Facebook Comments Box

Wednesday, February 13, 2013

BARUA YA JAMAL MALINZI YAGONGA MWAMBA

 
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tarehe 13 Februari 2013

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwajulisha wapenzi wa mchezo huu kuwa limepokea barua kutoka kwa Ndg. Jamal Malinzi ambayo inaomba kuangaliwa upya kwa maamuzi ya Kamati ya Rufaa za Uchaguzi ya TFF ya kuliondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea urais wa Shirikisho.
 

Barua hiyo ya tarehe 13 Februari 2013 ilielekezwa kwa mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Baada ya kuipata barua hiyo, Sekretarieti iliwasiliana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ambaye alielekeza kuwa Ndg. Malinzi alielekeza barua yake kwenye chombo ambacho hakikufanya uamuzi wa kuliengua jina lake na hivyo hakina mamlaka ya kuangalia upya suala hilo.
 

Mwenyekiti alishauri kuwa TFF imwandikie Ndg. Malinzi barua ya kumshauri kuwa aelekeze maombi yake kwenye chombo kilichofanya maamuzi kwa kuwa ndicho kinachoweza kuangalia upya maamuzi yake.
 

Sekretarieti pia imepokea maamuzi rasmi ya Kamati ya Rufaa za Uchaguzi ya TFF na imeshayawasilisha kwenye Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uchaguzi za TFF.

Angetile Osiah
Katibu Mkuu,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


YANGA YAINYANYASA AFRICAN LYON


 

 Mabingwa wa kombe la Kagame timu Young Africans leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa timu ya  African Lyon jumla ya mabao 4-0, katika mchezo uliofanyika jioni hii katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 36 na mabao 33 ya kufunga, iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo imefanikiwa kuzipata.
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na katika dakika 15 za kwanza washambuliaji wake Hamis Kiiza na Jerson Tegete walikosa nafasi za wazi za mabao ya mapema, kufuatia kutokua makini katika umaliziaji.
Jerson Tegete aliwaiunua mashabiki wa Yanga katika dakika ya 21 baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza kwa kichwa akimalizia pasi safi iliyopigwa na mlinzi wa pembeni David Luhende ambaye alipanda kuongeza nguvu mashambulizi.
Yanga iliendela kuutawala mchezo na hasa sehemu ya kiungo, ambapo Haruna Niyonzima, Athumani Idd Chuji, Frank Domayo waliweza kuitawala sehemu hiyo ya katikati hali iliyopelekea wachezaji wa African Lyon kuutafuta mpira kwa tochi.
Dakika ya 42, Jerson Tegete tena aliipataia Young Africans bao la pili kwa staili ya peke, baada ya kuupiga kwa kisigino mpira wa krosi uliokuwa umepigwa na Haruna Niyonzima na kumfanya mlinda mlango wa African Lyon Abdul Seif na walinzi wake wasijue cha kufanya.
Saimon Msuva alitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini mipira hiyo ilipowakuta wafungaji hawakua katika nafasi nzuri ya umaliziaji hali iliyopelekea kukosa mabao mengine ya wazi katika kipindi cha kwanza. 
 
 Kocha wa African Lyon, Salum Bausi, akiwa katikati ya uwanja akiwatuliza wachezaji wake kukubali kupigwa penati, waliyokuwa wakiigomea, huku wakimzonga refa.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 2-0 African Lyon.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo hali iliyopelekea kujipatia penati dakika ya 48 ya mchezo, kufuatia walinzi wa African Lyon kuzidiwa na kiungo Haruna Niyonzima hali iliyowapelekea kumcheza madhambi mchezaji huyo ndani ya eneo la hatari, mwamuzi aliamuru ipigwe penati ambayo iilipigwa na Hamis Kiiza ambaye alikosa penati hiyo.
Kocha wa Yanga Ernest Brandts alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, na Nizar Khalfani ambao walichukua nafasi ya Hamis Kiiza, Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Mabadiliko hayo yalizidi kuongeza kasi ya mashabuluzi langoni mwa African Lyon kwani dakika ya 70, Didier Kavumbagu aliipatia Yanga bao la tatu kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa African Lyon Obina Salamusasa kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Dakika ya 80 Nizar Khalfani aliipatia bao la  nne kwa ustadi mzuri wa umaliziaji, akimalizia pasi ya Said Bahanuzi ambaye aliwazidi ujanja walinzi wa African Lyon na kupiga krosi hiyo iliyowapita walinzi na mlinda mlango Juma Abdul.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 4 - 0 African Lyon

Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake  kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza washambuliaji wangu hawakuwa makini lakini kipindi cha pili timu ilibadilika sana hali iliyopelekea kuutawala mchezo kwa kipindi chote na kuongeza mabao mawili ya haraka.
Baada ya mchezo huu wa leo kikosi cha Young Africans kitaendelea na mazoezi yake kesho asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Azam FC februari 23 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar
 Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Jerson Tegete/Didier Kavumbagu 10.Hamis Kiiza/Sadi Bahanuzi, 11.Haruna Niyonzima
African Lyon: 1.Abdul Seif, 2.Yusuf Mlipili, 3.Sunday Bakari, 4.Ibrahim Job, 5.Obina Salamusasa, 6.Abdulehan Gulam, 7.Amani Kyata, 8.Mohamed Samata, 9.Idd Mbaga, 10.Bright Ike, 11.Adam Kingwande

Katika michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo, JKT Mgambo imeifunga Oljoro JKT mabao 2-0, Kagera Sugar imeifunga Coastal Union bao 1-0, Toto African imetoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Polisi Moro na Mtibwa Sugar imetoka suluhu na Ruvu Shooting.


TANZIA: SHEIKH NASSOR ABDALLAH BACHOO

UPDATE/TAARIFA MPYA

Waheshima  Taarifa Kamili ya Maziko ya Mpendwa Shekh wetu Nassor Bachu yatafanyika Kesho katika Msikiti wa Kikwajuni Saanne Asubuhi

Kwa taarifa ya jamaa wa marehemu waliitowa marehema amefarikia majira ya saa nne asubuhi ya yale, baada ya kuuguwa kwa muda mrefu,  marehemu alisafirisha Mjini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi.kwa kipindi alikuwa akipata matibabu katika hospitali za Mjini Dar. hatima marehemu  amerejeshwa Zanzibar na kuendelea na matibabu.

Shekh. Nassor alikuwa akipata matibabu kwa jamaa zake nje kidogo ya mji wa Zanzibar katika maeneo ya Chukwani hadi mauti yanamkuta leo asubuhi alikuwa chukwani Zanzibar.

 Maziko yatafanyika kesho katika msikiti wa Kikwajuni na kuzikwa Kijijini kwao Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi

Innaa lillahi wainnaa ilayhi raajiuun.

Sheikh Nassor Abdalla Bachoo ametangulia mbele ya haki.

Allahumma thaabit-hu biqauli thaabit. Allahumma gh-firlahu warhamhu waafihi waaf-anhu.

Sheikh Nassor Abdalla Bachoo hatosahaulika kamwe kwa mchango wake mkubwa katika elimu ya Uislamu na maendeleo ya Uislamu kwa ujumla ndani ya Afrika Mashariki na ulimwengu kwa jumla.

Kwa niaba ya Familia yangu natanguliza mkono wa ta’azia kwa familia ya sheikh, ndugu, jamaa na Waislamu wote kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika dini yetu tukufu ya Kiislamu.

Tunamuomba Allah Taala kwa utukufu Wake Ampokee sheikh miongoni mwa waja wake wema, Amsamehe madhambi yake na Amjazie penye upungufu. Ameen.

Tembelea bog: Miujiza-ya-quran na/au Facebook: Groups/Miujiza ya Quran
Kama kutakuwa na maswali tafadhali usisite kuwasiliana kwa email: miujizayaquran@gmail.com

Shukran

kitongoni.blogspot.com inaungana kuwaombeeni faraja nyote mlioguswa na msiba huu. Roho ya marehemu Sheikh Nassor Abdalla Bachoo ipumzike pema! AMIN!



TAARIFA YA KIFO CHA MSANII WA WANAUME HALISI


.

.
Taarifa ambazo millardayo.com imezipata muda mfupi uliopita ni kwamba msanii Baraka Sekela maarufu kama BK wa TMK Wanaume halisi amefariki usiku wa kuamkia leo, alikua amelazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa tatizo la moyo.

ANGALIA MAZOEZI YA SIMBA KUJIANDAA NA LIBOLO NA MIPANGO YA KUENDA UINGEREZA

Tizi kali likiendelea wakati Simba wakijiandaa kwa mechi  dhidi ya mabingwa wa Angola, C.R.Libolo kwenye mchezo wa awali na endapo watafuzu basi watakutana na El Merrikh ya Sudan  kwenye hatua ya 16 bora hapo mwezi Machi 15, 16, 17.
 Tizi likindelea

 Kocha msaidizi Jamhuri Kihwelu Julio akisimamia tizi

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya kukutana jana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.

 Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Short alisema ushawishi wa Malkia wa Nyuki umechangia yeye kutoa mwaliko huo na anaamini timu zote zitafaidika.

"Mazungumzo yetu na Rahma yalikuwa mazuri sana, nimefarijika na ninaamini mwaliko niliotoa utakuwa mwanzo wa uhusiano mzuri kwa kuwa mwanamama huyu amenishawishi," alisema.

Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu.

Awali Simba, ilijulikana kwa jina la Sunderland.


Tuesday, February 12, 2013

KAMA ULIKOSA MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS WA KENYA UANGALIE HAPA




RAIS KIKWETE ATAMBULISHA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NA KUMPOKEA JULIANA SHONZA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kuwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati kuu ya CCM ilkiyofanyika katika viwanja vya Makao makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waliokuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA.Kushoto anayevaa kofia ya CCM ni aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mtela Mwampamba na kulia ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA Bi Juliana Shonza.Weninge katika picha ni Katibu mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman Kinana(kulia) na kushoto ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula.(picha na Freddy Maro).


TFF WAOMBA YANGA WAWASHANGILIE SIMBA NA AZAM KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA



Release No. 026
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 12, 2013

WASHABIKI WAZIUNGE MKONO AZAM, SIMBA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaka washabiki wa mpira wamiguu kujitokeza kwa wingi wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simbazitakazocheza mechi za mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.Nguvu ya washabiki ni muhimu katika kuziweza timu hizo kufanya vizuri katikamechi hizo za nyumbani dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club Liboloya Angola.Azam itacheza Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katikamechi ya Kombe la Shirikisho wakati Simba itaikabili Club Libolo kwenyemechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika Jumapili. Mechi zotezitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

LYON, YANGA KUUMANA UWANJA WA TAIFA
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inamalizaraundi ya 16 kesho (Februari 13 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyejiAfrican Lyon dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mechi hiyo itakayochezshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoroinakutanisha timu zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo vinarawa ligi hiyo kwa pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na SalumBausi inakamata mkia ikiwa na pointi tisa tu.Nayo Toto Africans itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCMKirumba jijini Mwanza katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi JacobAdongo kutoka Musoma. Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wakuchukua watazamaji 20,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya MgamboShooting na Oljoro JKT.Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha waMtibwa Sugar ataiongoza timu yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo ambapo Mtibwa Sugar katika mechi yao iliyopita walichapwa mabao 4-1na Azam.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

USIWE NA HARAKA YA KUHUKUMU MAMBO

Katika dirisha lile la treni,ndani yake
Alikuwa kakaa mzee mmoja na kijana wake,
Ambaye alikuwa na makamu ya umri wa miaka 25.

Yule kijana akaanza kuonesha usoni mwake
alaza za furaha na mshangao.
Akatoa mkono wake dirishani,kisha akaurudisha
Haraka na kusema kwa sauti ya juu:
Baba angalia miti yote yakimbia kurudi nyuma!!

Yule mzee akatabasamu na kuonesha ya kwamba
Anaungana na mwanae katika furaha.

Kando yao walikuwa wamekaa wanandoa wawili.
Na wakisikiliza mazungumzo kati ya baba na mtoto.
Wakawa wakihisi aibu na kushikwa na mshangao,
Vipi kijana huyu mwenye makamo ya umri wa miaka 25
Anafanya vitendo kama vya mtoto mdogo???

Ghafla yule kijana akapiga kelele akisema:
Baba angalia umeme wa radi!
Angalia mawingu yanakwenda pamoja na treni!

Wanandoa wawili wakaendelea kushangaa!
Kulingana na mazungumzo na vitendo
Vya yule kijana.

Kisha mvua ikaanza kunyesha,na matone ya maji
Yakatua katika mkono wa yule kijana,ambaye
Alikuwa akionesha alama ya furaha katika uso wake.

Akapiga kelele kwa mara nyingine na kusema:
Baba mvua inavyesha !!! Na maji yamegusa mkono wangu !!!
Baba angalia !!!

Mara hii wanandoa walishindwa kujizuia,
Wakamuuliza yule mzee:
Mzee kwa nini humpeleki kijana wako hospitalini,
Ili aweze pata matibabu???

Yule mzee akawajibu:
Hivi sasa ndio twatoka hospitalini,
Na mwanangu ndio ameanza kuona kwa
Mara ya kwanza katika maisha yake.
***************­***************

Siku zote usiwe ni mwenye kutoa
Majibu ya mambo mpaka ujue uhakika wake.
Na daima uwe ni mwenye dhana nzuri
Kwa ndugu zako.


WAJUMBE 14 WA KAMATI KUU YA CCM

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha siku mbili Februari 10 na 11, 2013 kilichofanyika mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine kimeridhia uteuzi na kufanya uchaguzi wa Wajumbe 14 wa Kamati Kuu yake.
 

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imeridhia uteuzi wa Dokta Salim Ahmed Salim kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu kupitia nafasi 10 za uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM.
 

Wajumbe 14 waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:-


Wajumbe wa Kamati Kuu - Bara

1. Ndugu Pindi Chana

2. Ndugu Adam Kimbisa

3. Ndugu William Lukuvi

4. Dokta Emmanuel Nchimbi

5. Ndugu Jerry Slaa

6. Profesa Anna Tibaijuka

7. Ndugu Stephen Wassira
 

Wajumbe wa Kamati Kuu - Zanzibar.

1. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha

2. Ndugu Hussein Mwinyi

3. Profesa Makame Mbarawa Mnyaa

4. Dokta Salim Ahmed Salim

5. Ndugu Maua Daftari.

6. Ndugu Samia Suluhu Hassan

7. Ndugu Hadija H. Aboud


MADAKTARI KUPIGA SIMU BURE

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid(katikati),Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kulia) Mkurugenzi wa Shirika la Switchboard Ali Block wakionesha mabango ikiwa ni inshara ya uzinduzi wa kuwawezesha wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure,huduma hiyo inatolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Switchboard ili kurahisisha huduma za kiafya mahosipitalini.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid (kushoto)Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (katikati)pamoja na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim,wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kuwawezesha wahudumu wa Afya na madaktari kuwasiliana kwa simu za mkononi bure huduma hiyo inatolewa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Switchboard ili kurahisisha huduma za Afya mahosipitalini.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU