atakapotoa uamuzi.
Washitakiwa wanadaiwa kuwa waliomba rushwa kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage kwa lengo la kuzuia kutangazwa kwenye
televisheni habari za tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma akiwa mhasibu wa halmashauri hiyo.
Katika madai hayo, Muro na wenzake wanadaiwa Januari 28 mwaka jana jijini Dar es Salaam, walikula njama ya kutenda kosa hilo na Januari 29 mwaka jana katika Hoteli ya
Sea Cliff Dar es Salaam waliomba rushwa ya Sh milioni 10 kutoka kwa Wage.

Monday, February 18, 2013
INGIA HAPA KUPATA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012

Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza
rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.
Jumla ya
watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia dara
la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika
mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema
kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na
daraja la tatu ni 15426 na walio feli ni 24903.
Shule
bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo,
Feza Boys DSM, Marian Girls Bagamoyo, na Simini ndizo zipo tano bora
huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012
MPASUKO WAIKUMBA UVCCM
| Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis |
Chanzo kutoka ndani ya kikao hicho kilichotarajiwa kumalizika jana
katika ukumbi wa White House, mjini Dodoma, kilisema hali ya
kutokuelewana ilitokea mara baada ya Sadifa kutoa hotuba hiyo juzi
mchana.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kulikuwa na hali ya kutoelewana ndani
ya kikao hicho huku wasemaji wa umoja huo wakikatizwa mara kwa mara na
kelele za kuzomeana.
“Baadhi ya vijana walikaa katika makundi na kuazimia kumuondoa
mwenyekiti kwa kitendo chake cha kuwadhalilisha tena mbele ya waandishi
wa habari wakati wa ufunguzi wa kikao hicho,” kilisema chanzo hicho.
Pia vijana hao walikasirishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa Taifa
Sadifa kumtimua mmoja wa waliokuwa wagombea wa nafasi ya umakamu
mwenyekiti, Paul Makonda, kwa madai kuwa alikaririwa na vyombo vya
habari mara baada ya uteuzi huo akitaka kupewa nafasi ya kufikiriwa.
Aidha, wajumbe wa Baraza hilo walikerwa na kitendo cha Sadifa
kumwachisha kazi mmoja wa watumishi wa umoja huo kutokea Visiwani
Zanzibar aliyejulikana kwa jina moja la Jamal.
Mvutano huo uliodumu kwa zaidi ya saa mbili na kutawaliwa na vikao
vya siri, ulifanya kuchelewa kuanza kwa kikao hicho kwani badala ya
kuanza saa 5:00 asubuhi kilianza saa 7:00 mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mjumbe kutoka mkoani
Mbeya, David Mwakiposya, alisema hotuba aliyotoa mwenyekiti wao ni mbovu
na haifai.
“Kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa Vijana wa CCM ya mwaka 2008,
Baraza Kuu ndilo linathibitisha uteuzi wa wajumbe wa Baraza, lakini cha
kusikitisha aliwafukuza wajumbe wawili ambao wakati wa mkutano mkuu
yeye aliwateua na tena aliwaita mwenyewe waje katika mkutano huu,”
alisema na kuongeza kuwa:
“Ni kitendo kisichofaa kabisa katika nchi yetu wakati tungali
tunatengeneza demokrasia. Bahati nzuri alilizungumza hili mbele yenu,
hapa mmeniuliza maoni yangu kuhusiana na hotuba hii maoni yangu ndiyo
hayo siiungi mkono hotuba yake.”
Mwakiposya alisema Sadifa aliongea kuhusiana na suala la mapenzi
ndani ya baraza hilo kwamba limekuwa likisababisha kuvujishwa kwa siri
za vikao, jambo ambalo alisema halina ukweli wowote.
Alisema mwenyekiti huyo katika hotuba yake aliwatuhumu meza kuu
(viongozi wa juu wa umoja huo ), kuwa wamekuwa wakijihusisha na mapenzi
na hivyo kazi hazifanyiki jambo ambalo halina ukweli.
“Mimi kama mjumbe wa Baraza Kuu nimesikitishwa, nimeguswa,
sifurahishwi na hayo yaliyojitokeza katika hotuba hiyo, “ alisema
Mwakiposya huku akisisitiza kuwa hayo ni maoni yake binafsi.
Kuhusu suala Mwenyekiti huyo kutamka wakati akiwania nafasi hiyo
aliingizwa katika makundi yanayojiandaa kwa ajili ya urais, Mwakiposya
alisema: “Hiyo ndiyo tabu ya kuwa na kiongozi anayeamini katika hili
huku anatenda hivi.”
“Alipowateua hawa watu aliowafukuza tuliamini kuwa haegemei katika
makundi, lakini katika utekelezaji hakuna….Mimi sifahamu katika UVCCM
kama kuna makundi, lakini baada ya kusema hilo nikajua kuwa kumbe kuna
makundi,” alisema.
Na kwa upande wa siri kuvuja, alisema yeye ni mmoja wa watu ambao
anaamini kuwa kiongozi yoyote anayevujisha siri za vikao hafai katika
uongozi.
Hata hivyo, alisema hajawahi kusikia kuhusiana na kuvujishwa kwa
siri za vikao na viongozi licha ya kuwafahamu viongozi mbalimbali wa
umoja huo.
“Tunaonyana ndani ya vikao halali hatuwezi kuzungumza kwa
waandishi wa habari mambo ambayo tunayaona kuwa hayaendi sawa
tutayazungumza ndani ya vikao vyetu,” alisema alipoulizwa kuhusiana na
kauli kuwa kuna baadhi ya makundi yalionekana kukaa kabla ya kuanza kwa
kikao cha siku ya jana.
Kuhusu madai ya kutaka kumng’oa mwenyekiti wao, Mwakiposya alisema
hajasikia kitu kama hicho na kwamba kama kinakuwapo umoja huo
unataratibu za kikanuni za kufuata ili kumng’oa mwenyekiti.
“Kanuni ya mwaka 2008 inasema kama ikithibitika kiongozi yeyote
amekiuka kanuni Baraza linaweza kutoa pendekezo katika kikao cha juu
kumsimamisha, lakini kama sisi tunataka kumsimamisha kama vijana
hatujafikia huko bado,” alisema.
Alisema iwapo ikidhibitika kuwa hawawezi kwenda sambamba na kiongozi yeyote yule basi watafukuzana.
Alipoulizwa kama mwenyekiti huyo amekiuka kanuni yoyote, alisema
amekiuka kanuni ya kufukuza watumishi wa umoja huo kwa kumfukuza mmoja
wa watumishi kutoka Zanzibar.
Alifafanua kwa mujibu wa kanuni, kikao chenye mamlaka ya kumfukuza mtumishi ni Baraza Kuu la Umoja wa Vijana.
Kwa upande wake, Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM (jina tunasitiri),
alisema alisikia tetesi kuhusiana na kung’olewa kwa mwenyekiti, lakini
UVCCM ni jumuiya ya muda mrefu ambayo ina taratibu zake za kumuondoa
kiongozi.
“Usiwaone hivi, hawa ni viongozi waliokomaa, hakuna ambalo linaweza
kuharibika ila inachofahamu hakuna mtafaruku na kama ulikuwapo
umeisha,” alisema na kuongeza wajumbe hao wako salama na wanaendelea
vizuri.
Alisisitiza kuwa hakuna mkanganyiko utakaotokea mara baada ya
kumalizika kwa kikao hicho cha siku mbili ambacho kitafuatiwa na semina
na kwamba hakuna kitu kipya kwa kuwa kila inapokaa jumuiya hiyo kumekuwa
na harakati.
Katika tukio jingine waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali
vya habari, walijikuta wakikalishwa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo,
Mboni Mhita, kwa zaidi ya saa tatu katika ukumbi wa mikutano wa
sektarieti ya chama hicho.
Mhita aliwaita kwenye chumba hicho, kwa madhumuni ya kuwaeleza kile
kilichotokea katika kikao hicho kwa siku mbili za juzi na jana.
“Tukubaliane nitazungumza nitazungumzia agenda za jana (juzi) na
kinachoendelea leo (jana), tu, lakini sitazungumzia yatokanayo…ama
vinginevyo muendelee kumsubiri Katibu Mkuu aje aongee nanyi,” alisema.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuletewa faili aliloliitisha,
aliondoka na kuwataka waandishi wa habari kuendelea kusubiri kwa sababu
alikuwa akimsubiri mjumbe wa kitengo fulani aje azungumzie mambo ambayo
hata hivyo hakuyafafanua.
Akijibu madai hayo, Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, alisema
walipanga kuanza kikao saa 7:00 mchana na kwamba kwa kuwa wajumbe
wanafahamiana kukaa katika makundi si kosa.
“Maana Katiba yenyewe inaruhusu watu kukaa vikundi ili mradi wawe
hawavunji taratibu, sheria na kanuni…baada ya muda kufika si waliingia
kwenye kikao kama jana (juzi) kikao kilikuwa kizuri tofauti na vyombo
vya habari mlivyokuwa mkisema huko nje,”alisema.
Kuhusu hoja ya kumng’oa kwa madai ya kukiuka kanuni, Sadifa alihoji
“ Kanuni namba ngapi?.. Jamal hajafukuzwa sasa wewe utuambie
aliyemfukuza ni nani? Jamal ni mjumbe halali wa hiki kikao kama angekuja
lakini kwa bahati nzuri ama mbaya, Jamal mwenyewe alinifuata baada ya
majina kurudi na kuniambia kuwa amechoka anataka apumzike.”
Alisema kwasababu Jamal anafanya kazi mbili Zeco visiwani
Zanzibar na katika Chama kama Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana,
alimuomba apumzike ili aendelee na utumishi wake serikalini.
Kuhusu hotuba yake kuwadhalilisha, Sadifa aligeuka mbogo: “Nani, wajumbe? Tutajie? ama wewe? Eh, tuthibitishie.”
Hata hivyo, alikanusha kuwa hakuna mjumbe aliyedhalilishwa wala
aliyelalamikia hotuba yake na kuwalaumu waandishi wa habari kuwa wana
matatizo ya kuwagombanisha watu.
Kuhusu Makonda, alisema kanuni ya Umoja wa Vijana inasema yeye
anateua mtu ambaye anatakiwa kuthibitishwa ndani ya kikao cha Baraza
Kuu la umoja huo na kanuni hizo haziruhusu kupeleka kila kitu katika
vyombo vya habari.
Alisema baada ya kuona magazeti yamemnukuu Makonda akisema kuwa
hawezi kukubali uteuzi huo ili asije kuonekana kuwa amehongwa, alifahamu
hizo ni hasira za uchaguzi.
“Kwa hiyo mimi nilimpigia simu mmoja mmoja, Makonda Msarika,
jamani nimeona statement (taarifa), hizi katika magazeti haya, hebu
niambieni uteuzi huu mmeukubali ama mmeukataa? Wao wenyewe hakuna
aliyekuja kunipa kauli yake kama wamekubali uteuzi,” alisema.
Alimtolea mfano Makonda kuwa amemwita wakutane lakini alikataa,”
unajua siasa lazima ukae na mwenzako mzungumze mbadilishane mawazo ndiyo
siasa, jana usiku (juzi ), baada ya kumaliza kikao, nilimpigia
tukutane…tukae tuvunje migogoro iliyokuwapo, lakini hakuonekana.”
Alisema baadhi ya wajumbe walipoona ujio wa Makonda, walitaka kufanya vurugu wakihoji juu ya ujio wake.
“Kwa sababu pia baadhi ya wajumbe kwa kuona Paul Makonda, pale
walitaka kuanzisha vurugu, kwa busara tukatuliza sijui tumeelewana
vizuri?...Alitakiwa baada ya kusomwa kanuni na kujulikana wajumbe, basi
wajumbe wabaki kwa wakati ule si mjumbe kwa maana hakuthibitishwa na
Baraza Kuu kwa hiyo alitakiwa kwanza atoke ili Baraza Kuu liridhie ama
lisiporidhia sawa,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE
MULUGO: MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUTANGAZWA LEO
| Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo |
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo, aliiambia NIPASHE
katika mahojiano jana kuwa taratibu zote kwa ajili ya kutangaza matokeo
hayo zimekwisha kukamilika na sasa yatatangazwa rasmi leo.
Wiki iliyopita Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa,
akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza ajira mpya za
walimu aliahidi kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yatangazwa
mwishoni mwa wiki hiyo, lakini hata hivyo hayakutangazwa.
Dk. Kawambwa ambaye aliulizwa ni kwa nini matokeo ya mtihani huo
yanacheleweshwa kutangazwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, alisema
kimsingi hayajachelewa kwa sababu wanafunzi watakaochaguliwa kuingia
kidato cha tano wanatakiwa kuripoti mwezi Julai mwaka huu.
“Kila mtu anauliza suala la matokeo, kimsingi hatujachelewa sababu
hata wanafunzi watakaochaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano
watajiunga mwezi Julai, Mungu akipenda yatatangazwa kabla ya Jumamosi,”
alisema Dk. Kawambwa.
CHANZO: NIPASHE
CHADEMA KUITIKISA ARUSHA LEO
Katibu wa Muda wa Kamati ya Uratibu Kanda ya
Kaskazini, Amani Golugwa alisema mkutano huo utafanyika katika Viwanja
vya Shule ya Msingi Ngarenaro na utahudhuriwa na wabunge wote wa Chadema
kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa
Taifa, Freeman Mbowe. Kwa mujibu wa Golugwa, Kanda ya Kaskazini
inajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
“Tunazindua Kanda ya Kaskazini kutekeleza uamuzi
wa Baraza Kuu lililoagiza mfumo na shughuli za uendeshaji wa chama
ushuke hadi ngazi ya majimbo ambayo ndiyo sera ya Chadema,” alisema
Golugwa.
Kabla ya mkutano wa leo, viongozi zaidi ya 200 wa
Chadema kutoka mikoa na majimbo 30 ya Kanda ya Kaskazini wakiwamo
wabunge, wenyeviti, makatibu, wenyeviti na mameya wa Halmashauri
zinazoongozwa na Chadema,walifanya vikao vya ndani kuweka mikakati na
mfumo wa utendaji kikanda. Kwa mujibu wa Golugwa, ambaye pia ni Katibu
wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, kikao cha ndani pia kilihudhuriwa na
mwasisi na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei.
Mbowe ambaye ni mmoja wa wajumbe waliohudhuria
vikao vya ndani, ndiye atakuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu kwenye
mkutano wa hadhara ambao pia utatumika kuwatambulisha wajumbe wa timu ya
uratibu ya Kanda ya Kaskazini.
Mkutano huo ni wa pili kwa Chadema ndani ya wiki
mbili zilizopita baada ya kufanya mkutano mkubwa Dar es Salaam
uliotumika kuueleza umma udhaifu wa mhimili wa Bunge na ukandamizaji
unaodaiwa kufanywa dhidi ya wabunge wa chama hicho na uongozi wa mhimili
huo wa dola.
Katika mkutano huo, viongozi wa Chadema
waliutangazia umma namba za simu za Spika Anne Makinda na Naibu wake,
Job Ndugai ili wananchi wawapigie au kuwatumia ujumbe mfupi
kuwashinikiza kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za bunge katika
uendeshaji na maamuzi ya chombo hicho.
MH PINDA ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA KIISLAM NA KIKRISTO KUJADILI MGOGORO WA UCHINJAJI NYAMA
Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza akichangia katika kikao cha
klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji
wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa
Banki Kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam
na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.
Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam
na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa
Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Sheikh Mkuu wa
Wilaya ya Sengerema, Ahmed Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa
Buswelu, Athumani Ali katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji
wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu
kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16,
2013.
Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema,
Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda
na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro
wa uchinjaji wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini
Mwanza Februari 16,2013.
Sunday, February 17, 2013
MBELA ASKARI ALIEKATWA MIKONO ANATUMIA MIGUU KULIMA
Ukiliona shamba hilo la Mbela licha ya kuwa na mahindi, pia lina maharage, magimbi na ndizi yaliyostawi na kupendeza.
Huwezi kuamini kuwa shamba hilo linalimwa na Mbela, ambaye ni mlemavu kwa kutumia miguu yake.
Ulemavu huo umemkuta na kulazimika kulima kwa
miguu, baada ya kukatwa mikono yake alipokuwa akidai kurejeshewa mahari
kutoka kwa wakwe zake.
Mbela anasema kuwa pamoja na ulemavu alioupata
ukubwani, hawezi kutembea mitaani kuomba omba, wakati bado mwili wake
una viungo vingine anavyoweza kuvitumia kujipatia mahitaji yake ya kila
siku.
Kilichosabisha kukatwa mikono
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.
Anaeleza kuwa kabla ya kuwa mlemavu, aliwahi
kuajiriwa na Jeshi la Polisi, akifanyia kazi Kituo cha Polisi Makuyuni
mkoani Arusha miaka ya nyuma, lakini alicha kazi hiyo baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Baada ya hali hiyo, aliona bora arudi nyumbani kwao Kijiji cha Malumba wilayani Tunduru ili kuendelea kupata matibabu.
Mbela anasema kuwa alipofika kijijini kwao, aliendelea kupata matibabu na baadaye akapona.
Akizungumza kwa kusaidiwa na rafiki yake wa karibu ambaye amejitambulisha kwa jina la Zacharia Dikala, maarufu kama Babu Masai, Mbela anasema kuwa alikutana na matatizo ya kukatwa mikono miaka minne iliyopita.

Mbela ambaye pia ni baba wa watoto Mwanabibi Salim
(28), Siku Salim (19) na Said Salim (24) anaeleza kuwa akiwa na mkewe
na familia yake, siku moja ali kwenda nyumbani kwa wakwe zake waliokuwa
wakiishi katika kijiji hicho cha Malumba na kuchukua mbuzi wake aliotoa
mahari miaka ya nyuma wakati akimchumbia mkewe ambaye ndiye aliyemzalia
watoto hao.
Anasema kuwa wakati huo alikuwa na nguvu na
alitumia mabavu kufanya fujo, hadi akafanikiwa kufika zizini na kupora
mbuzi, bila kujua kama maisha yake yange badilika na kuishia pabaya.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
Hata hivyo, anajutia kitendo hicho akisema kwamba iwapo angefahamu mapema yataka yomkuta, asingethubutu kwenda kufanya fujo hizo.
“Nilikuwa najiamini sana, nilikuwa na nguvu sana,
nikaamua kwenda ukweni kwangu kufuata baadhi ya mifugo yangu, niliyotoa
mahari wakati namposa mke wangu,” anasimulia na kuongeza:
Subscribe to:
Posts (Atom)