Facebook Comments Box

Saturday, February 16, 2013

HII NDIO HUKUMU YA KESI YA SISTER ALIEFUMANIWA NA MME WA MTU

MAHAKAMA ya Mwanzo mjini hapa,  imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000 mlalamikaji.
Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa.

Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.
Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24  mwaka jana majira ya saa 7 usiku  ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas.
Akisoma  hukumu  hiyo juzi, hakimu wa  mahakama  hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote  kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi  uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.
Awali katika  utetezi wake  mdaiwa  aliiambia mahakama  hiyo kuwa  kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa  mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.
Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku  huo wa mkesha  wa Krismas  mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu,  walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika   moja ya vyumba katika nyumba ya kulala  wageni ya Chipa, akasainishwa.
“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa  hana  mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi  iliyoandaliwa na mwenyekiti  huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.


HAWA NDIO WABUNGE WALIOKUBALI KWENDA JKT NA SABABU ZAO






 JUMLA ya wabunge 47 kutoka vyama CCM, Chadema na NCCR-Mageuzi, wamekubali kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa ajili ya mafunzo na uzalendo kwa taifa.
Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Makao Makuu ya JKT, zinasema wabunge hao wametawanywa katika vikosi mbalimbali na wanatakiwa kuripoti kwenye vikosi vyao kunzia Machi mosi, mwaka huu.
Msemaji wa JKT, Meja Emmanuel Mruga, alipoulizwa kuhusu wabunge hao kujiunga na jeshi hilo, alisema mpaka sasa wana orodha ya wabunge 47 kutoka vyama mbalimbali.
Alisema wabunge hao, wametawanywa katika kambi mbalimbali kwa ajili ya mafunzo ambayo yatarajia kuanza mwezi ujao.
Alisema wabunge hao, waliomba wenyewe kwa ajili ya kupata mafunzo ambayo wanaamini yatawajengea uzalendo zaidi kwa taifa lao.
Baadhi ya wabunge ambao KITONGONI imepata majina yao na vyama wanavyotoka kwenye mabano ni David Kafulila (NCCR-Mageuzi), Zitto Kabwe (CHADEMA), Halima Mdee (CHADEMA), Freeman Mbowe (CHADEMA), Abdulkarim Shaha (CCM), Esther Bulaya (CCM), Twaida Galusi (CCM), Neema Hemed (CCM), Ezekiel Wenje (CHADEMA), Joshua Nassari (CHADEMA), Raya Ibrahim (CHADEMA), Godbless Lema (CHADEMA) na Nyambari Nyangwine (CCM).
Akizungumzia mafunzo hayo, Zitto Kabwe alisema kuanzia sasa anajiandaa kuanza maisha mapya ya jeshi na atapumzika siasa kwa muda wa miezi sita.
“Najiandaa kupumzika siasa, kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), nadhani ni hatua nzuri ambayo tunataka kuwaonyesha Watanzania wazalendo na vijana wenzetu,” alisema Zitto.
Naye Mdee, alisema zaidi ya robo tatu ya wabunge wote vijana wa chama hicho, waliomba kujiunga JKT na tayari wamepangwa katika vikosi mbalimbali.
“Si mimi na Zitto, nakwambia karibu robo tatu ya wabunge vijana wa CHADEMA, tumeamua kujiunga kwenye mafunzo ya JKT,” alisema Mdee.
Alisema yeye amepangwa kikosi cha 842 KJ kilichopo Mlale, mkoani Ruvuma.
Alisema wengine ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ambaye amepangiwa kikosi cha JKT Ruvu, Mkoa wa Pwani.
Habari zinasema Mbowe aliomba kujiunga JTK na amepangiwa kambi moja mkoani Tabora.
Akizungumzia sababu za kujiunga na jeshi hilo, Mdee alisema wanataka kujifunza mambo tofauti yatakayowasaidia kutekeleza wajibu wao wa kisiasa na kijamii sawasawa.
“Unajua sisi ni viongozi wa watu, tunadhani mafunzo ya kijeshi yatatusaidia kutekeleza kazi za kila siku, kujifunza ukakamavu, na zaidi kwa vipi tunaweza kujilinda kwa mantiki ya usalama binafsi.
“Kingine ni kujifunza kazi za kila siku za maisha, kiuchumi, kijamii, kilimo na vitu kama hivyo ukizingatia sisi ni viongozi tunaopaswa kuongoza watu, hususani wapiga kura kwa mifano.
Kuhusu kujifunza zaidi uzalendo kama ambavyo imekuwa ikisemwa na viongozi serikalini, Mdee alisema uzalendo ni tabia ya mtu binafsi na kamwe jeshi haliwezi kumfundisha mtu uzalendo.
“Ninakubaliana na suala la nidhamu, jeshi linaweza kumfundisha mtu nidhamu, lakini siyo uzalendo.
“Walioharibu nchi na kuitumbukiza katika ufukara na ufisadi karibu wote wamepitia jeshini, hatuna cha kujifunza kwao kutokana na kwenda kwao jeshini,” alisema na kuongeza:

“Ngoja twende huko tukajifunze mambo ya ziada, naamini tutapata kitu cha ziada kwa ajili yetu na jamii tunayoiongoza”.


SINGANO (MESSI) NA KAPOMBE KWENDA SUNDERLAND YA ENGLAND


WACHEZAJI chipukizi wa timu ya soka ya Simba Ramadhan Singano ‘Messi’ na Shomari Kapombe wanatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika kituo maalum cha vijana cha klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Sunderland.
Aidha, vuiongozi wa Simba, wanatarajiwa kwenda huko hivi karibuni  ambapo pamoja na mambo mengine watashuhudia mechi ya ligi kuu ya England baina ya wenyeji Sunderland dhidi ya Fulham itakayopigwa Machi 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema, hatua hiyo inafuatia ushirikiano baina yao na Sunderland uliotokana na matunda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Alisema katika makubaliano yao ya ushirikiano na udhamini, Sunderland ambayo imepania zaidi kuwekeza katika soka la vijana ambapo itakuwa ikichukua wachezaji katika makundi tofauti ya umri wa klabu ya Simba na kwenda kujifunza katika taasisi yao ya vijana.
Rage aliongeza kuwa, Kapombe na Singano watakwenda huko mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo maalum katika kituo cha kulea vijana cha timu hiyo, kama watafanya vema katika mazoezi yao huenda wakasajiliwa kuichezea timu ya vijana ya Sunderland.
Aidha, Rage aliongeza kuwa mazungumzo kuhusiana na udhamini wao na Sunderland yapo katika hali na ndiyo maana uongozi umealikwa kwenda huko si kwa ajili tu ya kushuhudia mechi bali kubadiklishana uzoefu na viongozi wa timu hiyo.
Akizungumzia maandalizi ya mechi yao yao ya ligi ya mabingwa Afrika kesho dhidi ya CR Libolo ya Angola, Rage alisema kikosi cha timu hiyo kipo katika hali nzuri na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakisha wanashinda, hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia.
Kuhusiana na kusuasua kwa Simba kwenye ligi kuu bara, Rage alisema hiyo inatokana na timu zote zinazoshiriki ligi hiyo kujipanga vema,huku akibeza watu wanaoendekeza ushabiki zaidi badala ya kuangalia ushindani uliopo uwanjani.
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharoos amewataka watu kujitokeza kwa wingi kuishangilia Simba katika mchezo wake wa kesho huku akiwasihi zaidi wanawake wenzake kwenda kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam utakapopigwa mchezo huo.

JE, WAJUA MPENZI WA PREZZO ALIEKUFA ALIKUWA MKE WA MTU? ANGALIA PICHA HIZI ZA HARUSI


 
 
 
 
 
 
 


Baada ya kuweka picha hizo za ushahidi kuwa marehemu alikuwa mke wake jamaa akaamua kutoa biti zito kwa Prezzo akae mbali katika kipindi hiki kigumu katika familia yake


UMOJA WA MATAIFA WASEMA MAZUNGUMZO NDIO NJIA SAHIHI YA KUMALIZA MIGOGORO YA KIDINI

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson
Wakati viongozi wakuu  mbalimbali nchini Tanzania  wakisisitiza haja na umuhimu wa viongozi wa
madhebu ya dini kuwa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara. Umoja wa Mataifa
nao kwa upande wake  unaeleza kwamba ni
kwa  njia ya  mazungumzo 
migogoro ya dini inaweza kuepukika.

 Kauli hiyo ya Umoja wa Mataifa,  umetolewa na  Jan Eliasson,Nabu Katibu Mkuu wa  chombo hicho ya kimataifa ,  wakati wa 
tukio maalum  la Muungano  kwaajili ya utamaduni wa Amani kwa njia
ya  maelewano ya  madhehebu ya dini. Tukio ambalo limefanyika
mwishoni mwa wiki hapa umoja wa mataifa likiwahusisha  wawakilishi kutoka  dini mbalimbali, vyama visivyo vya kiserikali
na mabalozi.

“Migogoro mingi inayoendelea  hivi sasa duniani,  ni migogoro ya kidini. Mazungumzo baina ya
imani mbalimbali yanaweza kusaidia kusuluhisha migogoro hii.  Tunaweza kupambana na chuki kwa njia ya
mazungumzo   ili kujenga maelewano   na
kujenga daraja la maisha bora kwa jamii zetu”.Akasema  Naibu Katibu Mkuu

Na kuongeza kuwa, dini zote
zimekuwa  mstari wa mbele katika juhudi
si tu za kuhimiza amani na upendo, bali hata katika miradi ya  kuwasaidia watu maskini kwa kutoa huduma  kama vile za afya, na kuwasaidia vijana.

 Hata hivyo akaonya kwamba, siasa kali za  kidini zimekuwa chimbuko la uharibifu wa kudumu
na  mateso  katika jamii.

Na kwa sababu hiyo akasisitiza
kutoachiwa kwa vikundi vya dini vyenye misimamo mikali  kuharibu na kuvuruga amani  na maendeleo na kazi nzuri inayofanywa na
madhehebu ya dini .



 “Hatuwezi kuruhusu kundi dogo la watu
wenye misimamo mikali  kuharibu kazi
nzuri zinazofanywa na  jumuia za kidini
kwa waumini wao duniani kote” akahimiza Bw. Eliasson

Akaelezea  wasi wasi wake kuhusu vijana kutumiwa  na vikundi vyenye misimamo mikali
kueneza  kampeni za chuki na  vurugu kwa ahadi za kupata dhawabu au wokovu
ili wao watimize malengo yao.

“Kwa kawaida  vijana wana nguvu.  Tunapashwa 
kutafuta   njia nzuri na sahihi za
kuwafanya wazitumie nvugu  zao kuboresha
maisha yao” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.

Naye 
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuk Jeremic kwa  upande wake alisema  Umoja wa Mataifa unaweza  kufaidika sana  kama viongozi wote wa dini watajihusisha na
kufanya kazi kwa moja ili kuleta amani. Huku akiutaka  Umoja huo kuogeza kasi ya kushirikiana na
madhehebu ya dini.

“ Hebu basi  na turejee na kukumbatia wito unaotolewa na imani
zetu, wito wa kuwasaidia watu wengine wenye matatizo, wito wa kuheshimiana
wenyewe kwa  wenyewe,ikiwa  ni pamoja na 
uhuru wa kuabudu wakati wowote na mahali popote bila ya kujali tofauti
zetu za imani”.

Rais huyo wa Baraza Kuu akasema kila
mtu anawajibu wa kuwasiliana na mwenzake na kusahau yaliyopitia na kuonya
kwamba kama vyanzo vilivyopita  vya
migogoro ya kidini vitaendelea kukumbushiwa mara kwa mara, kuna hatari kubwa ya
kuitumbukiza dunia katika  machafuko ya
kutisha.



ZIARA YA MAMA SALMA LINDI MJINI NA WANACHAMA WA CHADEMA NA CUF WALIOJIUNGA NA CCM


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mama Salma Kikwete mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nanyanje, wilaya ya Chikonje, wilaya ya Lindi mjini.

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Chikonje, wakimsikiliza Mama Salma Kikwete alipozungumza nao katika kikao cha ndani, kwenye Ofisi ya CCM ya Kata hiyo.

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Lindi mjini, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimsalimia mwananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara aliohutubia katika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje wilayani humo leo, akiwa katika ziara ya siku saba kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Mama Salma Kikwete akipokea kadi ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Salma Saidi (kushoto) baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nanyanje, Kata ya Chikonje mkoani Lindi.

Wanachama wapya wa CCM waliokabidhiwa kadi zao wakiwemo kutoka vyama vya CUF na Chadema, wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mama Salma Kikwete.

 Wasanii wa kundi la ngoma ya zindiko ya Chikonje wakionyesha umahiri wao katika mkutano huo.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi.


 Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma ya zindiko ya wakazi wa Chikonje, iliyotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo.

Wananchi wakiselebuka kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kijiji cha Nanyanje kata ya Chikonje mkoani Lindi.



BAHANUZI AMLAUMU KOCHA KWA KUTO KUMUAMINI

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Said Bahanuzi amesema anafikiri kwa sasa amerudi kwenye fomu isipokuwa tu kocha ndiye anashindwa kumwamini kuanza kikosi cha kwanza.
 

Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts amekuwa akimtumia Bahanuzi kama mchezaji wa akiba tangu aliporejea uwanjani.

Bahanuzi aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro alikuwa anasumbuliwa na maamivu ya nyama za paja aliyoyapata akiwa na timu ya Taifa Stars mwaka jana.
 

Katika mechi mbili za ligi ambazo nyota huyo ametokea benchi zikiwa zimebaki dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika amefanikiwa kutoa pasi ya bao kila mechi.

Mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Bahanuzi ndiye aliyetoa pasi kwa Hamis Kiiza kufunga bao la kusawazisha. Timu zote mbili zilifungana bao 1-1.


Pia, mchezo wa African Lyon uliochezwa Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Bahanuzi akitokea benchi alitoa pasi kwa Nizar Khalfan aliyefunga bao la tatu wakati Yanga ikishinda 4-0.


Mara zote anapoingia mshambuliaji huyo mwenye nguvu za miguu na uwezo wakufyatua mashuti makali, amekuwa akiichangamsha safu ya ushambuliaji ya Yanga tofauti alivyokuwa benchi.


"Kwa sasa nafikiri nimerejea kwenye fomu. Nafikiri kocha tu ndiye anashindwa kuniamini." alisema Bahanuzi mwenye bao moja kwenye ligi alilofunga kwa penalti dhidi ya Simba Oktoba 3, mwaka jana.


"Nilikuwa nasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. Kwa sasa nafikiri hali yangu imeimarika kama awali." alisisitiza.


Kwa upande wake Ernie Brandts alisema; "Siwezi kumchezesha dakika 90. Nadhani Bahanuzi ametoka kwenye majeruhi. Kwa hiyo nimekuwa nikimpa dakika 15 za mwisho kutizama maendeleo yake.


"Nafikiri ameimarika kwa mechi mechi ambazo nimemuona akicheza."


Friday, February 15, 2013

MAELFU WAMZIKA SHEIKH BACHO


Sheikh Nassor Alisaliwa katika Viwanja Vya Maisara na Kuzikwa kijijini kwao Donge
Kutokana na watu kuwa wengi sala ya maiti ilifanywa kwenye viwanja vya Maisara na sio msikiti wa kikwajuni kama ilivyotangazwa hapo mwanzo. Mwenyezi Mungu Amuweke marehemu mahala pema peponi Ameen.

Thursday, February 14, 2013

PICHA JINSI WATOTO WALIVYOVAA KAMA BEYONCE NA RIHANNA


Beyonce.
Picha zote za mastaa unazoziona hapa zinaonyesha jinsi walivyovaa kwenye Redcarpet ya tuzo za Grammy 2013 ambapo kwa ubunifu wake, Tricia Messeroux aliamua kufanya project ya kuwapiga picha watoto ambao wanafanana na baadhi ya mastaa waliotokelezea kwenye Grammy na kuwavalisha kama wao…. tazama alafu uniambie mtoto gani kafanana sana na staa na alietokelezea pia.
Rihanna.
Adele.
Justin Timberlake.

Taylor Swift

Wednesday, February 13, 2013

TANESCO AND SYMBION POWER SIGNS MoU FOR A JOINT VENTURE IN 400MW MTWARA PLANT



TANESCO and Symbion Power today signed a Memorandum of Understanding for building and operating a 400MW power plant in Mtwara through a Public Private Partnership. The work will include the construction of a 650 km transmission backbone from Mtwara to Songea where it will be connected to the TANESCO national grid through a line that will be built from Makambako to Songea.

 This development will be phased and it will take three years from financial closure to completion. The first phase will involve increasing the existing capacity in Mtwara to meet the growing demand in the southern regions including Lindi and Mtwara. Engineering study work will commence in March.

TANESCO and Symbion have been in discussions since Symbion presented a proposal to TANESCO and the Ministry of Energy in September 2012. This has now led to the signing of the board-approved MOU that allows the two companies to form a Public Private Partnership and develop the project. It will take around 12 months to put the necessary financing in place before the three-year clock begins to tick.

Speaking at the signing of the MOU in Dar es Salaam, Paul Hinks, the Chief Executive Officer of Symbion Power said, “The south of this country has been starved of energy for decades and this has severely stunted its development. This project will succeed because it includes transmission lines that will feed the grid system. The transmission lines will be owned exclusively by TANESCO but they will be built as a part of the project.”

 “Symbion and TANESCO will be working with a number of international funding agencies, banks and private equity firms in 2013 to put the financial package together, many of whom have already expressed great interest in the project. We are hopeful that U.S. government agencies such as the U.S. Exim Bank and the U.S. Overseas Private Investment Corporation will show keen interest in the investment too.”

 “In the three years since Symbion came to Tanzania we have seen rapid development and improved network stability. Tanzania will in the future have an abundance of gas and it can become entirely self sufficient and even a regional exporter to countries that are not blessed with the fuel resources that are available in the country. The days of complete reliance on rain-driven hydro electric systems are gone and alternative sources of power need to be implemented to ensure that there is security of supply.”

 Speaking during the signing event, TANESCO’s Acting Managing Director Eng. Felchesmi Mramba said, “For many years the Southern part of the country has been suffering from poor power reliability due to the region not being connected to the National Grid. However, through this planned partnership, Lindi, Mtwara and Ruvuma will be connected to the National Grid. Connecting the Southern regions to the National grid will significantly improve reliability of the entire network. This is one of the ways TANESCO can benefit from the PPP arrangement whereby the Public and Private sector join forces to undertake projects that would otherwise be difficult to implement.”

BUNGE KUFUTA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA

Picture
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa bunge uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi ya kamati kuondolewa pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3 zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (Picha na Aron Msigwa)
Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilila akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge amesema Bunge linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja (LIVE) kupitia televisheni kwa  nia ya kukomesha vitendo vya baadhi ya Wabunge wanaokikuka kwa makusudi Kanuni za Bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila na hivyo kutoa picha mbaya katika jamii.

Akasema ili kurejeza maadili kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Akasema jamii imeendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi kutokana na kukiukwa kanuni hizo.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Ameahidi kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bunge pamoja na uandaaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge, huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuitumia ipasavyo ofisi yake kupata  taarifa sahihi za kuwasaidia katika uandishi.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU