Facebook Comments Box

Friday, December 28, 2012

BASI LA ABIRIA USO KWA USO NA LORI LEO

Basi la Abiria limegongana uso kwa uso katika eneo lijulikanalo kwa jina la PIPE LINE INYALA Mbeya baada ya Dereva wa Lori kulipita gari lingine mlimani na ndipo alipokutana na Basi hilo uso kwa uso. Zaidi ya abiria 40 wamenusurika kufa katika ajali hiyo, Dereva wa Lori ambaye ndiye aliyetajwa kuwa na makosa alikimbia kusikojulikana baada ya ajali hiyo na bado anasakwa kwa udi na uvumba.

SAKATA LA ELIMU FEKI: MULUGO YUPO TAYARI KUTHIBITISHA

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema yupo tayari kumthibitishia Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Joseph Mbilinyi, maarufu 'Sugu', juu ya elimu aliyonayo kama alivyodai mbunge huyo. Bw. Mulugo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madai ya Bw. Mbilinyi ambayo ameyatoa katika vyombo vya habari kuwa, Waziri huyo ana elimu ya kuunga unga na jina lake kamili ni Amim. Alisema kauli ya Bw. Mbilinyi haina ukweli wowote bali yeye ni msomi na yupo tayari kuthibitisha ukweli huo kwa umma. “Mimi na Bw. Mbilinyi tuna vilema vingi, akitaka tuumbuane yatabainika mengi hasa katika upande wake, namfahamu muda mrefu kwa sababu nimesoma naye shule moja, nafahamu mambo yake mengi lakini kutokana na hekima zangu sihitaji malumbano na yeye,” alisema Bw. Mulugo. Alidai kumshangaa Bw. Mbilinyi, kuzungumzia jambo ambalo halifahamu lakini kwa kumsaidia ili asielendelee kuonekana mwanasiasa muongo, aitishe mkutano na waandishi wa habari na yeye atakuwa tayari kuthibitisha elimu yake kwa umma. Bw. Mulugo aliongeza kuwa, ni kweli wakati anasoma alikuwa akitumia jina la Amim na baada ya kufika elimu ya juu alianza kutumia jina la Philipo ambalo ni la ukoo ambapo Bw. Mbilinyi kama angekuwa makini, angefuatilia kwenye ukoo wake ili kujua jina hilo linamuhusu au la. Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo hivi sasa linashikiliwa na Bw. Mbilinyi, mwaka 2015 linarudi CCM na ukweli huo utathibitika katika uchaguzi. “Mimi ni Waziri kutoka CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC, hivyo Bw. Mbilinyi, asifikiri kuzua maneno hayo yatanitisha hadi nishindwe kutekeleza sera za chama changu,” alisema. Alisema ibara ya 5 ya Katiba ya CCM, inamwongoza kuhakikisha chama chake kinashinda uchaguzi wa dola wa ngazi zote pamoja na kulirudisha jimbo la Mbeya Mjini kutoka upinzani. “Katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitatumia nguvu zote kuhakikisha jimbo la Mbeya Mjini linarudi CCM, ninachoweza kumshauri Bw. Mbilinyi, ajifunze kutokana na makosa kwani ameanza kunitafuta siku nyingi lakini mimi sikuwa na muda wa kumjibu bali niliendelea kutekeleza majukumu niliyonayo,” alisema. Alisema Mbunge huyo na chama chake walijibiwa na wananchi wa Saza katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Wilaya ya Chunya na kusahau kilichowapeleka ni kampeni hatimaye wakaanza kunadi elimu ya Mulugo badala yake waliambulia kufukuzwa. Aliongeza kuwa, Bw. Mbilinyi alipaswa kulisema na hilo kama walifukuzwa na wananchi wa Saza ambao walimwambia wao, wanamfahamu vizuri Bw. Mulugo na wamemsomesha wenyewe kwa pesa zao baada ya kuthibitika ni yatima. Alisema wananchi hao walidai kuchoshwa na matusi ya Bw. Mbilinyi dhidi yake na kumtungia uongo lakini yeye hana muda wa kulumbana naye bali atamjibu kwa ushahidi. Kauli ya Bw. Mulugo imekuja siku chache baada ya Bw. Mbilinyi kudai kuwa, elimu ya Waziri huyo ni ya kuunga unga kwani alisoma naye Sekondari ya Mbeya Day, wakati huo akiitwa Amim si Philipo Mulugo hivyo kuanzia sasa ataendelea kumuita jina lake halisi na kusisitiza hana uwezo wa kumng'oa jimboni kwake.

Tuesday, December 25, 2012

MARA HII URAIS WA MUUNGANO NI ZAMU YA ZANZIBAR

Imeandikwa na Stonetown (Kiongozi) Miaka mitatu kutoka sasa, Tanzania itafanya uchaguzi wake mkuu utaohitimisha miaka kumi ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Tanzania kama nchi nyengine duniani, inafata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katika mfumo wa vyama vingi, na iwapo kuna demokrasia ya kweli, basi ni matarajio yetu kuwa chama chchote kitakachoshinda kitapewa haki yake na ridhaa ya kuongoza nchi. Lakini pamoja na hayo, suali la uwiano wa Ugombea wa kiti cha Urais kwa pande mbili za Muungano, limekuwa likipuuzwa sana kuanikwa katika mijadala mbalimbali nchini. Suali la makubaliano ya mapokelezano ya wadhifa huu mkuu wa nchi baina ya sehemu mbili za Muungano, haujawekwa sawa na ni moja kati ya changamoto kongwe zinazoungana na mkururo wa kero za Muungano hapa nchini. Tangu tuungane, ni miaka takribani 49 sasa. Wakati Zanzibar ikiwa na marais saba tangu 1964, Jamhuri ya Muungano ndio inatimiza nusu tu ya wale waliokwisha tawala Zanzibar, ikiwa na marais wane tu hadi sasa. Mara baada ya Muungano, Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalim Julius Nyerere, alishika hatamu ya kuiongoza Jamhuri hadi pale ‘alipong’atuka’ madarakani kwa hiari yake mwaka 1984/85. Katika kipindi hichi cha miaka 20, Mwalimu hakuwahi kueleza wala kufafanua lolote kuhusu mpokezano wa madaraka kwa zamu baina ya nchi zetu hizi mbili. Naamini alifanya hivi sio kwa kutojua umuhimu wa kitendo hicho muhimu. Kitendo ambacho kingeashiria usawa mkubwa na haki inayosimamiwa na Muungano wetu. Mwalimu hakulijadili hili kwa sababu alijua wazi kufanya hivyo kungeviza ajenda yake binafsi ya kuimeza Zanzibar ndani ya matumbo ya Tanganyika na kuiondoa kabisa katika ramani ya dunia. Hili ndio lililokuwa lengo lake, bila shaka. Mungu akikupangia nakama, huna ujuzi wala ujanja. Kwani hayati Sheikh Abeid Karume, ambae ndie aliyekuwa Rais pekee wa Zanzibar aliekuwa akithubutu kumhoji na kumjibu Mwalimu lolote, lakini lakuvunda halina ubani, Sheikh Karume alikufa mapema mno. Tena wakati huo anakufa, bahati mbaya zaidi, ilikuwa Muungano huu haujawa na sura mbaya iliyo wazi wazi kama sasa, japo kiwingu cha dalili hizo mbaya kilianza kuonekana kwa mbali. Sheikh Karume akauwawa, na sababu ya kifo chake, ikafikichwa fikichwa, kisijulikane cha ukweli hadi leo.Ni begeje tu. Na kwanini, watu washuhulike na hili wakati, kufa kwa panzi ni neema ya kunguru? Aliekufa ndio kafa! Rais Jumbe, alijaribu kwa sana kuhoji hali kama hii. Lakini alichelewa mno.Na kwa jinsi Mwalimu alivyokuwa amejipanga kikazi kiulinzi na kiusalama, juhudi za Sheikh Jumbe zikawaka na moto. Zikaunguwa na kusakatuka kama kijungu cha dagaa tonge, kilichosahauliwa na mpishi aliekwenda kujisuka akisahau kuwa moto hauna sumile. Sheikh Jumbe akang’oka kama Mbuyu uliopigwa halbadiri ya mbayana. Akakunguzuka na mashina yake yote! Njia nyeupe! Baada ya majaribio haya mawili ya kujitokeza kwa Wazanzibari waliowakijifanya hawaogopi kumuhoji Nyerere, kilichofata ni mpango wa kudhibiti nani awe Rais wa Zanzibar. Ikawa Rais anaewekwa huku kwetu si katika yoyote anaeweza kuuhoji wala kuujadili Muungano, ‘imma faimma’ Nyerere awe hai, au awe ameshakufa. Na hili likafanikiwa. Bahati nzuri tu ‘Mtu si mbwa’. Hawa unaowaona walihoji kidogo wakaitwa ‘samaki’ na wavyele wao, ni matokezeo tu. Kwani haki haizami na dhulma haidumu. Viongozi wetu wa Zanzibar, ni watu waliopangwa maalum kufuata utaratibu waliopangiwa na wakubwa zao kule bara. Na kwa maana hii hakuna aliyewahi tena kuhoji kuhusu mgawano wa nafasi ya Urais wa Muungano. Ambapo, penye Uungwana na haki ndani ya Muungano huo, bila shaka tulikuwa tupokelezane zamu. Hata kama tuko katika mfumo wa vyama vingi kiasi gani. Kwa upande wa CCM bara, hili walikuwa walione pia. Hasa wao wakiwa kama chama chenya nguvu na chenye kushika hatamu. Ipo haja, tena bila kuzozana, kuipa nafasi Zanzibar kuongoza katika Jamhuri ya Muungano, tena katika wadhifa wa Urais, jambo ambalo linaonekana kuwa zaidi ya ndoto ya ‘Alinacha’ kwa sasa. Suali la kumpa Mzanzibari Urais wa Muungano ni ndoto ya Alinacha kwa sababu nyingi. Kwanza tuchukulie chama cha CCM kiwe na matumaini makubwa ya kushinda. Ukweli ni kwamba CCM na Muungano ni mtu na mama yake mzazi. Nasema ni mama kwa sababu hutokea watoto wasio baba kabisa, wala watu wengine, lakini hakuna mtoto asie na mama. Na mapenzi ya mama kwa motto hayana kifano chake. Na tunategemea vivyo hivyo kwa mtoto na mama yake. Kama haya ni kweli, na dhamira ya Muungano ni ile ile ya kuelekea nchi moja. Tena wakati ambao Wazanzibari wanahitaji ‘kupumuwa’ kwa nguvu zote. Hili ni gumu. Isitoshe, ukiwauliza zamu ya Zanzibar lini, wanakujibu kuwa Mwinyi alikuwepo hapa. Hivi Mwinyi ni Mzanzibari? Kwa kigenzo kipi? Na haya naawe huyo Mzanzibari kama ataamuwa kujinadi hivyo, lakini sula linabaki kuwa Marais wawili sasa, yaani miaka 20, Urais uko bara. Kuna ubaya tena gani wakitupa tena kumi, kama kweli tuna nia njema?Hapa panahitajika tuwe wakweli wadadisi kidogo juu ya hili. Ama kwa upande wa CHADEMA, naona wazo hili si mahala pake hata kidogo. Ingawa CCM na chadema lao moja, na ndio ukaona CHADEMA iliibuka tu kutoka katika ombwe, na kuja kuwa chama chenye nguvu hata kuliko CUF kule bara ambayo ilikuwa inaimarika vizuri siku hadi siku. Lengo, ni kuiondoa na kuizima nyota ya CUF kule wakiamini kuwa, kuanguka kwa CUF bara ni mafanikio makubwa ya kuzima nguvu ya wazanzibari kutaka kujitawala na ‘kupumuwa’. Na hili wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kuna kila dalili kuwa CHADEMA, hawana mpango na Zanzibar zaidi ya kuimaliza zaidi. Na kama hili linasomeka hivyo katika ajenda zao za siri, hawana mpango wa kumpa Mzanzibari nafasi yoyote ile hata ya Ubunge sembuse Urais. Na hii ni kwa sababu moja kuu: CHADEMA ni wabaya zaidi kuliko CCM, kwani ubaya wao haujifichi. Isitoshe, mfungamano wao mkubwa na kanisa ambalo kwa kiasi kikubwa ndio linaloipa kiburi CHADEMA, unaifanya hali ya uwezekano wa Zanzibar wa kuwa na nafasi kubwa kama hio katika Muungano kuwa ya tembo kupenya tundu ya sindano. Pamoja na hayo, tusikate tamaa. Ipo haja kwa kila mmoja wetu wakiwemo viongozi kuhoji nafasi ya Zanzibar katika uongozi wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Ijapokuwa tunaonekana kukubaliana na kuridhika kabisa na kitazonge, na changa la macho la kupewa kwetu Umakamo wa Rais. Nafasi ambayo haina athari yoyote kwa taifa zaidi ya kufunguwa vikao, kujulia wagonjwa na kuhutubia mikutano ya mazingira na Ukimwi. Pia tumeridhika na suala la Rais wetu kuwa Waziri katika Jamhuri ya Muungano, jambo ambalo haliingia akilini kabisa. Maana naamini wazi Makamo wa Rais bara, kiitifaki ni mkubwa zaidi kuliko Waziri, ambae pia ni Rais akiwa Zanzibar. Huu ni mchezo wa kitoto au wa kuku lala, tustiane majivu ya macho. Ukweli tunatakiwa tusitosheke na hapo. Tuhoji, tudai, na tutoe kauli moja, ‘Mara hii Urais wa Muungano, ni Zamu ya Zanzibar’. Tuwatazame na pumzi zao! Natoa hoja.

NBC’s Managing Director, Lawrence Mafuru resigns

The managing director of National Bank of Commerce (NBC), Mr Lawrence Mafuru, has resigned from the financial institution to which he had been reinstated about two months after a three-month suspension spell. Mr Mafuru was suspended by the board of directors in July to pave the way for investigations into alleged irregularities within the National Bank of Commerce (NBC).

The allegations which originated from a whistleblower report raised issues around irregular governance practices, fraud and corruption against the NBC executive management team. The statement issued upon his reinstatement in October, and which was signed by board chairman Dr Musa Assad, pointed out, in part, that, the board “had resolved appropriately all the matters arising out of the investigation.”

Mr Mafuru told The Citizen yesterday that his resignation starts effective December 24 as he looks for other opportunities, “I am a professional banker and think it is high time I pursued other opportunities outside the bank,” he said, adding: “After four years of a very progressive career at NBC, first as country treasurer since August 2007 and later as chief executive officer since June 2010 to date, I think that it is appropriate to seek other challenges elsewhere and allow others to steer the ship at NBC.”

The head of Marketing, Communications and Corporate Affairs at NBC, Ms Mwinda Kiula-Mfugale , confirmed to The Citizen that it was true that Mr Mafuru has resigned, but said she would issue a statement only after getting instructions from the board of directors.

Mr Mafuru was appointed managing director of one of the largest financial service providers in Tanzania in June 2010, succeeding Mr Christo de Vries from South Africa.

NBC is one of the oldest banks in Tanzania, tracing its origins to 1967 when the government nationalised financial institutions, including banks, before the banking industry was deregulated in 1991.
In 1997, NBC was split into three separate entities – NBC Holding Corporation, National Microfinance Bank (NMB) and NBC (1997) Limited.

In 2000, South Africa’s Absa Group Limited acquired a majority stake in NBC (1997) Limited. The government retained 30 per cent shareholding and the International Finance Corporation (IFC), a member of the World Bank Group, took a 15 per cent stake.

Speaking of the success he has had with the bank in the four years that he worked with it, Mr Mafuru remarked: “ I am very satisfied with the success I have had especially on the transformation agenda of NBC operations. We now have a much cleaner balance sheet, a stronger pool of talented young men and women; our customer experience has improved relative to where we are coming from and even more important we are well positioned for strong and sustainable growth in the next three years.”

He added: “On a personal note, I have had the opportunity to grow and develop professionally – I have grown both as business manager and a leader not only in the bank but also at industry level where I was privileged to serve as Chairman of Tanzania Bankers Association; I take pride that I also have been actively involved in shaping the future of banking in Tanzania.”



Tuesday, December 18, 2012

NDEGE KUBWA KUANZA KUTUA KIGOMA




NDEGE kubwa za abiria za kimataifa zinatarajiwa kuanza kutua Uwanja wa Ndege wa Kigoma kuanzia Desemba 15 mwaka huu baada ya uboreshaji wake kufikia hatua nzuri.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na blog hii mjini Kigoma, Meneja wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama wa Anga (TCAA), Godlove Hongore amesema hadi kufikia katikati ya mwezi ujao meta 1,450 za kuruka na kutua ndege zitakuwa zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami kati ya meta 1,800 zinazotarajia kujengwa.
Alisema mkataba wa ujenzi wa mkandarasi wa uwanja huo unaisha Juni mwakani lakini ujenzi umeelezwa na msimamizi wa Kampuni ya Synohydro ya China kwamba unaweza kukamilika mapema zaidi ya muda uliopangwa.
Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mkoani Kigoma, Elipid Tesha alisema mazungumzo yanaendelea vizuri ili kampuni hiyo ya Synohydro ya China iendelee na sehemu ya pili ya mradi huo katika mwaka ujao wa fedha utakaohusisha ujenzi wa njia ya kurukia ndege kufikia meta 3,000 na jengo la utawala na abiria uwanjani hapo.
Alisema tayari fedha za fidia kwa ajili ya eneo la makaburi ambalo litatumika kwa upanuzi huo, ipo na mazungumzo yanaendelea ni kuwezesha mkandarasi huyo kuendelea na sehemu hiyo ya pili ya mradi huo.
Meneja huyo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mkoa, alisema kukamilika kwa Awamu ya Pili ya ujenzi wa awanja huo kutaufanya Uwanja wa Ndege wa Kigoma kuwa na hadhi ya kimataifa na kuruhusu ndege kubwa zaidi ya tani 70 kutua.
Alibainisha kuwa uwanja huo ukikamilika, utakuwa kitovu cha ndege nyingi kutoka nchi za ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika ya Kati kwenda Kusini na Kaskazini mwa Bara la Afrika na nje ya bara hilo.


KIGOMA UJIJI YATOA MWANAFUNZI BORA WA SAYANSI

SHULE ya Sekondari ya Kichangachui katika Manispaa ya Kigoma Ujiji imetoa mwanafunzi bora wa masomo ya sayansi kwa Kanda ya Magharibi katika mtihani wa majaribio (Mock Test) wa kidato cha nne uliofanyika hivi karibuni.
Akitoa taarifa kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Chung IL aliyefika shuleni hapo kukabidhi rasmi maabara kwa uongozi wa shule hiyo Mkuu wa Shule hiyo, Harles Lugenda alisema kuwa mafanikio hayo yametokana na kuanzishwa kwa maabara ya masomo ya sayansi katika shule hiyo.
Lugenda alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Justus Ferdinand ambaye aliongoza katika masomo ya Fizikia na Kemia ambapo alisema kwamba kuwepo kwa maabara hiyo iliyoanza kufanya kazi Januari mwaka huu kumeinuka ari ya wanafunzi wa shule hiyo kusoma masomo ya sayansi na kuahidi kufanya vizuri.
Maabara hiyo imetolewa na serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo (KOICA) ambapo kiasi cha Sh milioni 25 zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa vyumba viwili vya madasara vinavyotumika kama vyumba vya maabara na vifaa vyake.
Sambamba na ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara pia Serikali ya Korea kupitia shirika hilo inagharamia masomo ya wanafunzi wanane wanaosoma masomo ya sayansi shule hapo ambapo tayari wameshalipiwa ada kwa miaka minne ahadi watakapomaliza masomo yao ya sekondari.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Balozi Chung IL alisema kuwa msaada huo umelenga kunaimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo baina ya serikali hizo mbili na watu wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispa ya Kigoma Ujiji , Alfred Luanda alisema kuwa pamoja na msaada huo bado Manispaa hiyo inakabiliwa na upungufu wa maabara za sayansi na vifaa vyake katika shule zake mbalimbali na kwamba kama ipo fursa ya kupata tena msaada zaidi aliomba serikali ya Korea kuangalia uwezekano huo.


BREAKING NEWS: MTU MMOJA AUWAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI KATI YA POLISI NA MAJAMBAZI KARIAKOO LEO HII

Mtu mmoja ameuwawa mida hii katika majibizano ya risasi yaliyotokea maeneo ya Msimbazi kariakoo, mtaa wa Livingstone kati ya Polisi na majambazi waliotaka kupora fedha zilizokuwa zinapelekwa benki ya NBC.

Majambazi hao waliokuwa wamevalia nguo za kiraia inasemekana walijua fedha hizo zinapelekwa leo hivyo walijiandaa kupora na Mapolisi nao waligundua hilo mapema hali iliyofanya majambazi hao kurusha risasi hovyo na kukimbia ili kukwepa kukamatwa.

Hadi sasa ni mtu mmoja anayeripotiwa kuuwawa ila bado haijajulikana kama ni raia au jambazi wale maana pia majambazi walivaa kiraia.


AKAMATWA NA UCHAWI MAHAKAMANI KISUTU

Kijana ambae ni mganga kutoka katika mkoa wa Tanga wilaya ya Muheza eneo la Kerege amekamatwa na vifaa ambavyo vinadaiwa kuwa vya kichawi ambavyo alikuwa akiingia navyo mahakamani ili kumfanyia uganga mmoja ya watu wanaokabiliwa na kesi katika mahakama hiyo. Polisi waliweza kugundua kupitia vifaa maalumu ambavyo vimefungwa mahakamani hapo. Picha hapo juu ni mganga huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi

Sunday, December 16, 2012

YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA



Kocha Brandts na wachezaji wake

MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC wanatarajiwa kuondoka Desemba 28, mwaka huu mjini Dar es Salaam, kwenda Uturuki kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa kwenda kutetea taji lao hilo mjini Kigali, Rwanda.
Habari kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba wiki hii mwalimu, Ernie Brandts ataamua idadi na wachezaji wa kwenda ziara hiyo, ambayo ni maalum pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Kocha huyo Mholanzi, kwa wiki zaidi ya mbili amekuwa akikinoa kikosi chake kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo fupi ya baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
Yanga, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Yussuf Manji imepania kurejesha utawala wake katika soka ya Tanzania na kwa kuanzia inataka kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kwa kishindo mwishoni mwa msimu.
Yanga inataka pia kutetea Kombe la Kagame Januari mwakani mjini Kigali, katika michuano ambayo watakwenda na wapinzani wao wa jadi, Simba SC.
Yanga ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ikiwa inaongoza kwa pointi zake 29, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 24, wakati Simba ni ya tatu kwa pointi zake 23.     


Saturday, December 15, 2012

TAARIFA YA BAVICHA KUHUSU UNDUMILAKUWILI WA DR SLAA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI, WANACHADEMA NA UMMA WA WATANZANIA JUU YA MWENENDO WA UNDUMILAKUWILI WA BWANA WILBROD PETER SLAA KATIBU MKUU WA CHADEMA TAIFA Ndugu wanahabari, Rangi nyeupe katika bendera chama changu ninachokipenda (CHADEMA) chama changu ninachokipenda inasimamia ukweli na uwazi. Rangi hiyo inawataka wanachadema wote kuwa wazi katika kulinda, kusimamia falsafa, itikadi na sera za chama chetu. Nimehuzunishwa sana ka kukatishwa tama na kitendo cha undimilakuwili na umamluki wa Katibu Mkuu Bwana Slaa kwa kitendo chake cha kuendelea kumiliki kadi ya Chama cha Mapinduzi wakati akitambua kuwa yeye ni Kiongozu anyeongoza harakati za chama Kikuu cha Upinzani hivyo kutakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuonyesha mwenendo bora kwa kuishi maisha anayohubiri. Katiba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sura ya tano ibara ya kwanza ndogo ya 5.1.6 kinachosema “Mwanachama wa CHADEMA asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA” Akitambua kadi ndicho chombo kikuu kinachomtambulisha mwanachama ndani yachama hivyo, kitendo cha kuendelea kumiliki na kulipia kadi Chama cha Mapinduzi kimedhihirisha kuwa yeye ni mbwa mwitu aliyejivika ngozi ya kondoo ndani ya upinzani. Bwana Slaa amekuwa akiaminisha Umma kuwa yeye ni Kiongozi mzalendo safi huku akiendelea kuwatuhumu baadhi ya wanachama na viongozi wenzie kuwa ni mapandikizi,Hivyo kitendo hicho cha yeye kumiliki na kulipia ya CCM imeonyesha kuwa yuko CHADEMA kwa kazi maalum ya kuhujumu harakati za Ukombozi hivyo hana na amepoteza sifa ya kuwa Kiongozi wa Upinzani. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ibara ya tano, BWANA WILBROAD PETER SLAA NI PANDIKIZI kutokana na sababu zifuatazo, ambazo nimejiridhisha nazo bila chembe ya shaka yoyote hivyo tunamuomba apishe uchunguzi dhidi yake ili tukiona dhamira njema tuendeleze harakati za Ukombozi yeye amepoteza sifa, kwa kitendo cha kuwa na Kadi ya chama ambacho kimetesa Watanzania na kuwanyanyasa lakini yeye bila aibu kukusanya kadi za wananchi wanaojiunga na CHADEMA kuzichoma moto na huku yeye akiwa amebaki na yake kibindoni hii imepelekea yeye kufanya kazi na umamluki na kukivuruga Chama kama ifuatavyo:- Amekuwa akitumika kugawa Mabaraza ya chama kwa kuidhinisha kumlipa mshahara Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Ndugu JOHN HECHE kinyume cha Katiba na mwongozo wa baraza la Chama ilihali Viongozi wengine wa Kitaifa wa mabaraza hata wale wa Mikoani na Wilayani hawalipwi chochote wakati wao ndio wanaohangaika kukijenga Chama. Hii inaonyesha Bwana Slaa analipa fadhila kwa mwenyekiti huyo ambaye maamuzi yote ya baraza huamiliwa na Bwana Slaa, Mfano huu wakulipana fadhila anaoufanya Bwana Slaa ni mfumo wa CCM ambako Slaa ni mwanachama na baada ya kukiri kwamba ni kweli anamiliki Kadi ya CCM hadi leo hii. Bwana Slaa ni Kiongozi anyejihusisha na vikundi vya majungu jambo ambalo ni kinyume na Katiba na kanuni ya Chama kwa kudhihirisha kwamba Bwana Slaa ni mamluki ndani ya CHADEMA aliyekuja kutimiza kazi maalumu amekuwa akichochea mgogoro na kuchukua maamuzi ya kuwafukuza baadhi ya vingozi ambao wamekiongoza chama kwa muda mrefu. Bwana Slaa alifukuza viongozi wa chama Geita. Alifukuza madiwani Arusha. Hapa Mwanza alishinikiza kufukuzwa kwa madiwani wawili CHAGULANI NA MATATAbila kuzingatia falsafa ya Chama kuamini katika nguvu ya umma kwamba wananchi ambao ndio wapiga kura wenye maamuzi juu ya hao Madiwani hawakushirikishwa katika kutoa maamuzi wakati wa kuwafukuza. Bwana Slaa amesababisha madiwani watatu kufukuzwa hapa Mwanza kwakuwakataza wasihudhurie vikao vya Halmashauri. Hivyo kwasababu kupoteza kata tatu (3) ambazo ni Ilemela, Nyamanoro na Kirumba. Kwa madai kwamba hawamtambui Meya MATATA. Pia Bwana Slaa amekuwa akivunja uongozi wa chama bila kuzingatia Katiba ya Chama kama Geita, Nyamagana, mvomero Morogoro Lindi na Mtwara bila kufata Katiba kama inavyoeleza Ibara ya 6.3 (b) mamlaka ya nidhamu na uwajibikaji, “kwamba kingozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au kuachishwa Uongozi na Kikao kilichomteuwa”Lakini yeye amekuwa akifukuza na kuvunja Uongozi katika sehemu mbalimbali za nchi bila kuzingaita misingi ya Katiba, Anaongoza Chama kwa Mfumo wa Hailakia kwamba atakalosema yeye ndio sheria na linalotakiwa kufuatwa na haitakiwi kuhoji. Slaa amekuwa akiwafukuza na kuwaita kwa kuwatukana mamluki Vingozi ambao wamejenga Chama kwa muda mrefu bila hata ruzuku leo hii chama kinapata ruzuku ya zaidi ya Milioni 200 wanaonekana hawafai licha ya kutopelekewa ruzuku majimboni mwao. Vilele Bwana Slaa amekuwa akilazimisha Viongozi wa Chama Mikoani kumpokea anaedaiwa kuwa mchumb wake bibi JOSEPHINE MSHUMBISI kama Kiongozi wa chama Taifa,mchumba wake amekuwa chanzo pia cha migogoro ndani ya chama kwani amekuwa akipeleka watu majimboni na kuagiza viongozi wa Chamawamtambue kama mgombea wa ubunge mwaka 2015, Pia amekuwa akitumia rasiliamali za chama vibaya katika ziara yake. Amekuwa akichangisha michango kwa kisingizio cha M4C ( vuguvugu la mabadiliko) Huku pesa hizo akizitumia kwa ajili ya taasisi yake yake binafsi iitwayo JUKWAA LA WANAWAKE kwa kifupi Josephine Mshumbusi haifahamiki kama ni mwanachama wa CHADEMA au La:- Hivyo Bwana Slaa hatuna imani nae kwani vitendo hivyo vyote vinatishia usalama wa Chama. Jambo lingine la kusikitisha kwa wana – nyamagana na Mwanza nzima kwa ujumla bwana Slaa amemteua Ezekiel wenje mbunge wa Nyamagana kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje makao makuu ya chama Dar es salaam hivyo wananchi wa Nyamagana hawana mbunge kwani kwa sasa anaishi Dar es salaam na kufanya kazi huko. Sasa hivi wana- nyamagana hawana tena mbunge kwani yuko Dar es salaam amekuwa mbunge wa makao Makuu. Ndugu waandishi ,katika kudhihirisha kuwa Wenje sasa hivi sio mbunge wa wanachi bali mbunge wa Makao Makuu, Ndugu Wenje haelewi suala lolote linaloendelea jimboni kwake kwani ninyi wanahabari ni mashahidi alipotoa tamko la Uongo mbele yenu akidai machinga wa Mwanza wamesema wanampa siku 14 Mkurugenzi wa Jiji awe amejiuzuru , jambo ambalo lilithibitisha kuwa ni la uzushi kwani SHIUMA (Shirika la Umoja wa Wamachinga). Lilimjibu na kumtaka afute kauli yake kwani hajazungumza wala kuwahi kuonana na wamachinga aache kuwachonganisha na Serikali kwa manufaa yake binafsi kwani hao wameendelea kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo wakishirikiana bega begani na Mstahiki Meya na madiwani wao. Ndugu wanahabari katika hili bwana Slaa hawezi kukwepa lawama hivyo basi kama ana uso wa aibu apishe kiti akae pembeni tujenge chama chetu. Ndugu wanahabari: Naamini mnakumbuka mwishoni mwa mwaka huu bwana Slaa alipokuwa anafanya ziara ya kukagua uhai wa Chama Mkoa wa Dar es saalm na majimbo yake alisikika akitekeleza na kuunga mkono mfumo kandamizi na unaofinya Demokrasia na utumiaji mbovu rasimali za nchi hii kwakuwa na wakuu wa Mkoa na Wilaya cha kustaajabisha na kushangaza bila aibu wala soni Bwana Slaa aliwataka viongozi wa Ngazi mbalimbali katika Jimbo la Kigamboni (Chadema) wawe tayari kupewa ukuu wa Wilaya na Mikoa Chadema itakapo kuchukua dola. Kitendo cha bwana Slaa kuendeleza sera za CCM kama kuwepo kwa wakuu wa Wilaya na Mikoa kinapingana moja kwa moja na sera na itikadi za CHADEMA. Kauli tata kama hii inamuhalalisha bwana Slaa kutumikia mabwana wawlili yaani CCM na CHADEMA ndio maana tunamtaka arudishe kadi ya Chadema na aendelee na Chama chake cha CCM anachotekeleza sera na itikadi zake. Ndugu Nadhani mnakumbuka tarehe 28 /10/2012 tulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani baada ya nafasi hizo kuachwa wazi kwa sababu mbalimbali. Katikauchanguzi ule CHADEMA iliambulia viti 5 (vitano) kati ya viti 29. Lakini baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa nini CHADEMA ilifanya vibaya katika uchanguzi mpaka kupelekea kupata viti vichache kiasi hiki wakati CHADEMA kwa sasa ni chama pendwa kwa Watanzania uchunguzi unaonyesha kwamba katika uchaguzi ule wa madiwani Bwana Slaa ambae alizunguka katika kata zote zilizokuwa zimeachwa wazi hakuwa na agenda ya kuhakikisha CHADEMA inashinda bali alibeba agenda yake binafsi na chama chake pendwa CCM NDIO maana Kanda ya ziwa CHADEMA tulishinda kwa asilimia 99 kwa sababu ya hujuma ya undumilakuwili Bwana Slaa. Ndugu wanahabari: Vyanzo vya mapato katika Vyama vya Siasa ni ruzuku kutoka Serikalini, michango mbalimbali kwa wadau, ununzi wa kadi za vyama kwa wanachama na kulipia ada ya uanachama katika vyama vyao. Bwana Slaa anakichangia CCM ili kiendelee kujiimarisha zaidi kwa kulipia ada ya uanachama . Kwa hio ujenzi na uimarishaji wa CCM unasaidiwa na uwepo wa Bwana Slaa na michango yake katika CCM. HITIMISHO:- Kutokana na mwenendo wa Bwana Slaa Wilbroad ninataka mwenyekiti wa Chama Taifa achukue maamuzi sahihi ya kutuepusha na janga hili ndani ya Chamamaana ni bora uwe moto au baridi kuliko kuwa vugu vugu endapo akishindwa tutaitisha maandamo nchi nzima maana Ni watanzania wazalendo wengi walioumia, kifilisika, na hata kupoteza maisha wakipigania ukombozi wa nchi hii, leo hii mamluki kama WILBROAD PETER SLAA hatuweai kukubali waturudishe nyuma katikaharakati za Ukombozi. Tunamtaka ajiuzuru haraka iwezekanavyo. Hakuna kulala mpaka kieleweke. …………………………….. MIMI SALVATORY MAGAFU KATIBU BAVICHA MKOA WA MWANZA. nakala:wajumbe wote wa BAVICHA TAIFA

Friday, December 14, 2012

KOFFI OLOMIDE NDANI YA DAR

Millard Ayo Koffi Olomide na Ben Kinyaiya kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere Dar es salaam decemba 14 saa saba na nusu usiku, Koffi Olomide amekuja Tanzania kupiga show mbili moja Leaders Dar decemba 15 2012 na 16 decemba Mwanza ambapo zote zimeandaliwa na Primetime promotions.
.


 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU