Facebook Comments Box

Saturday, January 19, 2013

HII NDIO YANGA BWANA - HIVI NDIVYO ILIVYOWATANDIKA WASAUZI TAIFA LEO

 Didier Kavumbagu (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Black Leopards, wakati wa Mchezo huo, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Jerry Tegete.
jj
 Kikosi cha Yanga.
 Kikosi cha Black Leopards.
 Mchezaji wa Yanga, Kabange Twite (kushoto) akimiliki mpira huku akidhibitiwa na beki wa Black Leopards, Nkosiabo Xakane, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao lililofungwa na Jerry Tegete. (PICHA NA SUFIANI MAFOTO)


SIMBA YACHEZEA KICHAPO CHA 3 KWA 1

 Mabingwa wa soka Tanzania Bara,Simba wameshindwa kutamba mbele ya Wenyeji wao mara baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Jeshi la Oman. mechi hiyo ilichezwa Ijumaa jioni kwenye uwanja wa Qaboos Complex jijini Muscat.
bao la simba lilifungwa katika kipindi cha pili na Haruna Moshi 'Boban' huku Mwenyekiti wa Simba,Ismail Aden Rage akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine wa simba, Rahma Al Kharoos na Musleh Rawahi pamoja na Kocha Talib Hilal wakiishuhudia Simba ikizama mbele ya wanajeshi hao

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjlRCm9tsdl0GuqK8TLbE1shCvEZJgJ5ZlH_m5XkhR1hTThltEl1Xt8bq8XcTQF75XYFCL6no8X9TueY_JkNVtYjykqNT-6pBUZ_PX-fKmeb_-wQHsscSKl5YQpRPaAvlNjUKfcBaSRVcQ/s1600/rAGE.JPGMwenyekiti wa Simba na Mfadhili wa safari ya Simba Rahma Al Kharoos akiangalia timu ya Simba ikipokea kichapo

TRA,,TUME YA UCHAGUZI NA JUMUIYA YA SERIKALI ZA MITAA (ALAT) WATOA MAONI YA KATIBA MPYA





 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi akiwasilisha maoni ya Jumuiya hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam Ijumaa, jan 18, 2013. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Ally saleh akiongea katika mkutano na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliokutana na Tume kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqMBipiZ6xuBIr7S_HqKfhWiuqiFBoed3IEs9XBug6QoRugraXDI0Az5Ds1eGNQSGepfRtK37-qqZr9CU1TXRs9ua0wUX1VMSfErSIKhDoA3xD8p-04w6K9UDnSz8lIPc8OzlqnwMu59Q/s1600/CRC-TRA+Jaji+Warioba+na+Viongozi+wa+TRA.jpg
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Harry Kitillya (mwenye tai nyekundu) akiongea na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjd_pJBymQJ4i5jeCDYb62zhaA8NubxDoPSA2TSdrA9lKa6fWm3PMmw8CVwFlBK22h8TYtK3O0_l2A54dSMrmWFnP0-F0hJaKzK9VrmQoUslqkyipIyydYZhjKBPPvWqxr7lAvVuT40p2s/s1600/CRC-TRA+Picha+ya+pamoja.jpg

 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba (wa sita kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliongozwa na Mwenyekiti wa Bodiu ya TRA Bw. Bernard Mchomvu (wa nne kutoka kushoto) mara baada ya Mamlaka hiyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya jijini Dar es Salaam.



Friday, January 18, 2013

THEO WALCOTT AONGEZA MKATABA WA MIAKA MITATU NA NUSU ARSENAL

Baada ya malumbano ya muda mrefu mchezaji Theo walcott ameamua kukubali kuongeza mkataba na Arsenal kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Katika mkataba huo mchezaji huyo atakuwa akilipwa Paund 100,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya milioni miambili hamsini za tanzania. Mchezaji huyo alikataa kuongeza mkataba wa miaka mitano ambao ungempa paund 70,000 kwa mwezi. Mbali na mihele yote hiyo mchazaji huyo amepewa na bonasi ya paundi milioni 3 kwa ajili ya kuongeza mkataba huo. Imeichukua Arsenal mwezi mzima wa malumbano na mchezaji huyo kupata saini yake.

Baada ya kupata saini ya mchezaji huyo kocha wa Arsena alisema "We are all delighted that Theo has signed a new contract. He joined us as a 16-year-old and since then has developed very well to become an extremely important player for both Arsenal Football Club and England." akiwa anaelezea furaha yake na klabu kwa ujumla kwa mchezaji muhimu ambae alijiunga kilabuni hapo akiwa na miaka 16 mpaka sasa amekuwa muhimu kwa kilabu na timu ya taifa ya uingereza

Nae Theo alisema "I am very happy to have signed a new contract here at Arsenal. Thanks to everyone for their continued support, especially the manager, everyone at the club and most importantly the fans. I have made it clear from the start that I wanted to stay at Arsenal so I am pleased we have agreed a deal that everyone is happy with. What’s important now is for the team to realise its potential and win trophies.” Akionesha furaha yake baada ya kuweka saini na kuonesha nia ya kutafuta makombe katika kilabu hicho kilichopatwa na ukame wa makombe

SIMBA WAFANYA BONGE LA SHOW LA BONGO FLEVA WAKATI WA TAFRIJA YAO

Hapa wakimwaga burudani najua unaijua ile staili ya wazee wa Bongo Fleva "Piga keleleeeeeeeeeee"

Kwa show nzuri ilibidi mama aende kuwatunza.


Mdhamini wa safari ya Simba Rahma jana aliwaalika Simba nyumbani kwake eneo la Al Kheri jijini Muscat, Oman jana usiku kwa ajili ya chakula cha usiku.
Walikula pamoja na baadaye bendi maalum kutoka Tanzania iliwapigia muziki na wakaserebuka pamoja huku Rahma akimwaga noti kama maji.

Katika hafla hiyo, Rahma alikabidhiwa jezi ya Simba na Musleh Rawah ambaye ni mmoja wa wadau wa Msimbazi na jezi ya timu ya taifa ya Oman na kocha wa makipa wa timu hiyo, Haroun Amur.



GHARAMA ZA KUPIGA SIMU ZASHUSHWA


Picture
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za mitandao ya simu Tanzania wakisikiliza maoni mbalimbali, Dar es Salaam jana, kuhusu utozaji wa viwango sawa kwa upigaji simu kwa mitandao yote nchini ifikapo Mwezi Machi mwaka huu. (Picha: Charles Lucas/MAJIRA)
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kampuni za mitandao ya simu Tanzania wakisikiliza maoni mbalimbali, Dar es Salaam jana, kuhusu utozaji wa viwango sawa kwa upigaji simu kwa mitandao yote nchini ifikapo Mwezi Machi mwaka huu. (Picha: Charles Lucas/MAJIRA) Mapendekezo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kampuni za simu kushusha gharama hizo kwa dakika kuanzia Machi mosi mwaka huu ili kumpunguzia gharama ya kupiga simu kwa mteja wa kampuni moja ya simu ya mkononi kwenda kwa mteja wa kampuni nyingine yamekubaliwa kwa kiasi kikubwa. Wakizungumza Dar es Salaam jana katika mkutano wa kukusanya maoni ya wadau na watumiaji wa simu za mkononi ulioandaliwa na TCRA, Kampuni za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Vodacom Tanzania zilidai punguzo hilo litawapotezea mapato na kuvuruga nia yao ya kuendelea kuwekeza. Mwakilishi wa Airtel Tanzania, Mwanasheria Clara Mramba, alisema wao wanakubali punguzo hilo lakini gharama zishuke kwa hatua kutoka mwaka mmoja hadi mwingine kwa kuanzia Sh 84 Machi hadi Sh 29.26 mwaka 2017. Alidai kuwa kushuka kwa kiwango hicho kikubwa cha Sh 34.92 Machi, kunaweza kuharibu uwekezaji wao: Tunataka ianze kushuka kutoka shilingi 112 hadi shilingi 85 kwa mwaka huu, shilingi 63 kwa mwaka unaofuata, shilingi 47 kwa mwaka unaofuata, shilingi 34.5 kwa mwaka unaofuata na shilingi 26.96 kwa mwaka unaofuata. Mkisema mshushe gharama hizo kutoka shilingi 112 hadi shilingi 35 ambazo ni sawa na asilimia 69 mtapunguza kasi ya uwekezaji wetu kwa sababu sekta ya mawasiliano inahitaji uwekezaji mkubwa. Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Mwanasheria Walarick Ngitu, alisema kama gharama hizo zitashuka kwa kiasi hicho watashindwa kufunga minara ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini. Alipendekeza punguzo lianze kwa asilimia 35 na mwakani asilimia 20 na kwenda taratibu hadi mwaka 2017 jambo litakalosaidia sekta hiyo ikue huku gharama ikipungua taratibu: Watu wengi wa vijijini wanapigiwa zaidi simu kuliko wao kupiga, kwa hiyo mkishusha gharama hizo ni wazi minara ya mawasiliano haitafungwa vijijini kwa sababu kampuni itakuwa haipati faida na itawekeza zaidi mijini, tunaomba bei hizo zisishuke kwa uharaka wa namna hiyo. Mwakilishi wa Tigo Tanzania, Revocatus Nkata, alisema endapo gharama hizo zitashuka zitawasumbua kulipa kodi ya Serikali kwa sababu mapato yao yatapungua. Alitaka punguzo lianzie Sh 80 na soko lisiingiliwe kwa kuwa tayari limekomaa ili liendelee na ushindani: Uwekezaji wetu tunaotaka kuufanya lazima utapungua kama gharama hizi zitapungua, pia ni dhahiri tutapata tabu ya kulipa kodi serikalini. Si hivyo tu, bali soko la mawasiliano sasa hivi limekomaa hivyo halihitaji kuingiliwa, bora liachwe na kampuni ziendelee kufanya biashara. Kampuni za Sasatel, Sixtelecom, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), BOL na Zantel na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia zimekubali gharama hizo kushuka. Mwakilishi wa Sasatel, Godfrey Murisi, alisema punguzo hilo litawafaidisha wateja na watakuwa waaminifu kutokana na huduma wanazozipata. Mwakilishi wa Sixtelecom, Said Abdala, alisema Tanzania ndio nchi pekee ambayo ina gharama kubwa katika muingiliano wa simu na ikishuka italeta ushindani katika soko. Mwakilishi wa TTCL, Mrisho Shaaban, alisema mtumiaji wa simu hatakiwi kubebeshwa gharama zisizo za lazima na agizo hilo lilitakiwa kuanza mapema kabla ya Machi, mwaka huu. Mwakilishi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Samson John, alisema gharama hizo zitakaposhuka zitampa mtumiaji unafuu wa kupiga simu na itaondoa ukiritimba katika soko: Gharama zikishuka maana yake mtumiaji atafaidika na kampuni nyingine mpya zitapata nafasi ya kutoa huduma za mawasiliano sokoni, sisi tunataka sekta ya mawasiliano ikizidi kutanuka na ukiritimba wa baadhi ya kampuni uondoke. Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Samson Mwela alisema wamekubaliana na mapendekezo hayo, kwa kuwa sekta hiyo inaendeshwa kwa ushindani ambao unalindwa, hivyo ni lazima mtumiaji apate haki zake. Alisema kupungua kwa gharama hizo, kutawapunguzia watumiaji mzigo wa simu ikiwa ni pamoja na kudhibiti simu bandia zinazotumiwa na wengi na kuongeza unafuu wa matumizi ya simu mpaka vijijini. Stanley Mwabulambo wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), alibainisha kuwa waliunga mkono kwa kuwa mpango wa kibiashara wa kampuni hizo hutegemea gharama za muunganisho. Alizitaka kampuni hizo kuwa bunifu katika ushindani huku akitaka punguzo hilo lionekane kwa mteja na TCRA ihakikishe punguzo hilo haliongezwi upande mwingine. Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Ushindani kutoka Tume ya Ushindani (FCC), Shadrack Nkelebe alisema mapendekezo hayo yataongeza ushindani kwa kuruhusu wateja kuwa na chaguo na kampuni moja. Waziri wa zamani wa Ujenzi na Uchukuzi, Nalaila Kiula aliunga mkono mapendekezo hayo na kuitaka TCRA kuzitazama zaidi kampuni za simu kwa manufaa ya wateja kutokana na huduma wanazotoza gharama kubwa. Akifunga mkutano huo wa mwisho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCRA, Jaji mstaafu, Buxton Chipeta, alisema maoni yaliyotolewa yatafanyiwa kazi: Mawazo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi na tutakuja na jibu moja kabla agizo halijaanza kutekelezwa, nia yetu kubwa tunataka mtumiaji wa simu asiumizwe na mtoa huduma za mawasiliano naye asiumie. Mkurugenzi wa Ofisi za Kanda wa TCRA, Victor Nkya alisema jana kwamba katika mapendekezo yao gharama hiyo inatakiwa kushuka kuanzia Machi kutoka Sh 112 ya sasa mpaka Sh 34.92. Mwakani inatarajiwa kuwa Sh 32.4; mwaka 2015 Sh 30.58; mwaka 2016 Sh 28.57 na mwaka 2017 Sh 26.96. Kutokana na mapendekezo hayo ambayo yalitokana na utafiti uliobaini kuwa gharama hizo nchini ni kubwa, wadau na kampuni zilizohudhuria kongamano la wadau la kujadili bei hizo, walikubali. TCRA ilitoa mapendekezo hayo baada ya kupata ripoti ya Kampuni Mwelekezi Mshauri kutoka Uingereza iliyofanya utafiti kwa kuangalia mapato na faida za kampuni za simu nchini.


2013 AFRICA CUP OF NATIONS (AFCON) MATCHES TIMETABLE/FIXTURES



Thursday, January 17, 2013

HUYU NDIO ALIO WAPELEKA SIMBA OMAN




Rahma al Kharoos ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya simba, leo jioni alitembelea mazoezi ya Simba kwenye uwanja wa Oman Club
Rahma pia ndiye mmiliki wa RBP Oil, aliwahi kuwa mdhamini mkuu wa Twiga Stars, pia aliwahi kuwa mmoja wa wamiliki wa African Lyon..ni kati ya wapenda michezo.
Pia ndiye aliyeidhamini safari yote ya Simba hapa Oman kwa kuwalipia hoteli, tiketi pamoja na chakula kwa muda wote wa siku 14 watakazokuwa hapa.



PICHA NA SALEHE ALLY WA CHAMPION



HIZI NDIO MBINU ZA KUWATAMBUA WALIOFICHA FEDHA USWISI

 
Tutawatambuaje wenye mabilioni Uswisi? 

WAKATI Serikali na Bunge zikiwa kwenye mvutano kuhusu hatua za kufuatwa kurejesha mabilioni ya fedha za Kitanzania yaliyofichwa kwenye benki za nchini Uswisi, swali kubwa lililopo ni kwamba ni akina hasa ambao wana fedha huko.

Mtoaji wa hoja binafsi kuhusu suala hilo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, amegoma kutaja majina ya vigogo wanaotajwa kuhifadhi fedha akitaka uchunguzi ufanyike na majina yafahamike wakati huo, huku serikali ikimtaka ataje majina ili ipate pa kuanzia kwenye uchunguzi huo.

Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema, inataka kuendesha uchunguzi kuhusu madai hayo ya Zitto lakini kwanza inataka mbunge huyo ataje majina ya baadhi tu ya vigogo ambao ana ushahidi wamehifadhi fedha Uswisi.

Pamoja na hayo, swali moja ni lazima lipate majibu, leo au kesho. Swali lenyewe ni hili; ni akina nani waliokwiba fedha za Watanzania na kwenda kuzihifadhi ughaibuni?

Niseme mapema kwamba kuwa na akaunti nje ya nchi si dhambi. Dhambi inakuja pale inapofahamika kwamba fedha hizo zilipatikana isivyo halali.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Uswisi iliyotolewa Juni mwaka jana, Watanzania wamehifadhi kiasi cha dola za 
Marekani milioni 178 (zaidi ya Sh bilioni 300) katika benki mbalimbali nchini humo. Ripoti hiyo haikutaja majina, wala kiwango walichonacho watu hao na kutokana na taratibu za kibenki za taifa hilo la Ulaya, ni lazima kuwepo na sababu nzito za wao kutoa taarifa zozote kuhusiana na wateja hao.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya Benki Kuu ya Uswisi si ya kuaminika sana kwa vile taifa hilo linafahamika kwa kutoa taarifa zisizoaminika kuhusu kiwango hasa cha fedha kilichohifadhiwa na wateja wake.

Kwa mfano, wakati Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipodai fedha zilizoibwa na aliyekuwa rais wa taifa hilo, Mobutu Sesesseko, zilizokadiriwa kufikia dola bilioni tano, Waswisi walirejesha dola milioni nane tu wakidai ndiyo kiasi kilichokuwapo!

Hata hivyo, ripoti hiyo ya Benki Kuu ya Uswisi imesaidia tu kuthibitisha kwamba wapo Watanzania waliohifadhi mamilioni ya dola katika akaunti mbalimbali nchini humo.

Swali linakuja ni akina nani hao? Nimefanya utafiti kidogo na yafuatayo yanaweza kusaidia kupata majina ya wahusika.

1. Mazingira ya wizi

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ufisadi (Global Financial Integrity, GFI), katika mataifa mengi ya kiafrika, fedha huibwa katika mazingira makubwa matatu- rushwa, ukwepaji kodi na mauzo ya bei za kurusha ya bidhaa au huduma mbalimbali.

Kuna maeneo mengine madogo kama vile ‘usafishaji’ wa fedha haramu, biashara ya silaha, dawa za kulevya na mambo mengine lakini GFI inaamini kwamba maeneo haya madogo yanafanya kazi zaidi katika mataifa ambayo yana serikali zisizo imara.

Kwa vile Tanzania ina serikali imara (walau), kulinganisha na nchi kama vile Somalia, sababu hizo tatu za awali kwa mujibu wa GFI ndizo zinazoweza kutoa picha kuhusu ni akina waliohifadhi fedha zao nchini Uswisi kutoka nchini mwetu.

GFI wametoa takwimu zinazoonyesha kuwa zaidi ya dola za Marekani milioni 148 (Sh bilioni 246) huibwa Afrika kila mwaka kutokana na rushwa. Dola milioni 50 (Sh bilioni 80) kwa ukwepaji kodi na dola milioni 30 (Sh bilioni 48) zinazotokana na misaada kutoka kwa wahisani. Je, wapi tuanzie kuchunguza?

2. Idara ya Usalama wa Taifa (TISS)

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Tanzania la Juni mwaka jana, katika kipindi cha kati ya mwaka 2001 hadi 2008, Tanzania imepoteza zaidi ya Tsh. trilioni 1.2 kutokana na mikataba mibovu, rushwa na ununuzi wenye kutia shaka.

Haya yote yamefanyika wakati Idara ya Usalama wa Taifa nchini ikiwa inatazama na katika hali ya kawaida haiwezekani kwa idara hii kutofahamu chochote kwenye kashfa kama za ununuzi wa rada ya mtumba, Meremeta, Deep Green, EPA na Richmond.

Kimsingi, serikali imeshindwa kutoa maelezo kuhusu mradi wa dhahabu wa Meremeta ikidai suala hilo lina maslahi ya taifa na vigogo kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa wanatajwa kuhusika na mradi huo.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, serikali ya Uswisi ilirejesha nchini Peru kiasi cha dola milioni 180 (Sh bilioni 288) zilizodaiwa kuhifadhiwa humo na aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa wa nchi hiyo, Vladimiro Montesinos, wakati wa utawala wa Rais Alberto Fujimori.

Kwa vyovyote vile, watu wetu wa usalama watakuwa wanajua kitu kuhusu ufisadi wote huu. Ipo imani kwamba makachero wa Tanzania ni miongoni mwa walio bora katika Bara la Afrika. Ni lazima TISS imulikwe ili ieleze iwapo ilikuwa na taarifa kuhusu ufisadi uliokuwa ukifanyika lakini taarifa hizo hazikufanyiwa kazi na watawala au yenyewe nayo ina mkono kwenye hilo.

Kwa sababu tayari tuna ushahidi wa Montesinos. Kwa sababu tayari serikali imekwishakutaja usalama wa taifa kwenye ufisadi wa Meremeta.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa katika hizo trilioni 1.2 zilizoibwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, nyingine zitakuwa zimeangukia Uswisi.

3. Mawaziri

KWA mujibu wa taratibu zilizopo nchini, Waziri wa Fedha anaruhusiwa kutoa misamaha ya kodi kwa kampuni au taasisi mbalimbali pale atakapoona inafaa.

Tayari mawaziri wawili wa zamani wa serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba na Daniel Yona Ndhira, wamefikishwa mahakamani kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.2 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart.

Utafiti huu hauna haja ya kuwatia hatiani akina Mramba lakini kwa sababu GFI inasema sehemu ya fedha zinazoibwa hupatikana kwa misamaha ya kodi huu ni mfano mmoja wapo wa namna mtu anavyoweza kutumia mamlaka yake kujitajirisha.

Kama serikali imeweza kufungua mashitaka kwa mawaziri wawili tu wa zamani wa fedha ambao hasara waliyotia imefikia kiasi cha Sh. bilioni 11.2, je imepoteza kiasi gani kwa mawaziri wengine katika awamu tofauti za uongozi?

Kama kweli serikali inataka kufahamu ni akina nani wana fedha Uswisi, sehemu nzuri ya kuanzia ni hapa kwa mawaziri wa fedha na uchumi waliopita kwenye awamu tofauti hapa nchini.

Wengi wa vigogo wa nchi mbalimbali waliobainika kuhifadhi fedha Uswisi wanatoka katika nchi zenye utajiri wa maliasili kama Tanzania.

Serikali inaweza kuangalia zoezi zima la ugawaji wa vitalu kwa kampuni kubwa za mafuta zinazotafuta uwepo wa nishati hiyo hapa nchini na misamaha mbalimbali iliyowahi na inayoendelea kutolewa kwa makampuni ya madini hapa nchini.

Kuna taarifa kwamba baadhi ya makampuni makubwa ya kigeni hutumia rushwa ili wapewe vitalu vya gesi katika maeneo ambako kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana gesi kuliko mengine. Wakipewa upendeleo huo, huweka fedha kwenye akaunti za waliowasaidia zilizo nje ya nchi.

Uchunguzi wa hili usiishie tu kwa mawaziri bali uende hadi kwa makatibu wakuu wao na maofisa wa ngazi za juu waliokuwa na ushawishi katika utoaji wa misamaha, vitalu na leseni mbalimbali za uchimbaji wa madini.

Humu ndimo wanapopatikana wengi wenye fedha chafu nchini Uswisi.

4. Jeshi la Polisi Tanzania

WAKATI ‘dili’ zinapofanyika na kubainika, watu wa kwanza kupewa taarifa ni Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukamata watuhumiwa. Hawa ndiyo wanaoandaa mashitaka na hawa ndiyo wataamua kuwapo au kutokuwapo kwa kesi.

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Afrika Kusini, Jackie Selebi, amefungwa jela hivi karibuni, kutokana na uhusiano wake na mhalifu maarufu nchini humo, Glen Agliotti. Mhalifu huyo alikuwa akimpa mkuu huyo zawadi mbalimbali na pia kumwekea fedha katika akaunti zake.

Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi zinazokamata sana dawa za kulevya ingawa kuna tuhuma kwamba magwiji wa biashara hizo wana mahusiano mazuri na baadhi ya vigogo wa Jeshi la Polisi.

Tukichunguza vizuri mabosi wa Polisi, tunaweza kupata kitu kuhusu akina nani wamehifadhi fedha zao Uswisi au popote duniani isivyo halali.

5. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

KATIKA kashfa ya ununuzi wa rada, jina la aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, limeibuka mara nyingi na vyombo vya upelelezi vya Uingereza vinamtaja kama miongoni mwa wahusika wakuu wa kashfa hiyo.

Mwanasheria Mkuu wa serikali ndiye mshauri mkuu wa serikali kwenye mikataba minono (mikubwa) baina ya nchi na nchi au nchi na mashirika makubwa ya kimataifa.

Yeye ndiye anayeweza kuamua iwapo serikali iingie kwenye dili au la. Kama Chenge na baadhi ya wasaidizi wake walitajwa kwenye kashfa ya rada, ni wazi kwamba ofisi hii inatakiwa kumulikwa wakati serikali ikitafuta walioficha fedha Uswisi.

Kwa bahati nzuri, tayari inafahamika kuwa Chenge ana akaunti katika nchi za kigeni kama ilivyobainika wakati wa uchunguzi wa kashfa ya rada.

6. IKULU

Fujimori, Mobutu, Sani Abacha, Francosi Duvallier, Omar Bongo na Theodor Nguema wana mambo matatu yanayowafananisha; wote waliwahi kuwa marais katika nchi zao,  walifanya ufisadi wa kutisha na wote walificha mabilioni yao Uswisi.

Japo hii haimaanishi kuwa waliowahi kuwa marais wa Tanzania nao wana akaunti katika taifa hilo, sio vibaya kujiridhisha kwa kufanya uchunguzi ili kubaini kama wanaweza kuwa wameficha fedha Uswisi.

Kwa Tanzania, marais wenyewe wako wanne tu na hivyo kuchunguza si kazi ngumu.

Ikumbukwe kwamba rais pekee wa Tanzania kufungua ofisi ya biashara akitumia anuani ya Ikulu, Benjamin Mkapa, alipoumwa goti takribani miaka kumi iliyopita, alikwenda kutibiwa nchini Uswisi !

Labda tujiulize, angewezaje kuishi kule kwa miezi mitatu bila ya kuwa na akaunti katika mojawapo ya benki za huko? Je, ilikuw (ina) kiasi gani cha fedha?

Kwa mfano, Mkapa si ndiye aliyekuwa rais wakati wa ubinafsishaji? Serikali yake si ndiyo iliyopitisha misamaha mingi ya kodi kwa makampuni ya madini? Si mkitaka mnachunguza tu?

Tukiwa na nia ya kutaka kujua nani ana fedha Uswisi tutajua tu. Mimi nimetoa mchango wangu wenye pa kuanzia tu. Wengine wanaweza kutoa michango yao kwenye maeneo mengine.


KIBONZO KINACHO NANGA BARAZA LA VIJANA LA CHAMA KIMOJA




HII NDIO HALI YA HEWA YA DAR ES SALAAM ASUBUHI NA ADHUHURI YA LEO





 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU