Facebook Comments Box

Monday, September 17, 2012

MWAKYEMBE AENDA KUINGIA MKATABA BERLIN

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia tarehe 15 hadi 19 septemba kwa ziara ya kikazi. Moja ya tukio muhimu atakalo lifanya huko ni kusaini mkataba wa ushirikiano wa usafiri wa anga (Bilateral Air Service Agreement- BASA) baina ya nchi ya Tanzania na Berlin tarehe 17 septemba 2012. Tarehe 16 septemba Mheshimiwa alitembelea maonesho ya kimataifa ya sekta ya usafiri wa anga yaliyofanyika Berlin.
Mh Mwakyembe akiwa ndani ya moja ya ndege zilizokuwa kwenye maonesho hayo

Mh akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa ndege za Airbus

Mh Mwakyembe akipiga picha na Balozi wa Tanzania Berlin Mh Ahmada (kushoto) na Afisa wa wizara ya uchuzi Ndg Ubwa (kulia)


Mh waziri akifanya mazungumzo na viongozi wa sekta ya anga wa Berlin



NYUMBU WARUDI SERENGETI KUTOKA MAPUMZIKONI






Msafara maarufu kwa jina la "Annual Animal Migration" unaohusisha wanyama aina ya Nyumbu wakiwa wanarudi katika mbuga ya Serengeti ya Tanzania wakiwa wanatoka katika mbuga ya Masai mara ya Kenya. Nyumbu hao walisafiri umbali wa zaidi ya kilometa 1000 katika mapumziko yao hayo. Msafara huo ambao ni maarufu zaidi duniani umevuta watalii wengi. Mwaka huu Nyumbu hao wamewahi kurudi kutokana na mvua zilizowahi kunyesha nchini Tanzania ambazo zimewawekea mazingira mazuri ya chakula. Nyumbu hao hukutana na mikasa na mazingira magumu wakati wa safari yao hiyo ambapo huwabidi kukatiza katika mto ambao una mamba na viboko ambao nao huwafanya msosi. Nyumbu hao waliorudi wanakaribia kuwa zaidi ya milioni moja na laki tano na huu ni msafara wa awali.

PICHA ZA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU

Polisi wa kutuliza ghasia akimzuia mwananchi

Waangalizi wa usalama wakiwa kazini


Mawakala wa vyama wakifuatilia zoezi zima la upigaji kura

Mmoja ya wanasiasa akiongea na waandishi wa habari



Sunday, September 16, 2012

CHAMA CHA MAPINDUZI CHA SHINDA UBUNGE JIMBO LA BUBUBU

Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Bububu







Chama Mgombea Ubunge Kura %

1
CCMMasolwa Masolwa COSMAS 5,29656.3%
2
CUFSoud Khamis RASHID 3,80440.4%
3
JAHAZIIdrissa Mohammed ALI 550.58%
4
SAURashid Ali ALI 170.18%
5
TADEASalum Seif SEIF 160.17%
6
UPDPSaid Ahmad ASHA 120.12%
7
PPTOmar Said AYOUB 90.09%


ZILIZOHARIBIKA1952.07%


Jumla9,404








BREAKING NEWSS! STEVE NYERERE APATA PIGO.

Msanii wa maigizo na mchekeshaji mkongwe kutoka Bongo Movie Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere amepata pigo la kufiwa na mtoto wake leo hii maeneo ya kinondoni, kwa sasa Steve yupo kwenye ziara ya Tamasha la  Serengeti fiesta 2012.



CLOUDS MEDIA NA WASANII WA BONGO FLEVA NA BONGO MOVIES WATOA MSAADA DODOMA

Picha ya pamoja ya uongozi wa Clouds Media na Wasanii wa Bongo Fleva na Wasanii wa Bongo movies wakiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini na watoto wa kituo cha The Village of Hope pamoja na walezi wao cha Mkoa wa Dodoma
Msanii Diamond akiwasalimia watoto wa kituo hicho pamoja na kuwaimbisha nyimbo zake
Father Vicent Boselli akitoa maelezo ya kituo hicho kwa wasanii na viongozi wa Clouds Media


Baadhi ya walezi wakiwa wamebeba watoto wa kituo hicho

Anti Ezekiel akijitambulisha huku akiwa amembeba mmoja ya watoto wanaolelewa na kituo hicho

Wasanii Juma Nature na Shettah wakisalimia watoto wa kituo hicho

Hapa wakikabidhi misaada mbalimbali


Baadhi ya wanafunzi wa kujitolea kutoka maeneo mbalimbali duniani wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo hicho

Misaada akiingizwa ndani



Saturday, September 15, 2012

MATOKEO YA LIGI YA UINGEREZA BAADA YA MECHI ZOTE KUISHA

England - Premier League
 19:46September 15 

 FTNorwich C.0 - 0West Ham U.

 FTArsenal6 - 1Southampton

 FTAston Villa2 - 0Swansea C.

 FTFulham3 - 0West Bromwich A.

 FTManchester U.4 - 0Wigan Athletic

 FTQueens Park R.0 - 0Chelsea

 FTStoke C.1 - 1Manchester C.

 FTSunderland1 - 1Liverpool


ALIE ANDAA FILAMU YA KUMKASHIFU MTUME MUHAMMAD (SAW) AKAMATWA NA POLISI




HAPA NDIPO WALIPO KUTANA HENRY STANLEY NA DAVID LIVINGSTONE


Hapa ndipo walipo kutana ilikuwa chini ya muembe. Wazee wa ujiji wanasema muembe huo ulikatwa na kutengenezwa hiki kibaraza na sio muembe unao onekana nyuma ya picha hii


Mwaka 1871 hapa ndipo walipokutana Henry Stanley na david Livingstone Ujiji


Kijana Ibrahim Fivawo kutoka Dar Es Salaam akifanya utalii wa ndani katika sanamu la Henry Stanley na David Livingstone mjini Ujiji



LIVE SCORE: YANGA 0-0 TANZANIA PRISONS - SIMBA 3-0 AFRICAN LYON- AZAM 1-0 KAGERA SUGAR


FT YANGA 0 - 0 TANZANIA PRISONS
Kavumbangu ametoka ameingia Hamis Kiiza 

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
Mpira ni mapumziko, Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
DK 80: Yanga 0- 0 Prison
DK 30: Yanga 0-0 Prisons

FT SIMAB 3-0 AFRICAN LYON
Uwanja wa taifa Dar -Emmanuel Okwi anaifungia Simba bao la 3. Mpaka sasa Simba 3 African Lyon 0
 Emmanuel Okwi na Chollo wanaipa Simba uongozi wa 2-0 dhidi ya African Lyon -ambao wamekosa penati muda mfupi uliopita ikipigwa na Sammy Kessy.

DK 25: Mpira ume-balance na kila timu ikicheza kwa umakini kuzuia kufunga goli la mapema.

 DK: 10 - Prisons 0 - 0 Yanga

FT AZAM 1 - 0 KAGERA SUGAR
     AZAM 1 - 0 KAGERA SUGAR 

FT JKT OLJORO 1 - 1 TOTO AFRIKA
JKT Oljoro 1- 1 Toto Afrika
JKT Oljoro 1 - 0 Toto Afrika

*******************************************************

1.Ally Mustafa 'Barthez' 1
2.Juma Abdul - 14
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Mbuyu Twite - 9
7.Nizar Khalfani - 7
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11

10.Didier Kavumbagu - 21
11.Stephano Mwasika - 3

Subs
1.Yaw Berko - 19
2.Shadrack Nsajigwa - 2
3.David Luhende - 29
4.Athuman Idd Chuji - 24
5.Shamte Ally - 15
6.Saimon Msuva - 27
7.Hamis Kiiza Diego - 20

Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Manager: Hafidh Saleh
Kit Manager: Mahmoud Omary 'Mpogolo'
Massagist: Jacob Onyango
Team Doctor: Dr Suphian Juma
TANZANIA PRISONS
1: Daudi Abdallah
2:  Henry Mwalungala
3: Laurian Mpalile
4: Lugano Mwangama
5: David Mwantika
6: Khalidi Fupi
7: Sino Agustino
8: Fred Chudu
9: Elias Magali
10: Peter Micheal
11: Ramadhan Katamba


Friday, September 14, 2012

KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANGOSI YAIBIWA

Marehemu Daudi Mwangosi.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.
Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”
Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU