Facebook Comments Box

Monday, January 14, 2013

TENGA KUTOGOMBEA TENA UONGOZI TFF


Tenga kutogombea tena uongozi TFF.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema hatagombea tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema wakati anaingia kwenye uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF kama taasisi kwa kuweka mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba na kanuni, jambo ambalo limefanyika.

“Wajumbe wamekuwa wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana. Nilishafika pale pa kufika. Tulipoanza wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo tumeifanya. Tulipoingia mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema Rais Tenga.

Amesema walitengeneza Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa wapiga kura ambapo hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea migogoro, hata ikitokea kuna mfumo wa kuidhibiti.

Rais Tenga ameishukuru Sekretarieti ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kamati za uchaguzi za wanachama wa TFF na vyama wanachama wa TFF kwa hatua iliyofikiwa katika uchaguzi ambapo mikoa yote imekamilisha uchaguzi na kubaki vyama shiriki pekee.

Ametoa mwito kwa wadau kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga taasisi ajenda iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini kifanyika ili mpira uchezwe katika maeneo mbalimbali.
“Tumeshatengeza mfumo, sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira. Changamoto ni tufanye nini ili mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo ajenda ili tuangalie tunakwendaje mbele,” amesema.
Pia amesema ushirikiano ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni wa ajabu. Vilevile ameishukuru vyombo vya habari, Serikali, klabu, wadhamini na wafadhili kwa mchango wao katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

HEBU MCHEKI MAN KICHEFU NA WANAHOFIA




ANGALIA PICHA ZA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA IFM LEO


www.kitongoni.blogspot.com
Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha wakiwa mbele ya geti la wizara ya ulinzi wakipeleka madai yao ya kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai kuwa ijumaa walifanya kikao na jeshi la polisi cha ajabu kesho yake wanafunzi wawili walivamiwa na majambazi na kulawitiwa na kuibiwa vitu vyao.

Ulinzi ukiwa umeimarishwa wizarani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha
Hapa wanafunzi wakiwa safarini kwenda kumuona kamanda kova

Kamanda Kova akimsikiliza Rais wa wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) akimuelezea kadhia nzima. Baadae Kamanda Kova aliamuru wanafunzi hao waende wote Kigamboni kushughulikia kadhia hiyo

Kamanda Kova akitoa taarifa kwa waandishi wa habari

Hapa wanafunzi wakiimba "tunavuka bure , tunavuka bure" huku wakielekea kwenye kivuko


Hapa wanafunzi wakigoma kushuka kwenye kivuko ilichukua saa zima ndio wakashuka na kuruhusu kivuko kiendelee na shughuli zake kama kawaida
Wakati wengine wakikataa kushuka wengine walikuwa wakiongezeka



WABABA WA BSS (2012) AKABILIWA NA KESI YA KUTEMBEA NA MWANAFUNZI


 Mapenzi yao yalianza tangu binti akiwa kidaato cha tatu lakini halikuwa penzi lenye mashamu shamu kwa kuwa wabababa alikuwa bado hajamiliki pesa na heshima katika jamii inayomzunguka kama sasa mara tuu baada ya kuchukua kifuta jasho cha bss na vijihela alivyopewa na mapapaa waliokubali kazi aliioifanya bss hivyo kuwa na kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunz ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo. Wababa aliwekwa ndani kwa muda wa siku mbili na kesi bado ipo mahakamani na wazazi wa binti wameapa kumweka ndani wababa na kumfanya kama Babu Sea huku binti akiwa hajaonekana siku ya 4 sasa na kutokujulikana alipo kwa madai anampenda wababa na wakimfunga tu nae anakunywa sumu.


Sunday, January 13, 2013

SAFARI YA YANGA YA MWAKA 1973 KUZINDUA TOTO AFRICA FC MWANZA ( Part II)

Waliosimama kuanzia kulia Mzee Kwala, Sululu, Chotta, Muhamed Mkweche, Muhamed Yahaya "Tostao" (anaechungulia jina lake halijapatikana) Kassim Manara,Shirsaz Shariff (wawili wa mwisho majina yao hayajapatikana) Waliochuchumaa kuanzia kushoto Abdulrahman, kibonge, Bilal Kabange, Muhamed Rishard Adolph, Muhamed Sengendo, Gordian Mapango, Jaffar Abdulrahman (wawili waliobaki majina yao hayajapatiakana ila kati ya hao wote ambao majina yao hayajapatikana mmoja wao ni Dr Ramadhan Dau)

Baada ya kuona ilivyopatikana timu ya Yanga B na mwaliko wa safari leo tunaendelea kuona safari ilivyokuwa na nini kilitokea.
Safari ilifanyika na ili kuwapa hamasa vijana Yanga ilitoa mchezaji mmoja kutoka timu ya wakubwa ambae alikuwa ni Boi Wiskens ambae alikuwa namba tatu mchezaji huyu alichezea hadi timu ya Taifa. Kutokana na ubovu wa barabara mchezaji wa Yanga B Muhamed Yahaya Tostao aliumia goti. walipofika wakakuta timu zitakazo shiriki ni Toto wenyewe kama wenyeji, Pamba na Cooperation United ya Shinyanga.Kikawaida list ya Yanga huwa inapangwa Dar Es Salaam ila Kocha Victor yeye alikuwa anaruhusu kipa kupanga beki yake na list ilikuwa hii ambayo ilicheza mechi ya kwanza na Pamba na kushinda 3 kwa 1.
1. Bilal Kabange 2. Jafar Abdulrahman 3. Shiraz Sharif 4. Muhamed Mkweche 5. Muhamed Rishard Adolph 6.Muhamed Yahaya Tostao 7 na 8 wamesahaulika 9 Kassim manara. Kipa alipomtaja Tostao kila mtu alikataa na kusema mgonjwa ila usiku wa walipofika Mzee Mangara Tabu Mangara alipiga simu hospitali ya mwanza (Bugando) na Tostao akapewa huduma na akaambiwa mechi ikiisha arudi kwa matibabu zaidi. Kama kawaidamechi zote Yanga walishinda kwa 3 kwa 1 isipokuwa moja tu Cooperation United ambayo walishinda 2 kwa 1 na golini alikaa Juma Pondamali messah. Baada ya mechi na kuchukua ubingwa Yanga walipewa zawadi ya saa ya ukutani kubwa ambayo walirudi na kuikabidhi kwa uongozi pamoja na kombe.
Baada ya kufika Dar Es Salaam Simba B waliomba barua ya kucheza na Yanga B kwenye uwanja wa Karume. Wakati huo Yanga B ikiwa haijafungwa mechi hata moja (watakubali au hawatakubali vipi iliundwa Nyota africa na Pan Africa Ijumaa ijayo itaendelea kwa ajili ya sehemu ya mwisho)

HII NDIO KAMPUNI YA FILAMU INAYOMILIKIWA NA WEMA SEPETU


Kupitia mtandao wa kijamii wa picha wa Instagram, Wema Sepetu ameshare picha za kwanza zinazoonesha logo ya kampuni yake iitwayo Endless Fame Films. “Nawaomba mzidi niombea nifike nnapotaka endless fame ifike… Inshallah,” ameandika mrembo huyo.


PETER WA P SQUARE AKIWA MAREKANI NA MTOTO WAKE


Mwimbaji wa kundi la P Square la Nigeria, Peter Okoye alikua California Marekani kwenda kumsalimia mtoto wake wa kiume ambae amepata na girlfriend wake Lara Omotayo ambae kwa sasa yuko San Francisco Marekani na akiwa huko atajifungua mtoto wake wa pili na Peter Okoye mwishoni mwa january 2013.
Kundi la P Square limekataa kupokea mialiko ya showz za january 2013 ili wapumzike kutokana na mfululizo wa show walizopata siku zilizopita.
.
.
.
.

Peter Okoye na baby mama wake Lola Omo

HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA SAED KUBENEA KWENYE KATIBA MPYA


 
Nani anataka nini katika katiba mpya?

Haya ni maoni yaliyowasilishwa na Saed Kubenea wa MwanaHALISI; gazeti lililofungiwa na serikali kwa muda usiojulikana tangu 30 Julai 2012.
 
                                                                      

JUZI (10 Januari 2013) wenye vyombo vya habari na asasi nyingine za habari waliwasilisha kwa Tume ya Katiba Mpya, mapendekezo ya asasi zao na hata kuongeza maoni binafsi kama mwenyekiti wa mkutano wa Katiba, Prof. Mwesiga Baregu alivyoruhusu.

Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), wachapishaji wa magazeti ya MwanaHALISI na MISETO, aliwasilisha maoni yake. Ndimara Tegambwage ameyasoma na kuyafanya moja ya mambo muhimu aliyoona yenye thamani. Anatushirikisha:

Mapendekezo: Katiba Mpya (Na Saed Kubenea)

1. Kuhusu vyombo vya Habari
KATIBA itamke kuwa vyombo vya kutunga sheria (Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Baraza la Wawakilishi, Bunge la Tanganyika au Bunge la Shirikisho; na vyovyote vile vitakavyokuwepo) visitunge:
a) Sheria inayopingana (inayokinzana), inayokwaza au kuingilia uhuru wa kuwa na maoni (kufikiri)
b) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa kujieleza (kutoa kauli)
c) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa habari (kupata habari zozote zinazohusu jamii zilizoko mikononi mwa serikali)
d) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa vyombo vya habari (kazi za utafutaji, ukusanyaji na usambazaji wa habari inayofanywa na waandishi wa habari na watangazaji)
e) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa kujumuika kwa amani (mikutano/maandamano ambavyo kihalisi ni njia za wanajamii kuwasiliana au kupeleka ujumbe kwa wahusika)

2. Kuhusu Mamlaka ya DPP
Katiba itamke kuwa:
a) Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ateuliwe na chombo huru cha uteuzi (siyo rais wa nchi) na athibitishwe na Bunge
b) DPP awajibike kwa Bunge (Chombo cha kutunga sheria)

3. Mapendekezo mengine
1. Katiba itamke kuwa ARDHI ni mali ya Watanzania. Isiwekwe chini ya rais bali iwe chini ya wananchi wa Tanzania. Serikali itakuwa tu na mamlaka ya kutwaa ardhi kwa ajili ya manufaa ya umma ambayo yameainishwa kama vile ujenzi wa miundombinu, utunzaji wa mazingira na uboreshaji makazi. Serikali isiwe na uwezo wa kutwaa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa mtu binafsi au kampuni kama inavyoelezwa sasa na Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999.

2. Katiba itamke kuwa kila kijiji kitakuwa na serikali ya kijiji ambayo itaongoza kijiji hicho pamoja na uwezo wa kutunga sheria ndogo na kuzipitisha chini ya usimamizi wa mkutano mkuu wa kijiji. Serikali za vijiji ndizo zitakuwa na mamlaka ya kusimamia na kulinda haki za wananchi juu ya umiliki wao wa ardhi ya kijiji na kupanga mipango ya matumizi ya ardhi. Zitakuwa na uwezo wa kutoza kodi na kuendesha miradi ya maendeleo vijijini.

3. Katiba itamke kuwa rasilimali za madini, mafuta, gesi na maliasili, ni mali ya Watanzania na ni lazima zitumike na kuvunwa kwa manufaa ya Watanzania. Serikali haitasaini mikataba bila kibali cha bunge; bali itakuwa na uwezo wa kutoa leseni za utumiwaji wake. Utoaji huo wa leseni lazima pia uwe wa wazi na ambao utaidhinishwa na Bunge.

4. Katiba itamke kwamba migogoro yote ya uwekezaji sharti isuluhishwe kwa mujibu wa sheria za Tanzania na Mahakama za Tanzania. Hili ni takwa la Kanuni ya makubaliano ya Calvo na vilevile Azimio Na. 1803 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la Mwaka 1962 na Azimio Na. 3281 la 1974 la Baraza hilo juu ya Haki na Wajibu wa Mataifa juu ya Maliasili.

5. Katiba itamke kuwa rais atachaguliwa kwa kupigiwa kura na kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura za watu wanaotakiwa kupiga kura. Yeye na serikali yake ni lazima awajibike kwa bunge na kila uteuzi anaofanya kwa nafasi za juu za uongozi, sharti uidhinishwe na bunge baada ya Bunge kuhojiana nao.
6. Katiba itamke kuwa Bunge lina madaraka na haki ya kumfuta kazi rais kwa kutowajibika au kwa kutumia madaraka yake vibaya.

7. Katiba itamke kuwa rais hatakuwa na haki au uwezo wa kulivunja bunge kwa sababu yoyote ile.

8. Katiba itamke kuwa rais hatakuwa na kinga dhidi ya mashitaka yoyote yale akiwa madarakani na baada ya kutoka madarakani. Mtu yeyote anaweza kufungua kesi dhidi yake binafsi au ofisi yake.

9. Katiba itamke kuwa uteuzi wa majaji wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa ufanywe na chombo huru (badala ya rais) na ufuate umahiri na uelewa wa sheria pamoja na uadilifu wa kimaadili na kisheria.

10. Katiba itamke kuwa mhimili wa Mahakama, ukiongozwa na Jaji Mkuu, ndio usimamie na kuwasilisha bajeti yake bungeni (badala ya serikali kama ilivyo sasa).

11. Katiba itamke kuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na viongozi wengine wakuu wa tume, wateuliwe na chombo huru cha uteuzi baada ya wanaotaka nafasi hiyo kuomba na kufanyiwa usaili. Aidha, maamuzi ya tume, kwa nafasi yoyote ile ya wagombea, yaweze kupingwa na mtu yeyote mahakamani.

12. Katiba itamke kuwa kukosa uadilifu au kutumia madaraka vibaya, kama itakavyothibitishwa na chombo husika, ni kosa la jinai.

13. Katiba itamke kuwa wote wanaojipatia utajiri kwa kuhujumu uchumi au watu wanaojitajirisha kwa kutumia madaraka yao ya umma, lazima washitakiwe kwa kosa la uhaini na mali zao zote, ikiwa ni pamoja na zile za walionufaika kutokana na kosa hilo, zitaifishwe.

14. Cheo cha Makamu wa Rais kiondolewe. Kibaki cha Waziri Mkuu.

15. Katiba itamke kuwa wakuu wa mikoa, wilaya (kama ni lazima kuendelea kuwa nao) wapatikane kwa kupigiwa akura ili w3aweze kuwajibika vema katika maeneo yao. Mameya wa miji na majiji nao wachaguliwe na wananchi moja kwa moja badala ya kuchaguliwa na madiwani.

16. Katiba itamke haki ya kuishi katika mazingira safi na salama lazima.

17. Katiba itamke kuwapo haki ya kufungua kesi za kutetea katiba, haki za binadamu na utawala wa sheria bila gharama zozote zile.

18. Katiba itamke kuwa elimu na afya ni haki kwa Watanzania wote.

19. Katiba itamke haki ya starehe.


Mwisho.


Saturday, January 12, 2013

KAMA TANZANIA HAINA DINI NI HUKO BARA SIYO ZANZIBAR- PROF ABDUL SHERIF

Prof Abdul Sherif

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetahadharishwa isilete hoja ya nchi kutokuwa na dini katika katiba ya nchi kwani Wazanzibari hawatakubali kupokonywa haki zao za kidini kama Mahakama ya Kadhi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar, Professa Abdul Sherif muda mfupi baada ya kutoka kwenye meza ya utoaji wa maoni mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaliofanyika juzi katika ukumbi wa Eacrotanal Mjini Unguja ambapo aliwasilisha maoni ya Baraza la Katiba Zanzibar.

Professa Sherif amesema mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayofanyika yazingatia suala la dini kwani katiba ya Tanzania inazungumzia serikali haina dini lakini katiba ya Zanzibar haina kifungu hicho na hivyo suala la dini waachiwe watu wenyewe badala ya kuingizwa katika katiba.

Alisema huenda kuingizwa kifungu hicho kunaweza kuleta matatizo hasa kwa kuzingatia Zanzibar ina asilimia 99 ya waislamu na hivyo hawawezi kukubali kufutwa mahakama yao ya kadhi ambayo wameikuta tokea miaka kadhaa ya wazazi wao.

“Kuwepo kwa kifungu cha katiba kuhusu dini kunaweza kuchochea suala hata la mahakama ya kadhi nadhani wazanzibari hawatakubali kuambiwa mahakama ya kadhi ifutwe sasa sisi tunashauri suala hili lisiingizwe katiba katiba” alishauri.

Professa Sherif ambaye ni bingwa wa historia na ameshawahi kupokea tunzo mbali mbali duniani kutokana na mchango wake mkubwa katika kuandika vitabu kadhaa vya historia amesema wazanzibari wana haki ya kuwa na mahakama ya kadhi kutokana na kuwa idadi yao ni kubwa na hivyo wana haki ya kujiamulia mfumo wa wanaoutaka katika kuendesha nchi yao.

Aidha alisema miaka kadhaa wazanzibari wameishi bila ya kutokea ugomvi wa aina yoyote kuhusiana na dini na ndio maana hata wakati wa utawala wa Uingereza kuna makanisa makubwa yalijengwa Zanzibar ambapo wakati huo wakristo walikuwa wachache mno lakini kutokana na kuheshimu dini nyengine utawala wa Sultan ambaye ni muislamu alithubutu kutoa kibali cha kujengwa makanisa.

“Miaka yote wazanzibari hawajawahi kugombana kwa habari ya dini wanagombana kwa mambo mengine lakini sio dini wamekuwa na uvumilivu mkubwa na kushirikiana na ndio maana kuna mahekalu, misikini na makanisa lakini watu wake hawagombani” alisema Professa Sherif.

Akizungumzia masuala mengine kwa ujumla alisema bunge la Tanzania halikuwa na haki wala mamlaka ya kupunguza au kuongeza mambo ya muungano ambao yalikubaliwa katika hati ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar zilipoungana ambapo awali yalikuwa mambo 11 tu.

Professa Abdul Sherif amesema mambo yaliongezwa yamefanyika kinyume cha sheria na hivyo yalioongezwa yote yamekuwa batili kwa mujibu wa sheria kwa kuwa bunge halikuwa na madaraka hayo.

Katika hatua nyengine Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimependekeza katika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwepo kwa mfumo wa serikali pamoja na kuwepo kwa fursa ya mgombea binafsi kuwania uongozi wa nchi badala ya mfumo uliopo sasa.

Akiwasilisha maoni yake mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba jana, Katibu wa chama hicho, Mussa Kombo alisema mfumo wa kuwepo kwa serikali tatu ndio utakaofaa kwa sasa pamoja na kupendekeza kuwepo kwa mgombea binafsi katika kuwania nafasi za urais nchini.

Alisema mfumo wa serikali tatu utasaidia kuondosha manungunuko na malalamiko yasiokwisha kati ya pande mbili hizo ambapo kwa miaka kadhaa sasa serikali imeshindwa kutafanyia kazi mambo ya kero za muungano.

“Sisi kama ZLS tunaona mfumo wa serikali tatu ndio unaofaa kwa sasa kuingizwa katika katiba mpya kuwepo na serikali ya Zanzibar na kuwepo na serikali nyengine jina lolote litakaloitwa na pia kuwepo na serikali ya muungano ambayo hiyo itakuwa ni ndogo itashughulikia masuala ya muungano tu” alisema Mussa nje ya mkutano wa utoaji wa maoni yaliofanyika ukumbi wa Eacrotanal Mjini Unguja.

Kombo alisema katiba mpya ianishe waziwazi hizo serikali tatu na mamlaka zake ili kusiwepo na utata kwani mfumo uliopo sasa haujaelezwa kikamilifu katika katiba na hivyo kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka pande mbili zilizoungana.

Aidha alisema ZLS imeona kuwepo na mgombea binafsi atakayewania nafasi ya urais kwani imani yao ni kwamba anaweza kupatikana kiongozi mzuri atakayetokana nje ya chama cha siasa.

“ZLS tunaamini tunaweza kupata kiongozi nje ya chama” alisema Kombo na kuongeza kwamba mambo mengine waliopendekeza na ZLS kuingizwa katika katiba mpya ni suala la uraia, ulinzi, sarafu, na uhamiaji ambayo yote yawe ni ya muungano na mambo mengine yaliobaki yasiwe na muungano.

Kombo alisema mambo ambayo sio ya muungano yanapaswa kuamuliwa kwa pamoja na kwa ridhaa ya pande mbili zilizoungana huku kila serikali iwe na chombo chake cha maamuzi ambapo walipendekeza kuwepo na bunge la Zanzibar, bunge la bara au vyovyotelitakavyotwa na kuwepo na bunge la pamoja.

Alisema tabia ya serikali ya upande mmoja kujiamulia na serikali ya pili kushindwa kutoa maamuzi haipendezi na hivyo wameshauri jambo lolote liamuliwe kwa pande mbili tena kwa makubaliano.

Akizungumzia suala la haki za binaadamu kuingizwa katika katiba Professa Chris Peter Maina wa Kituo Cha Huduma za Sheria Zanzibar, alisema haki zote za binaadamu ziwekwe katika katiba ikiwa pamoja na haki ya kupata elimu na afya iwe ni ya lazima pamoja na ile haki ya msingi ya kuishi.

Professa Maina alisema katika mpya ianishe haki ya kutumikishwa kwani kumekuwepo na tatizo kubwa la watu kuchukuliwa na kupelekwa nje ya nchi kutumikishwa na hivyo katiba iseme wazi kwamba haki hiyo ni ya msingi, ikiwa pamoja na haki ya kuandamana

Pia alipendekeza katika katiba mpya kuwepo na uhuru wa vyombo vya habari badala ya katiba ya sasa inavyosema uhuru wa kupata habari peke yake.

Mambo mengine aliyotaka yawemo katika katiba ni uhuru wa fikra na maoni iwe ni pake yake na uhuru wa dini na imani huku akipendekeza haki ya kupiga kura kwa watu waliofungwa au waliopo rumande na kulindwa kwa mali iliyopatikana kihalali.

Maoni mengine ya kituo hicho cha huduma za sheria ni pamoja na kuwepo wimbo wa taifa na alama za utaifa, lugha ya taifa, katiba iwe ndio juu ya kila kitu, ulinzi wa katiba na pia katiba ianishe nani mtanzania na aelezwe katika katiba.



KIGOMA; NDEGE YA ATCL YAPASUKA KIOO IKIWA ANGANI

Hii ndio ndege ya kwanza iliyopata ajali Kigoma
 
ZAIDI ya abiria 25 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la ndege nchini ATCL kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam wamenusurika kifo kutokana na ndege waliyokuwa wakisafiria kupata hitilafu ikiwa angani jambo lililomlazimu rubani wa ndege hiyo kufanya jitihada na kuirudisha kiwanjani.

Hali hiyo imetokana na moja ya vioo vya mbele vya ndege hiyo kupasuaka na hivyo kuruhusu upepo mkali kuingia ndani na hivyo kuwafanya marubani wa ndege hiyo kufanya kazi ya ziada kuhakikisha ndege hiyo inatua salama.

Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari yake ya kwanza mkoani humo ikiwa ni miezi 10 baada ya ndege nyingine ya shirika hilo kuanguka na kuharibika mkoani Kigoma.

Baadhi ya abiria waliokuwemo kwennye ndege hiyo, Athumani Batumwa na Fred Mbassa wamesema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ilipata itilafu ya kioo cha mbele kiasi cha dakika 30 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kigoma.

Kaimu meneja wa shirila la ATCL, Kepteni Milton Lazaro amekiri kutokea kwa hitilafu hiyo na amewaondoa hofu wasafiri juu ta tatizo hilo nakwamba ni sehemu ya matatizo yanayoweza kutokea kwa ndege yoyote.



MAHSUSI KWA WATU WA UJIJI



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU