Facebook Comments Box

Wednesday, January 16, 2013

PEP GUARDIOLA KUWA KOCHA MPYA WA BAYERN MUNICH

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwaka mzima, kocha kihispaniola Josep Guardiola leo hii ametangazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani kuanzia mwezi wa sita mwaka huu.

Taarifa rasmi kutoka kwenye klabu hiyo iliyotolewa muda mfupi uliopita inasema kwamba Guardiola atachukua majukumu yake ya kuwa manager mpya wa timu hiyo baada ya msimu wa 2012-2013 kuisha, na amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuifundisha timu hiyo inayoongoza ligi ya Bundesliga.

NYUMBA YA KAPTENI WA NDEGE YA RAIS YABOMOLEWA


Nyumba iliyokuwa katika mtaa wa Ohio kitalu namba 15 inayoripotiwa kwua ilikuwa inamilikiwa na Kapteni Msataafu wa Ndege ya Rais, Bw. Felix Kileo imevunjwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya udalali ya Rhino Auction Mart, kwa madai kuwa kampuni hiyo imepewa kazi hiyo ya kubomoa na tassisi ya Benki ya Wakulima, TIB.

Kwa mujibu wa maelezo ya wabomoaji hao, TIB wanataka kujenga jengo la orofa kwenye eneo hilo, baada ya nyumba hiyo kupewa na serikali na mtumishi wa serikali aliyekuwa anaishi kwenye nyumba hiyo kupewa nyumba nyingine.

Mtoa maelezo hayo amesema, mtumishi huyo wa Serikali alikaidi kutoka katika nyumba hiyo ndiyo maana kampuni hiyo ilipewa kazi ya kuingia kwa kuvamia nakuanza kuvunja.

Ndugu wakaribu wa Kapteni huyo ambae mwenyewe hakuwepo kwa muda huo eneo la tukio wamelalamikia kitendo anachofanyiwa ndugu yao.

“Huyu mimi ni nduguyangu amekuwa mtumishi wa serikali za awamu zote, amestaafu mwaka jana kama rubani wa ndege ya Rais lakini anachofanyiwa ni udhalilishaji, na vitendo hivi si vya kistaraabu hata kidogo. Ni ufisadi tu huu. Pesa zitatoa roho ya mtu!” alisikika akisema mmoja wa kaka wa Kapteni huyo.

Kwa mujibu wa ndugu hao kesi ya msingi iko mahakamani na kesho kutwa inasikilizwa lakini wameshangazwa kitendo cha kuwavamia bila hata barua ya mahakama ya kuvunja nyumba hiyo.

Baada ya kufunguliwa kesi, upande wa serikali ulishinda, lakini Kapteni huyo kupitia mawakili wake walikata rufaa iliyotaka zoezi la kuendeleza kiwanja hicho kusimama.


EXCLUSIVE: INTERVIEW YA KWANZA YA OKWI BAADA YA KUSAINI MKATABA NA ETOILE DU SAHEL

">

OKWI AWASHUKURU SIMBA



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU