Monday, January 21, 2013
ATCL KUANZA SAFARI ZAKE ZA DAR KIGOMA KESHO
Wahandisi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha ndege yao aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilipata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida.
Matengenezo hayo yanafanyika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani.
Uongozi wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013.
ANGALIA PICHA ZA MTOTO ALIEZIKWA MZIMA NA KUFUKULIWA NA KUKUTWA MZIMA
Mama mmoja nchini Nigeria ameamua kumzika mtoto wake akiwa hai. Baada ya taarifa kupatikana polisi walienda na kuamua kufukua. Baada ya kufukua walimkuta mtoto huyo na kumkimbiza hospitali aliposafishwa mtoto huyo alikutwa hai.
HALMASHAURI YA KIGOMA KUSOMESHA WATOTO WOTE WANAOSHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
Ofisa Elimu Shule ya Msingi wa
Manispaa ya Kigoma Ujiji, Shaaban Bane aliyasema hayo wakati wa kuwasafirisha
watoto wanane waliotambuliwa kwenda Kasulu kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa
mchakato huo.
Bane alisema baada ya kufika kwenye
manispaa hiyo, aligundua tatizo la watoto wengi wadogo wenye ulemavu kutumika
kama vitega uchumi na familia zao kwa kuomba fedha mitaani badala ya kwenda
shuleni.
Kimsingi alisema kuwa hiyo inaonesha
kuwa uduni wa kipato (umasikini) wa familia hizo ambazo haziwezi kuwapeleka
watoto hao shuleni na kwamba wao kama Serikali wameona wachukue jukumu la
kuhakikisha watoto hao wanapata haki yao ya kupata elimu.
Kwa sasa, Ofisa Elimu huyo alisema
kuwa jumla ya watoto wanane wamepatikana kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa
ya Kigoma Ujiji na mchakato wa kuwafanya wajiunge na shule maalumu ya Kabanga
wilayani Kasulu umekamilika na jana walisafirishwa kuelekea huko.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma
Ujiji, Alfred Luanda alisema wazazi wanalo jukumu la kuhakikisha watoto wao
wanapata elimu badala ya kuchukulia ulemavu wao kama kigezo cha kuwafanya wao
ni masikini na kuanza kuzunguka mitaani kuomba fedha kwa wasamaria wema.
UKUTA WA STENDI YA UBUNGO WAANGUKA NA KUHARIBU VIBAYA MAGARI YA WATU LEO HII
Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal
umeangukia magari zaid ya 19 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo
bajaji tatu,yaliyokuwa yamepaki
eneo ambalo hutumika kupaki wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeeleza
kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa
kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
umeangukia magari zaid ya 19 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo
bajaji tatu,yaliyokuwa yamepaki
eneo ambalo hutumika kupaki wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeeleza
kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa
kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari,ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi.
Si Magari tu,hata bajaji pia zimeathiriwa vibaya kama uonavyo pichani
Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Afande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi
ZITTO AITIKISA SERIKALI KUHUSU GESI
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA)
Kwa wiki ya tatu mfululizo kumekuwa na malumbano kuhusiana na suala la ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. Kumekuwa na madai yenye nguvu ya hoja kutoka kwa wananchi wa Mtwara dhidi ya porojo kutoka kwa viongozi wenye dhamana ya kujibu madai haya ya watu wa Mtwara. Watu wa Mtwara kwa umoja wao na kwa kuungwa mkono na viongozi wa dini zote wamekuwa wakitaka Serikali ifikirie upya suala la mradi wa ujenzi wa Bomba la gesi na badala yake kujenga mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara na kusafirisha umeme huo kwenda maeneo mengine ya nchi. Kwenye moja ya maandishi yangu (Serikali iwasikilize watu wa Mtwara) nimeshauri kuwa Taifa liwe na gridi nyingine ya Taifa ambayo itatokana na Gesi tu na ianzie Mtwara.
Ikumbukwe kwamba katiba ya nchi, ibara ya 9 katika mabano J inataka mamlaka ya dola na vyombo vyake vyote kuhakikisha ya kwamba shughuli zote za kiuchumi zinaendeshwa kwa namna ya kwamba pasiwe mrundikano wa utajiri au shughuli za uzalishaji kwa watu wa chache. Katiba inaendela kwa kuelekeza kwamba uchumi wa nchi upangwe katika uwiano sawia (9, d). Watu wa Mtwara wanatekeleza matakwa haya ya katiba kwa kukataa mrundikano wa shughuli za kiuchumi wa nchi na utajiri wa nchi kua kwenye mikoa michache na hasa mkoa wa Dar-Es-Saalam.
Serikali imekuwa ikitoa majibu ya porojo na kuwatusi watu wa Mtwara na kama ilivyozoeleka Rais Jakaya Kikwete na Mawaziri wake wamekuwa wakisema suala la Mtwara linatumika na wanasiasa kujitafutia umaarufu. Inasikitisha sana kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwaambia mabalozi wa nchi za kigeni waliopo hapa nchini kuwa yanayoendelea mkoani Mtwara yanachochewa na Wanasiasa tuliosimama na wananchi wanaodai haki ya kufaidi utajiri wa nchi yetu. Rais Kikwete na Mawaziri wake wameshindwa kabisa kuonyesha uongozi katika suala hili na hatimaye kuhatarisha umoja wa kitaifa.
Kwa udhaifu wa serikali na tabia ya kutafuta mchawi badala ya kutatua tatizo la msingi, wananchi wameendelea kukutana na hata wengine sasa kuanza kusambaza ujumbe wa kukata kipande cha nchi na kuanzisha Jamhuri ya Kusini. Nimeona kwenye mabango ya mkutano wa hadhara uliofanyika 19/1/2013 wananchi wakibeba mabango yanayoaishiria kuchoka kuwa sehemu ya Tanzania na kuanzisha Jamhuri ya Makonde kuanzia jiwe la Mzungu wilayani Kilwa mpaka mto Ruvuma. Haya yanatoka na kiburi cha Serikali kujishusha na kuwasikiliza wananchi wanao dai haki yao ya kikatiba.
Ni Serikali iliyokosa uhalali wa kutawala inayoweza kudharau hisia hizi za wananchi. Serikali ielewe kwamba kamwe haitaweza kulinda kila nchi ya bomba hili iwapo italijenga kwa nguvu. Badala ya kuzungumza na vyombo vya habari Serikali ifanye mazungumzo na wananchi wa Mtwara na kukubaliana na matakwa yao. Kitendo cha Serikali kung’ang’ania msimamo wake dhidi ya watu wa mtwara ni kitendo kinacho weza kuipasua nchi na hivyo kwenda kinyume na masharti ya katiba ibara ya 28 ambayo inasema: “kila raia ana wajibu wa kulinda uhuru wa nchi, uhuru mamlaka na umoja wa taifa.”ibara ya 28, 1.
Inawezekana Serikali inaogopa kuvunja makubaliano na Wachina ya mkopo wa dola za kimarekani 1.2 bilioni ambao imeuingia bila hata kushirikisha Bunge. Inawezekana Serikali na hasa watendaji wa Serikali waliojadili mkopo huu wameshapata chao na hivyo kuogopa kusikiliza madai halali ya wananchi. Lakini yote hayo hayawezi kuwa zaidi ya Umoja wa nchi yetu. Hatuwezi kukubali nchi yetu ipasuke vipande vipande kwa sababu tu ya kulinda mkataba wa bilioni 1.2 tuliokopa China, ambayo serikali inang’ang’ania.
Tunafahamu kwamba ubalozi wa China umeandika barua serikalini kuwaondoa raia wa China waliopo Mtwara kwa hofu ya maisha yao. Serikali inaficha ukweli huu kama ilivyoficha ukweli kwamba Naibu Waziri wa Nishati na Madini bwana George Simbachawene alifukuzwa na wananchi wa Mtwara alipokwenda hivi majuzi. Serikali itaficha ukweli mpaka lini? Lazima tupate majawabu.
Kwanza Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa Bomba hili. Kamati ya Bunge ya POAC ilipokuwa inapitia mahesabu ya TPDC iliomba mkataba na kwa mshangao mkubwa wabunge wakaambiwa Mkataba haupo TPDC bali upo Wizarani. Kwa nini Mkataba huu wa matrilioni ya Fedha unafichwa? Mkataba huu ulisainiwa pamoja mikataba mingine 2, mmoja wa kujenga nyumba za wanajeshi wa thamani ya dola za kimarekani 400 milioni na mwingine wa mawasiliano jeshini wa dola za kimarekani 110 milioni, na mikataba yote mitatu imesainiwa kimya kimya bila kushirikisha wananchi kupitia Bunge. Lazima mikataba yote hii iwekwe wazi.
Pili, Mkataba huu uchunguzwe kama unalingana na thamani ya fedha maana kwa utafiti wa awali inaonyesha kuwa bei ya ujenzi wa bomba imepandishwa maradufu. Wastan wa kujenga bomba la gesi duniani ni dola za kimarekani 1.2 milioni kwa maili moja. Mradi huu wa Tanzania utagharimu dola za kimarekani 2.2 milioni kwa kilomita moja (maili 1 ni sawa na kilomita 1.6).
Tatu, Serikali ibadilishe Mkataba huu kuwa wa mkopo wa kujenga Mitambo ya kufua umeme Mtwara na ujenzi wa Msongo wa Umeme kama gridi ya pili ya Taifa. Kwa sasa Tanzania ina gridi moja ambayo inabebwa na bwawa la Mtera linalo tegemea mto Ruaha ambao hivi sasa unakauka miezi 5 katika miezi 12 ya mwaka. Ni dhahiri kwamba kwa usalama wa Taifa na hata kwa gharama Nchi itafaidika zaidi kwa kujenga gridi nyingine kutokea Mtwara badala ya kusafirisha gesi kuja Dar-Es-Salaam.
Serikali haitashinda vita hii kwa kuzusha kwamba ama wanasiasa wanaopinga wanatumika na makampuni mengine au kwa mataifa ya magharibi kutaka kuvuruga nchi. Serikali ijitazame yenyewe. Bila kufanya hayo tunayo pendekeza hapo juu, wananchi wataendelea kupigania hako yao. Hii ni vita ya uwajibikaji. Wananchi wanataka kufaidika na rasilimali za nchi yao. Kwa vyovyote vile upande wa wananchi utashinda. Vita ya uwajibikaji kwenye rasilimali za nchi sio ya vyama vya siasa, ni vita ya wananchi. Chama cha siasa kitakachokwenda kinyume na matakwa ya wananchi, kinajichimbia kaburi.
–
Zitto Kabwe
Sunday, January 20, 2013
BARABARA YA LINDI MTWARA SI SHWARI
NSSF YAANZA KUUZA NYUMBA ZAKE ZA KIBADA KIGAMBONI
Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yacoub Kidula (kulia) akimkabidhi funguo ya
nyumba, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid
Mahmoud Hamid baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika
eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es
Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Mkurugenzi wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Yacoub Kidula akiangali akikagua nyumba ya shirika hilo kabla ya kuikabidhi kwa mnunuzi wa nyumba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Baadhi ya nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
zilizopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada
Kigamboni jijini Dar es Salaam.
POLISI LINDI YAZUIA MAANDAMANO YA GESI YALIOANDALIWA NA VYAMA VYA SIASA
JESHI la Polisi mkoani Lindi,limezuia kufanyika kwa maandamano ya
kuunga mkono majirani zao wa Mtwara,kupinga kusafirishwa kwa njia ya
bomba la gesi asilia,kutoka mkoani humo kupelekwa Jijini Dar es salaam
kwa ajili ya kufufua umeme utokanao kwa rasilimali hiyo.
Kwa mujibu wa barua kutoka Ofisi ya Jeshi hilo,ambayo inaonyesha
kukosewa kwa mwezi na mwaka,yenye kumbukumbu LND/271/VOL.1/17 ya
Decemba 17/2012,na mwandishi wa habari hizi kupata nakala yake,na
kusainiwa na Kamanda George Mwakajinga,imepelekwa kwa vyama vinne vya
siasa.
Vyama vilivyopelekewa barua za zuio la maandamano hayo ni pamoja na
Chama cha mapinduzi (CCM), (CUF), CHADEMA na NCCR-MAGEUZI.
Kwa mujibu wa barua hiyo,inawataka viongozi wa vyama hivyo vinne vya
siasa kuchukua hatua mapema ya kuwasihi na kuwaelimisha wanachama wao
kwanza, kwa ujumbe wa gesi kama ulivyotolewa na wananchi wa mkoa wa
Mtwara.
“Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaandikia kuwakumbusha tarehe kuwa 04/01/2013,siku ya Ijumaa mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila
alipata fursa ya kuwaalika wadau wote,wazee wa mji wa Lindi,viongozi
wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa,alizungumzia na
kufafanua mwelekeo na msimamo wa Serikali katika suala la gesi na jinsi
mkoa unavyochangia pato la Taifa kwa gesi ya Songosongo na jinsi
anavyojiandaa kwa ugunduzi mpya kwenye kina kirefu cha bahari ya Hindi
wilaya ya Kilwa”Imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Aidha,barua hiyo imeeleza kwamba Jeshi hilo la Polisi,lisingependa
kukwaruzana na jamii katika maandamano hayo ya barabarani kwa hoja za
kisera za kiuchumi ambazo ni za ki-Taifa, zinazoweza kuzungumzika
katika mifumo mingine ya kiutawala kama vile katika vikao vya Bunge.
“Tunaomba ushirikiano na ushirikishwaji wa Jamii katika utii wa
sheria bila Shuruti katika kudumisha amani na utulivu ndani ya mkoa wa
Lindi”Imeeleza barua hiyo.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa vyama vilivyopelekewa barua
hizo,wamemuomba kamanda huyo wa Polisi mkoani hapa,George
Mwakajinga,kutoupotosha umma juu kauli yake,kwani maandamano
yanayotarajiwa kufanywa ni kuunga mkono jirani zao wa Mtwara katika
kutetea gesi iliyogunduliwa huko kutopelekwa nje ya mkoa huo kwa njia
ya Bomba,na sio kupinga kauli ya mkuu wa mkoa wa Lindi.
“Sisi tunawaunga mkono jirani zetu wa Mtwara, juu ya kuondolewa gesi
kupelekwa Dar es salaam,kwani huo ni uonevu na unyang’anyi mkubwa
unaofanywa na hawa viongozi wetu waliopo madarakani”
“Kwani sisi watu wa mikoa ya kusini tumeikosea nini hii Serikali,kama
ni gesi tumewapa kutoka Songosongo Kilwa,licha ya wenzetu kuizuia kwa
njia ya kiustaarabu,yaani kuifikisha mahakamani,lakini
tuliwaachia na Kilwa kukosa kiwanda cha mbolea kama ilivyokuwa
imepangwa,sasa leo wanataka kuihamisha ya Mtwara tuendelee kuwa
masikini”Walisema viongozi na wanachama hao.Januari 04 mwaka huu,viongozi wa Chama cha wananchi (CUF) mkoani
Lindi, wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja vya
Sera,Manispaa ya Lindi,Walitoa wito kwa wananchi kushiriki katika
maandamano yatakayofanyika Februari 23 mwaka huu,ili kuwaunga mkono
jirani zao wa mkoa wa Mtwara,kupinga uamuzi wa Serikali kusafirisha
gesi kwa njia ya bomba na kuipeleka Jijini Dar es salaam kwa ajili
ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme.
Mambo mengine yaliyotajwa na viongozi hao ni pamoja na kuwepo kwa
mfumo wa ununuzi wa mazao kwa utaratibu wa mfumo wa Stakabadhi
ghalani, kwa maelezo kwamba umekuwa hauwasaidii walengwa (wakulima) na
badala yake umekuwa ukiwasaidia wachache
ANGALIA PICHA ZA MAANDALIZI YA KUAPISHWA RAIS OBAMA WA MAREKANI
Maandalizi
makubwa yafanyika jijini Washington DC kwa Sherehe za kuapishwa kwa
Rais wa Marekani Barack Obama yameanza kukamilika.
Vyombo vya Habari mbali mbali hapa nchini Marekani vimekuwa katika kukamilisha matayarisho ya kupata matukio ya kuapishwa Rais Barak Obama kwa muhula wa Pili Ikiwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuchaguliwa kwa mara ya pili na hivyo kuifanya sherehe hiyo kuwa ya Kihistoria.
Sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya National Mall na Memorial Parks zitahudhuriwa na mamilioni ya Raia wa marekani na wageni kutoka nchi mbali mbali kote ulimwenguni.
Rais Obama wa Marekani alichaguliwa kwa kura nyingi baada ya kumshinda mgombea wa kiti cha chama cha Republican Mitt Romney na kuingia awamu ya pili ya Urais ya Urais wa Marekani
Vyombo vya Habari mbali mbali hapa nchini Marekani vimekuwa katika kukamilisha matayarisho ya kupata matukio ya kuapishwa Rais Barak Obama kwa muhula wa Pili Ikiwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuchaguliwa kwa mara ya pili na hivyo kuifanya sherehe hiyo kuwa ya Kihistoria.
Sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya National Mall na Memorial Parks zitahudhuriwa na mamilioni ya Raia wa marekani na wageni kutoka nchi mbali mbali kote ulimwenguni.
Rais Obama wa Marekani alichaguliwa kwa kura nyingi baada ya kumshinda mgombea wa kiti cha chama cha Republican Mitt Romney na kuingia awamu ya pili ya Urais ya Urais wa Marekani

Karibia mwenzi mzima ufundi wa maandalizi ya Obama inauguration 2013
yaliokua yakifanyika katika maeneo mbali mbali ya Jijini Washington DC
yaaza kutia Sura, hapa ni Jengo la Congress ya Marekani Jijini
Washington DC.

Baadhi ya ufundi uliokamilika katika jingo la Capitol Hill liliopo
washington DC na viti vilivyopangwa rasmi kwa ajili ya wageni wanunuzi
watikiti za 2013 Inauguration History ndio makazi yao yatakapokua hapa
kwa siku ya Jumatatu Jan. 21, 2013

Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry akipata picha ya 2013 katika
jingo la Congress ya Marekani liliopo washington DC katika jingo la
Capitol Hill liliopo down town Washington DC Nchini Marekani.
Picha 2008 Inauguration History: Hivi ndivyo itakavyokua Siku ya
Jumatatu Januwari 21, 2012 kwenye Jumba la Congress ya MarekaniDown Town
Washington DC.

Sehemu kubwa ya sherehe ya kuapishwa kwa rais Obama ikifanyiwa ukarabati wamuda.
Rubber floor tiles zikitandazwa maeneo ya sakafu zilizokua na mchanga
kwaajili ya kuhifadhi tope tope zisitimke na kuharibu eneo hilo kubwa la
National Mall,

Kukanyaga mchanga Marekani ni kosa kubwa na ndio maana wameweka Rubber
floor tiles kwaajili ya kukanyagia ili kunusuru michimbuko ya tope tope
na kutoshafua barabara kwa msongamano wa watu watakaomiminika kutoka
Nchi mbali mbali kuja kushuhudia kuapishwa kwa Obama

Sehemu iliotandikwa Rubber floor tiles: Hivi ndivyo Rubber floor
tiles zinavyotandikwa kwenye michanga ili kunusuru topetote raia
wasichafuwe maeneo ambayo bado yanafanyiwa ukarabati sehemu ya National
Mall Jijini hapa.

Hivi ni baadhi ya yyoo vya Potty shortage vinavyotumika kwa haja ndogo
na kubwa viko tayari kwaajili ya raia na wa geni watakao miminika
kuanzia kesho Jumapili na Jumatatu siku ya Obama's inauguration

Fundi mitambo wa NBC NEWS akianda mpango mzima wa kuahabarisha sherehe za kuapishwa kwa rais wa Marekani Barack Obama Live

Banda la CBS NEWS lilijengwa kwa muda vile vile wako tayari kwa kutoa
huduma za kuhabarisha matangazo ya moja kwa moja kwenye kumbukumbu za
2013 Inauguration

Channel marufu ya CNN wakia kwenye uwanja wa National Mall na wao pia
wapo tayari kwa kutoa huduma za kuhabarisha na matangazo ya moja kwa
moja kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Obama 2013 Inauguration

Basi lililowakilisha baadhi ya wafanyakazi wa CNN kumbukumbu ya 2013 Inauguration ndani ya Jiji la Washington DC

Basi jengine lililowakilisha wafanyakazi wa C-SPAN kumbukumbu ya 2013 Inauguration ndani ya Jiji la Washington DC

Kamera iliopo mbele ya Presidential Inaugural Review Stands, in front
White House Washington, D.C. baada ya kuapishwa kwa Obama. hii ni moja
itakayo tumika kwenye Inaugural Review Stands

Cheif wa swahilivilla akia mbele ya White House na mmoja wa wafanya
kazi wa Super Control Camera ambayo kwa jina wanaita Gym Camera inauwezo
wa kunyanyuka juu umbali wa futi 16 na kuhabarisha Live.

Sony Camera ipo tayari kwa kuhabarisha mbele ya Presidential Inaugural
Review Stands, mbele ya White House Jijini Washington DC.

Nyuma ya Presidential Inaugural Review Stands ni White House kuna ujia
mrefu wa Red carpet ndio atakaotumia kuingilia kwenye Review Stands.

Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry akiwa mbele ya Presidential
Inaugural Review Stands ambayo kutumika kwa ajili ya uzinduzi wa Rais
Barack Obama baada ya kuapishwa.

Mjengo wa Matangazo pamoja na Camera LIVE uliojengwa kwa moda mbele ya White House

Benchi nyingi zilizojengwa kwa ahili ya wageni na rais kutoka sehemu mbali mbali watatumia kukalia wakati wa Parade
HII NDIO SHEHENA YA MIHADARATI ILIYOKAMATWA ARUSHA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP),Liberatus Sabas (kulia) akiongea na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya
jinai Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP),Camirius
Wambura aliyeshika madawa ya kulevya aina ya mirungi nje ya jengo la
Makao Makuu ya jeshi hilo Jijini Arusha mara baada ya kukamata shehena
hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),Liberatus Sabas (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na Waandishi wa habari nje ya jengo la makao makuu ya jeshi la Polisi Jijini Arusha.
Gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo lilikuwa na shehena ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya uzito wa kilogramu 1800.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP),Liberatus Sabas (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani na Waandishi wa habari nje ya jengo la makao makuu ya jeshi la Polisi Jijini Arusha.
Gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 284 AGL ambalo lilikuwa na shehena ya mirungi viroba vipatavyo 173 vyenye jumla ya uzito wa kilogramu 1800.(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
Subscribe to:
Posts (Atom)










