| Hii ni ofisi ya tanesco temeke ikiwa na bango linalo onesha huduma za dharura ni masaa 24 lakini ofisi hiyo imefungwa. |Ni masaa 24 kwa wiki? au walimaanisha nini kusema huduma ni masaa 24? |
Sunday, November 11, 2012
HII NI OFISI YA TANESCO TEMEKE
Saturday, November 10, 2012
HATIMAYE LORD EYEZ AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Tukio zima limefanyika double view hotel, sinza. Lord amewataka watu wasimhukumu na tuwe na subira hadi mahakama itakapoamua
Pia kasema anaandaa mchakato wa kuwachukulia hatua wote waliopotosha habari kwakuwa alishinikizwa kuonekana ameiba
BONGO STAR SEARCH
Salama katokelezeaaaaaa
Madam ritha tayari kwa shindano
Zantel's Director of Communications, Awaichi Mawalla
Madam ritha tayari kwa shindano
Zantel's Director of Communications, Awaichi Mawalla
AZAM WAMFUKUZA MCHEZAJI MWINGINE TENA
BEKI wa Azam FC, Aggrey Morris Ambroce amefukuzwa kwenye kambi
ya timu hiyo leo mjini Tanga, baada ya kuthibitika naye alipokea rushwa kutoka
klabu ya Simba ili kuihujumu timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara.
Aggrey ameondolewa kambini leo, siku moja tu baada ya kipa
Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni nao kusimamishwa kwa
tuhuma hizo.
Azam ilifungwa na Simba mabao 3-1 Oktoba 27, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam katika mechi za Ligi Kuu na baada ya hapo ikamfukuza kocha wake
Mserbia, Boris Bunjak na kumrejesha Muingereza, Stewart Hall.
Habari kutoka ndani ya Azam zimesema kwamba baada ya kupata
taarifa hizo, uongozi ulizifanyia kazi taratibu na kujiridhisha kabisa
wachezaji hao watatu walikula njama za kuihujumu timu katika mechi hiyo.
Kwa sababu hiyo, uongozi kwanza umewasimamisha wachezaji hao
na hatua zaidi zitafuatia baadaye.
Hata hivyo, Dida hakucheza mechi hiyo, kwani Oktoba 27,
kikosi cha Azam kilikuwa;
Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad, Aggrey Morris,
Abdulhalim Humud, Jabir Aziz aliyempisha Abdi Kassim, Himid Mao aliyempisha
Kipre Balou, John Bocco ‘Adebayor’ aliyempisha Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre
Herman Tcheche na Salum Abubakar.
Siku hiyo,
Azam walitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka
beki Mkenya Paschal Ochieng na kumchambua Juma Kaseja, kabla ya Felix Mumba
Sunzu Jr., kuisawazishia Simba dakika mbili baadaye, akiunganisha kwa kichwa
krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.
Okwi
aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni
mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni mwa timu hiyo na Mwinyi Kazimoto na
dakika tano tu tangu kuanza kipindi cha pili, Mganda huyo tena akawainua vitini
mashabiki wa Simba, akifumua shuti la umbali wa mita 19, baada ya kuwatoka
mabeki wa Azam.
Habari zaidi
zinasema kwamba, uchunguzi unaendelea kufanywa juu ya wachezaji wengine
wanaotuhumiwa kuwa katika mkumbo huo wa kuihujumu timu na ikithibitika ni
ukweli, watachukuliwa hatua pia bila kujali majina yao.
Azam tayari
iko Tanga tangu jana saa 8:00 mchana wa kwa ajili yao ya mchezo wao wa mwisho
wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya
Mgambo JKT, Uwanja wa Mkwakwani.
KAMATI YA SAIDIA SERENGETI ISHINDE RIDHIWANI KIKWETE NDANI
![]() |
| Ridhiwani |
Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:
1. Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo
2. Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.
Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
1. Ridhiwani Kikwete Mwenyekiti
2. Ahmed Seif (Magari) Mjumbe
3. Nassoro Bin Slum Mjumbe
4. Henry Tandau Katibu
5. Ahmed Mgoyi Mjumbe
6. Aboubakar Bakhresa Mjumbe
7. Angetile Osiah Mjumbe
8. Kassim Dewji Mjumbe
9. Abdallah Bin Kleb Mjumbe
10. Salim Said Mjumbe
Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia.
Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012.
BASI LA YANGA LAPASULIWA KIOO NA MTU ALIOVAA NGUO NYEKUNDU
![]() |
| Basi la Yanga |
BASI la Yanga limefanyiwa fujo na watu wasiojulikana, wanaosadikiwa
kuwa ni mashabiki wa Simba, eneo la Kabuku, wakiwa njiani kuelekea Tanga.
Baraka Kizuguto, Ofisa tovuti wa Yanga aliye katika msafara
wa timu ameiambia kitongoni mida hii kwamba, jamaa aliyerushwa jiwe alikuwa juu
ya mti na limepasua kioo, ila halijajeruhi mtu.
Amesema wametoa ripoti Polisi, ingawa hawakufanikiwa kumkamata
mtu kwa sababu wahusika walikuwa wamekwishakimbia baada ya tukio.
Yanga iliyoondoka leo alfajiri Dar es Salaam tayari ipo Tanga
, imefikia katika hoteli ya Central City, barabara ya Nane na jioni itafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Yanga iko Tanga kwa ajili mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji
Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili.
Yanga imepania kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika
mazingira mazuri katika msimamo wa Ligi Kuu, ambayo mzunguko wake wa pili
utarejea Januari mwakani.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa
sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam jana na wachezaji wake wote wapo
vizuri, chini ya kocha wake Mholanzi, Ernie Brandts.
Wchezaji wa
Yanga wamepania kuvunja rekodi ya Coastal Union kutofungwa kwenye Uwanja wao wa
nyumbani, Mkwakwani, Tanga katika mechi hiyo.
Akizungumza
na kitongoni kwa niaba ya wenzake mapema wiki hii, Nahodha Msaidizi wa
Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ alisema kwamba wanataka kustawisha uongozi
wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwafunga Coastal Jumamosi.
Alisema
wanajua Coastal ni timu nzuri na wanatarajiwa upinzani katika mechi hiyo, ila
ameonya Yanga ya sasa ni tishio na wachezaji wako vizuri ‘ile mbaya’.
“Kwa kweli
mimi na wachezaji wenzangu tunamshukuru mwalimu mpya (Ernie Brandts) kwa kutupa
vitu vipya na muhimu. Timu yetu imebadilika na kila mtu anaona sasa. Wale
Coastal si hawafungwi kwao wale, sasa sisi tutaenda kuwafunga pale pale, tena
kipigo kikali,”alisema.
Lakini pia
habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba tayari wachezaji wameahidiwa donge
nono iwapo watashinda mechi hiyo.
Wachezaji
hao, walizawadiwa Sh. Milioni 15 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mwishoni
mwa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Ushindi huo,
uliifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi
moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na
Simba SC yenye pointi 23, ambayo juzi imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini
Morogoro.
Thursday, November 8, 2012
AZAM YASIMAMISHA WACHEZAJI BAADA YA KIPIGO CHA SIMBA
Azam imeonekana kuingia katika mgogoro na wachezaji wake mahiri kwa madai kuwa walipewa pesa ili kuihujumu timu yao ili ifungwe na simba. Timu hiyo ilifungwa 3 kwa 1 na simba. Wachezaji walio simamishwa ili kupisha uchunguzi ni 1. Erasto Nyoni 2. Said Moradi 3. Deograatius Munishi a.k.a Dida
MAHAKAMA KUU YATOA UAMUZI KESI YA LEMA
Baadhi ya wananchi, wapenzi wa Chadema wakimlaki Mh Lema mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama.
Jopo la Majaji likiwa tayari kuanza kazi
Wananchi na viongozi wakiingia kuandikisha chumba cha mapokezi katika Ofisi ya Chadema Kinondoni, Dar es Salaam.
Pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufani kupitia Wakili wao Alute Mughwai ili rufaa ya Lema kupinga kuvuliwa ubunge isisikilizwe limetupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kuridhika kwamba kosoro zilizolalamikiwa zilikuwa kwa upande wa Mahakama.
Pia kifungu kilichomhukumu Lema kina makosa hivyo kesi itatajwa tena baada ya siku 14 kwa ajili ya kuendelea kusikiliza hoja za walio kata rufaa.
Wadaiwa kwenye shauri hilo ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matu
Lema anawakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, anayesaidiana na Tindu Lissu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Kijana Walter Chilambo ameibuka mshindi katika shindano la kutafuta vipaji la Epiq Bongo Star Search. Walter alionekana kukua kila siku wakati akiwa katika jumba hilo la kujifundishia muziki. Tofauti na miaka iliyopita watu wengi wameufurahia ushindi wa Walter. Mshindi wa pili umeenda kwa Salma na watatu ni Wababa.





