Facebook Comments Box

Wednesday, January 23, 2013

RAISI JAKAYA KIKWETE AMALIZA ZIARA NCHINI UFARANSA

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemaliza ziara ya kikazi  ya siku tano (5) rasmi leo tarehe 23/01/2013 nchini ufaransa. Picha zifuatazo zinaonesha matukio yote ya Ziara hiyo.


Picture

WAZIRI: WAKALA WA KUSIMAMIA UENDELEZAJI WA MJI WA KIGAMBONI


 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africajijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza rasmi kuanzishwa kwa Wakala wa kusimia maendeleo ya mji wa Kigamboni inayoitwa Kigamboni Development Agency (KDA) Kushoto ni Christian Mwangaja Kaimu Kamishna mambo ya Ardhi na katikati ni Sellasie Mayunga Upimaji na Ramani.

1. Serikali imedhamiria kujenga Mji Mpya Kigamboni katika Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, Dhana ya mji mpya Kigamboni ni kuwa na mji wa kisasa ambao ni kitovu cha kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jiji la Dar es Salaam ili liweze kushindana na miji mingine duniani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii na kukuza ajira, hasa kwa vijana. Ujenzi wa mji mpya ni hatua mojawapo katika mkakati wa serikali wa kukabiliana na changamoto za ukuaji wa jiji la Dar es Salaam.

 2. Tarehe 18 January, 2013 Serikali ilianzisha kisheria wakala maalumu, Kigamboni Development Agency (KDA) itakayosimamia uendelezaji wa Mji Mpya Kigamboni kama Mamlaka ya Upangaji Mji (Planning Authority). Eneo litakalosimamiwa na KDA lina ukubwa wa hekta 50,934 na linahusisha Kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji na Pemba Mnazi . katika kusimamia uendelezaji huo, KDA itaongozwa na mpango kabambe. Rasimu ya mpango huo imekwisha andaliwa kwa baadhi ya kata.

 3. Uendelezaji wa Mji Mpya utagharimiwa na Serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutumia fedha zilizo ndani na nje ya bajeti rasmi ya serikali. Utaratibu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (Public Private Partnership) utatumika. Aidha, mbinu za kisasa za kupata fedha kama vile kuuza hisa na kutoa hatifungani (bonds) zitatumika.

4. Ili kutekeleza kusudio la kuendeleza eneo la Kigamboni, hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na:-
  • Kutoa elimu kwa umma juu ya manufaa ya kuendeleza eneo la Kigamboni na taratibu za uendelezaji.
  • Kutafuta fedha za kutosha kutekeleza mradi.
  • Kupima maeneo husika na kuyaandaa kwa ajili ya uendelezaji.
  • Kujenga nyumba mpya za kuishi kwa ajili ya kuwahamishia wananchi ambao makazi yao yataathiriwa na ujenzi wa Mji Mpya; na
  • Kufanya uthamini wa mali na kuwafidia wananchi watakaolazimika kahama kutokana na ujenzi wa mji.

5. Muundo wa KDA unatokana na Sheria ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997. wakala itaongozwa na Mkurugenzi Mtendaji na Wakurugenzi sita ambao watakuwa Wakuu wa Idara, KDA itasimamiwa na Bodi ya Ushauri pamoja na Baraza la Ushauri ambalo  litakuwa na wajumbe wanaowawakilisha wadau wote, hususan Wabunge na Madiwani waeneo litakaloendelezwa na KDA.

6. Matokeo ya utekelezaji wa Mpango kabambe wa Mji Mpya ni kama ifuatavyo:
  • Kuwa na mji uliopangwa kwa kiwango cha kimataifa utakaokuwa mfano wa kuigwa na miji mingine nchini.
  • Kupunguza ujenzi holela;
  • Kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na shughuli za kiuchumi na kijamii kama vile za viwanda , hoteli, utalii, biashara, elimu, ofisi, afya na vituo vya michezo;
  • Kupunguza msongamano wa magari na huduma za kiuchumi na kijamii katikati ya jiji la Dar es Salaam;
  • Kuongezeka kwa thamani ya ardhi katika maeneo ya mji kutokana na kuboreshwa kwa miondombinu ya barabara, maji na umeme itakayowezesha kukuza biashara, ujenzi wa majengo na viwanda.
  • Kuhamasisha uwekezaji ili kuongeza ajirra, has kwa vijana; na
  • Wananchi  wengi wataweza kumiliki nyumba katika maeneo yaliyopangwa na kutumia nyumba zao kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.


Taarifa na elimu kwa umma kuhusu hatua zote za uendelezaji wa mji  zitaendelea kutolewa na Wizara pamoja na KDA kwa njia mbalimbali (k.m. kupitia mikutano maalum, vyombo vya habari na vipeperushi).

 Prof. Anna K. Tibaijuka (MB)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
23 January, 2013



TEGETE AFUNGA KWA PENATI HUKU YANGA IKIIFUNGA BLACK LEOPARDS TENA

Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja
Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90 kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.
Nginja nginja tuu
Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kumalizika


MAGAZETI YA LEO 23/01/2013

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.


KAULI YA CHADEMA KUHUSU MANENO YA NAPE NNAUYE



Mkurugenzi wa Sera na Mafunzo wa CHADEMA, BENSON KIGAILA

CHADEMA wamesema kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye kwamba Chadema kitakufa kutokana na kuwa na Sumu ya Ubaguzi haina ukweli wowote, na wamemtaka kiongozi huyo kutafakari zaidi kauli hiyo kwa maslahi ya Chama chake.

Mkurugenzi wa Sera na Mafunzo wa CHADEMA BENSON KIGAILA anasema CHADEMA haiwezi kufa kwa dhana iliyozungumzwa na Nape na badala yake Chama hicho tawala ndicho kinachoweza kufa kutokana na changamoto ikiwemo ufisadi.

Akikaririwa Benson amesema “anachodai yeye kwamba kuna ubaguzi ndani ya CHADEMA, tunataka tumwambie kwamba chama cha siasa kinakufa pale kinapoacha msingi wake, dhamiri yake na majukumu yake ya kusimamia malengo na maslahi ya Umma”

Kwenye mistari mingine Chadema imemtaka Naibu Katibu wa CCM Mwigulu Nchemba kutoa ushahidi wa kauli aliyoitoa hivi karibuni kwamba Chadema  imekuwa ikipanga mipango ya mauaji.




CHRIS BROWN NA RIHANNA WAKWARUZANA TENA


 
 Chris Brown na Rihanna ndani ya Swimming Pool
 
 

Nyumba ya Chris Brown iliyopo Holiwood Marekani

Polisi Hollywood Marekani wanamtafuta mwanaume ambae aliwafanya wakimbie spidi mpaka kwenye jumba la mwimbaji staa Chris Brown baada ya mwanaume huyo kuripoti habari za kutisha kwa alichoshuhudia nyumbani kwa Chris Brown.
Kwa mujibu wa CME, huyu mwanaume akijidai ni shuhuda alipiga simu kuomba msaada polisi baada ya kudai kashuhudia ugomvi wa mwanamke na mwanaume ukiendelea kwenye nyumba ya Chris Brown na baadae risasi zikapigwa baada ya majibizano ya mdomo kuzidi.

Kwa mujibu wa polisi ambao walikimbia spidi kuokoa hiyo hali kuendelea, hakuna chochote kilichotokea nyumbani kwa Chris Brown ambae hata hivyo hakuwepo nyumbani na wala hakuja tokea tukio kama hilo kwenye huo mtaa ndio maana kwa sasa wanachunguza ni nani alipiga simu na akawazingua kwa kuwapotezea muda na mafuta.

Huyu jamaa alikua anamaanisha ugomvi wa mwanamke na mwanaume yani ni Rihanna na Chris Brown ambao wanadaiwa kurudiana mapenzini sasa hivi baada ya kuachana kwa kesi ya Chris Brown kumpiga Rihanna kwenye penzi lao la mwanzo.


MATOKEO YA MECHI ZA AFCON 22 JANUARI, 2013

Tunisia

Algeria.


.
Ivory Coast.

Togo




Tuesday, January 22, 2013

KADO KUICHEZEA COAST UNION MZUNGUKO WA PILI







Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia maombi ya usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wengine waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah Seif, Malika Ndeule na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, Njaidi Mohamed na Mahmoud Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed kayi na Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin Selemani, Shaibu Nayopa, Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami Mnyangamala, Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim, Chacha Marwa, Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward Mzeru na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius Mrope (Kagera Sugar).
Rajab Mohamed, Zakayo Joseph, Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro Pazi- kwa mkopo, Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT Ruvu), Moaka Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto Africans).
Obadi Mungusa, Juma Seif, Yusuf Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa mkopo, Buya Jamwaka, Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel Dhaila (Simba).
Rashid Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji Martin Mlolere aliyeombewa usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji amekataliwa kwa vile taratibu za uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya Majimaji.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
T.F.F


Monday, January 21, 2013

MWANACHUO WA ST JOHN UNIVERSITY DODOMA AUWAWA KINYAMA

 
 
JESHI la polisi mkoani Dodoma limeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa kinyama kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima na watu wasiojulikana.
Marehemu Lidya mwenye umri wa miaka 57 anadaiwa kuuawa siku ya jumapili hii majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa maeneo ya chuo hicho chenye wanafunzi 5500
akiwa anarejea nyumbani baada ya masomo ya jioni.
Ni simanzi,vilio,huzuni na majonzi katika vyunga vya chuo hiki kufuatia tukio hili la kusikitisha ambalo linadaiwa kuyaweka katika mashaka na wasiwasi mkubwa maisha ya wanafunzi hawa.
Licha ya kulitupia lawama jeshi la polisi baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa baada ya kufikwa na mkasa huo uliositisha safari ya maisha yake mwili wa marehemu Lidya uliharibiwa vibaya na mnyama asiyejulikana kwa kunyofolewa macho,masikio,pua,mguu na viuno vingine.
Prof.Gabriel Mwaluko ni makamu mkuu wa Chuo na Karimu Meshack ni afisa habari ambao kwa pamoja wanaelezea kilichorjiri.
Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo Kamanda wa mkoa ACP David Misime anawataka wakazi wa mkoa huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.
Wakati huo huo Kamanda Misime anasema msako mkali umeanza wa kuwatia nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwa ajili ya hukumu.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU