Facebook Comments Box

Monday, February 4, 2013

LINDA IKEJI AVUTA MKOKO MPYA

Anaitwa Linda Ikeji blogger Mnigeria ambae Naija wanamuita #Mchapakazi japo amehusishwa kwenye kashfa ya kuwa kwenye dini inayomuabudu shetani, ukiachia mbali hiyo kashfa ni kwamba hili gari alilonunua ni Infinity Fx 35 Suv YA 2011 ambayo thamani yake ni Naira milioni 8 za Nigeria.
Baada ya kutoa uthibitisho wa ununuzi wa hili gari, blogger maarufu Linda ambae pia ni mfanyabiashara amesisitiza kila mmoja kujipanga na kujituma kwenye kila anachowaza kwamba ni msingi wa maisha yake.
.
.
.
.
.
.


Sunday, February 3, 2013

HATIMAYE KITALE APATA JIKO

www.kitongoni.blogspot.com 
Yule msanii wa filamu na vichekesho Hamis Kitale maarufu kama kitale leo mepata baraka ya kuvuta jiko yaani kuoa. Msanii huyo ambae alipata umaarufu kwa kuigiza kama teja. Ameachana na kambi ya wasela kwa kuoa leo.




MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM KIGOMA LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM},Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete leo wameongoza Matembezi ya Mshikamano yaliyoanzia kwenye eneo la Mnarani na kuishia kwenye ofisi za CCM mkoani Kigoma,asubuhi ya leo. Matembezi hayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,Rais Jakaya Kikwete {wa pili kushoto}na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi {CCM} yanayofanyika leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.Matembezi hayo hayo yamehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla.
























HUU NDIO UHARIBIFU ULIOLETWA NA MOTO KWENYE GHOROFA LA PPF TOWER





PAMOJA NA KUPEWA PENATI YA KUTATANISHA SIMBA WASHINDWA KUNGURUMA

.Dk 90 mpira umeisha. FULL TIME SIMBA 1-1 JKT

Dk 85 Simba inafanya mabadiliko ametoka Ramadhan Chombo ameingia Kiggi Makassy.

Dk 86 Penalty, Simba inapata penalti katika mazingira ya kutatanisha. Shomarh Kapombe anapiga anakosa.

Dk 84 JKT imefanya mabadiliko ametoka Amos Mgisa ameingia Samwel Madenge

Dk 74 Simba imefanya mabadiliko ametoka Abdallah Seseme ameingia Haruna Moshi Boban.

Dk 70 Timu zinashambuliana kwa zamu, JKT wanaonekana wamezinduka.

Dk 62 Gooo..! Nashon Matali anaifungia JKT bao la kusawazisha akiunga pasi ya Mgosi. Simba 1-1 JKT

Dk 60 JKT imefanya mabadiliko, ametoka Emmanuel Pius ameingia Amos Mgisa.

Dk 54 JKT imefanya mabadiliko, ametoka Credo Mwaipopo ameingia Mussa Holoa.
Dk 51 Simba wanapiga kona na beki Damas Makwaya anaokoa mpira katika mstari wa goli. Simba 1-0 JKT. Simba imefanya mabadiliko, ametoka Mrisho Ngassa anaingia Abdallah Juma.

Dk 47 Timu zinashambuliana kwa zamu Simba wakiendelea kuongoza.

DK 45: Mpira mapumziko Simba 1 - 0 JKT


 Dk 39 Simba inatawala mchezo hasa kiungo na ushambuliaji japokuwa JKT nao wanaonekana kutafuta bao la kusawazisha. Simba 1-0 JKT

DK 18: Simba 1 (Kiemba) - 0 Jkt Ruvu.

Dk 9 Mussa Mgosi wa JKT anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa Juma Kaseja wa Simba: Simba 0-0 JKT.   

Mpira umeanza Simba 0 -0 JKT

First Eleven of Simba SC vs JKT Ruvu Taifa leo
1- Juma Kaseja
2-Haruna Shamte
3-Paul Ngalema
4-Komalbil Keita
5-Shomari Kapombe
6-Abdallah Seseme
7-Haruna Chanongo
8-Mwinyi Kazimoto
9-Mrisho Ngassa
10-Amri Kiemba
11-Ramadhan Chombo


JKT RUVU: Shaaban Dihile, Credo Mwaipopo, Kessy Mapande, Kisimba Luambano, Damas Makwaya, Jimmy Shoji, Hussein Bunu, Nashon Matali, Mussa Mgosi, Zahoro Pazi, Emmanuel Pius

Friday, February 1, 2013

WEMA SEPETU ACHUKUA FOMU ZA KUSHIRIKI BBA 2013

Mwanadada Wema Sepetu ametia maguu kwenye ofisi za Mult Choice Tanzania na kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki shindano la Big Brother Africa katika mchakato huu wa awali



PAKITI YA VODKA YAKUTWA NDANI YA TONIC WATER YA COCA COLA

Picture
Hii ni aina ya soda ya Tonic Water ya kampuni ya Coca Cola, Mbeya ikiwa na kiroba cha pombe kali aina ya Vodka
BAADHI ya wananchi ambao ni watumiaji wa vinywaji baridi Jijini Mbeya wameyalalamikia baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji wa bidhaa hizo kwa kutozingatia usalama wa watumiaji.

Malalamiko hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni mwananchi mmoja aliyoomba kuhifadhiwa jina lake kununua soda aina ya Tonic Water inayotengenezwa na kampuni ya Coke kukutwa ikiwa na karatasi la pombe kali aina ya Vodka.

Soda hiyo ikiwa mpya bila kufunguliwa ilikutwa katika duka moja eneo la Simike baada ya mteja huyo kuuiwa kwa lengo la kiutuimia lakini kabla ya kuifungua ndipo laipogundua uchafu huo.

Kufuatia hali hiyo, Mwandishi wa habari hii  alipewa taarifa na mhusika ambapo walienda moja kwa moja hadi kiwandani Coke eneo la Iyunga Jijini Mbeya na kupokelea na Meneja mauzo wa wilaya (Area Sales Manager). Baada ya kupokelewa na kuelezwa hali iliyotokea, Meneja huyo aliwapeleka waandishi kwa kitengo cha ubora wa bidhaa ambao bila woga walisema tuwaachie soda hiyo baada ya kuridhishwa kuwa ni mpya na inatoka kiwandani hapo.

Walidai waachiwe soda hiyo ili kuifanyia uchunguzi wa kimaabara katika uchunguzi utakafanyika kwa wiki moja hali iliyoleta wasiwasi kwa walalamikaji huku wakihoji, “uchunguzi gani ufanyike ili hali uchafu unaonekana?”

Aidha, walidai kuwa pamoja na kukataliwa kubakishwa kwa soda hiyo, walisema mlalamikaji hatanufaika na chochote ikiwa na kiwanda kutoathirika na tatizo hilo licha ya kuhusika na kuzalisha bidhaa yenye uchafu.

Hali kama hizo zimekuwa zikiwaathiri watumiaji wa vinywaji hivyo hasa wanaotumia  nyakati za usiku muda ambao si rahisi kwa mteja kugundua hali ya uchafu katika vinywaji.

Hata hivyo, mhusika aliyepatwa na janga la soda hiyo kutoka kiwanda cha Coke aliiomba mamlaka zinazohusika kufuatilia hali ya usafi wa vifaa vya kubebea vinywaji hivyo kabla ya kupelekwa sokoni kwa watumiaji ili kunusuru afya za wananchi.



WAZIRI MKUU AKIWAKILISHA BUNGENI TAARIFA YA MGOGORO WA GESI YA MTWARA




DR MIGIRO AFUNGUA MSHINDANO YA MPIRA WA PETE MKOANI KIGOMA


 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akisalimiana na mmoja wa wachezaji wa timu ya Mwandiga Queens wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.


 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akizungumza na wachezaji wa timu ya Shule ya Sekondari ya Mwananchi  wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.



 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wachezaji wa timu za Mwandiga Queens,Lake Tanganyika na Mwananchi muda mfupi kabla ya kufanyika wakwa uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.

 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akirusha mpira golini ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mashindano ya mchezo wa mpira wa pete (Netball) maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi,yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3,Februari kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Mkoani Kigoma.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU