Jengo la Coco Plaza ambalo kuna Ofisi za CRDB.

Wateja wakipata huduma

Kaimu
Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei (kushoto)
akitoa maelekezo ya huduma mbalimbali wanazotoa katika tawi hilo jipya
kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai. Tawi hilo limefunguliwa
hivi karibuni katika jengo la Coco Plaza jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Nasib Kalamba.

Ofisa
Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba (katikati) akitoa ufafanuzi kwa
mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai katika
tawi jipya la benki hiyo lililopo katika jengo la Coco Plaza jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo, Godlisten Mtei.

Ofisa
wa benki ya CRDB, JacqlineSawe akitoa maelekezo kwa mteja wa benki hiyo
katika tawi la Oysterbay lililopo katika jengo la Coco Plaza jijini Dar
es Salaam.

Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba
(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa
Elimu, Joseph Mungai katika tawi jipya la Oysterbay jijini Dar es
Salaam.

Maofisa wa benki ya CRDB wakiandikisha wateja wapya katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam.

Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei (kushoto) akitoa maelekezo ya huduma mbalimbali wanazotoa katika tawi hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai.

Ofisa wa benki ya CRDB, George Abraham kisaini baadhi ya nyaraka za kibenki.
BENKI
ya CRDB, imefungua tawi jipya Osysterbay jijini Dar es Salaam ikiwa
na lengo la kuwafikia wateja wake, ambapo takribani wateja 400 wamekuwa
wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo.Tawi hilo
limeanza kufanya kazi hivi karibuni, ambapo limeonekana kuwa ni msaada
mkubwa kwa wakazi wa Osysterbay na maeneo ya jirani.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Kaim Meneja wa CRDB,
Godlisten Mtei alisema lengo kubwa la kupeleka tawi hilo ni kuwapa
huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo hilo. Alifafanua
kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa ni mkombozi kwa wateja
mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na watu
mbalimbali. “Tawi letu linatoa huduma zote za
kibenki, na tunazidi kuwakaribisha wateja wetu ili wajionee huduma bora
zitolewazo na benko yetu na pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za;
Mashine ya kutoa na kuweka fedha (ATM) ambayo hufanyakazi masaa
24”alisema.
Mtei alitaja huduma zingine kuwa ni
pamoja na TemboCardVisa, Akaunti ya Hundi na ya watoto inayojulikana
kama Junior Account pamoja, Malikia akaunti ambayo ni maalum kwa
wanawake na Akaunti ya Akiba. Hata hivyo aliongeza kuwa,
tawi hilo litakuwa likitoa Akaunti ya Tanzanite, huduma za mikopo
mbalimbali na huduma za bima ili kuzidi kuwapatia huduma bora wateja
wao.Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi
limekuwa likitoa huduma ya kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi
(SimBanking), pamoja na Akaunti ya Wanafunzi ambayo inafahamika kama
Scholar Account.
Meneja huyo aliwataka Wananchi na
wateja wapya kutumia tawi hilo pekee katika eneo hilo ili kupata huduma
za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye
matawi yaliyo mbali. Katika hatua nyingine Meneja Mauzo wa benki
hiyo Richard Joseph alisema, katika harakati za kufanikisha wananchi
wanajiunga na benki hiyo wameamua kuweka tawi katika eneo la Namanga
jijini Dar es Salaam ambapo kwa siku zaidi ya watu 70 wanaojiunga na
benki hiyo.