Saturday, September 15, 2012
HAPA NDIPO WALIPO KUTANA HENRY STANLEY NA DAVID LIVINGSTONE
| Hapa ndipo walipo kutana ilikuwa chini ya muembe. Wazee wa ujiji wanasema muembe huo ulikatwa na kutengenezwa hiki kibaraza na sio muembe unao onekana nyuma ya picha hii |
| Mwaka 1871 hapa ndipo walipokutana Henry Stanley na david Livingstone Ujiji |
| Kijana Ibrahim Fivawo kutoka Dar Es Salaam akifanya utalii wa ndani katika sanamu la Henry Stanley na David Livingstone mjini Ujiji |
LIVE SCORE: YANGA 0-0 TANZANIA PRISONS - SIMBA 3-0 AFRICAN LYON- AZAM 1-0 KAGERA SUGAR
FT YANGA 0 - 0 TANZANIA PRISONS
Kavumbangu ametoka ameingia Hamis Kiiza
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
Mpira ni mapumziko, Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
DK 80: Yanga 0- 0 Prison
FT YANGA 0 - 0 TANZANIA PRISONS
Kavumbangu ametoka ameingia Hamis Kiiza
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
Mpira ni mapumziko, Tanzania Prisons 0 - 0 Young AfricansKavumbangu ametoka ameingia Hamis Kiiza
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza,Tanzania Prisons 0 - 0 Young Africans
DK 30: Yanga 0-0 Prisons
FT SIMAB 3-0 AFRICAN LYON
Uwanja wa taifa Dar -Emmanuel Okwi anaifungia Simba bao la 3. Mpaka sasa Simba 3 African Lyon 0
Emmanuel Okwi na Chollo wanaipa Simba uongozi wa 2-0 dhidi ya African Lyon -ambao wamekosa penati muda mfupi uliopita ikipigwa na Sammy Kessy.
DK 25: Mpira ume-balance na kila timu ikicheza kwa umakini kuzuia kufunga goli la mapema.
DK: 10 - Prisons 0 - 0 Yanga
FT AZAM 1 - 0 KAGERA SUGAR
AZAM 1 - 0 KAGERA SUGAR
FT JKT OLJORO 1 - 1 TOTO AFRIKA
JKT Oljoro 1- 1 Toto Afrika
JKT Oljoro 1 - 0 Toto Afrika
*******************************************************
1.Ally Mustafa 'Barthez' 1
2.Juma Abdul - 14
3.Oscar Joshua - 4
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (C) - 23
5.Kelvin Yondan - 5
6.Mbuyu Twite - 9
7.Nizar Khalfani - 7
8.Haruna Niyonzima - 8
9.Said Bahanunzi - 11
10.Didier Kavumbagu - 21
11.Stephano Mwasika - 3
Subs
1.Yaw Berko - 19
2.Shadrack Nsajigwa - 2
3.David Luhende - 29
4.Athuman Idd Chuji - 24
5.Shamte Ally - 15
6.Saimon Msuva - 27
7.Hamis Kiiza Diego - 20
Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Manager: Hafidh Saleh
Kit Manager: Mahmoud Omary 'Mpogolo'
Massagist: Jacob Onyango
Team Doctor: Dr Suphian Juma
11.Stephano Mwasika - 3
Subs
1.Yaw Berko - 19
2.Shadrack Nsajigwa - 2
3.David Luhende - 29
4.Athuman Idd Chuji - 24
5.Shamte Ally - 15
6.Saimon Msuva - 27
7.Hamis Kiiza Diego - 20
Head Coach: Tom Saintfiet
Assistant Coach: Fred Felix Minziro
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Manager: Hafidh Saleh
Kit Manager: Mahmoud Omary 'Mpogolo'
Massagist: Jacob Onyango
Team Doctor: Dr Suphian Juma
TANZANIA PRISONS
1: Daudi Abdallah
2: Henry Mwalungala
3: Laurian Mpalile
4: Lugano Mwangama
5: David Mwantika
6: Khalidi Fupi
7: Sino Agustino
8: Fred Chudu
9: Elias Magali
10: Peter Micheal
11: Ramadhan Katamba
Friday, September 14, 2012
KAMATI ILIYOUNDWA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANGOSI YAIBIWA
Ikiwa ni siku moja tu baada ya
kufikishwa Mahakamani kwa askari polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya
mwandishi wa habari Iringa Daudi Mwangosi, Kamanda wa polisi Iringa
Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa wizi uliofanywa kwa kamati
iliyoundwa kuchunguza kifo hicho.
Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”
Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.
Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”
Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.
Thursday, September 13, 2012
MADAKTARI NAIROBI WAGOMA TENA
| NAIROBI |
September 13 2012 Madaktari wote wa hospitali za Serikali Kenya wanatarajia kuanza kugoma kwa sababu serikali haijafanya kama wanavyotaka, yani kuongezewa mishahara.
Katika vichwa mbalimbali vya habari nchini Kenya Mtangazaji William Tuva wa Citizen Radio na Citizen Tv ameripoti pia kwamba baada ya vurugu kuendelea kati ya makabila ya Waorma na Wapokomo kwenye wilaya ya Tana River ambapo inaaminika zaidi ya watu 100 wamefariki dunia wakiwemo Polisi, Mbunge wa Galole ambae ni Naibu Waziri Godana amekamatwa na polisi na kupelekwa Mahakamani akidaiwa kuwa mmoja ya watu wanaohusika na uchochezi wa hizo vurugu, baadae aliachiwa kwa dhamana ya shilingi laki nne za Kenya.
Vurugu za sasa kwenye wilaya ya Tana River zimehusisha watoto pia kuuwawa kikatili na nyumba kuchomwa ambapo wataalamu wa mambo wanasema vurugu hizi zinahusika na siasa, yani kuna wanasiasa wanachochea kwa sababu uchaguzi mkuu unakaribia.
Kwenye sentensi nyingine William Tuva ameamplfy kuhusu mlipuko uliotokea Mogadishu Somalia kwenye hoteli aliyokuwemo rais mpya wa Somalia pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri lakini hao viongozi wote wamenusurika, waliopoteza maisha ni watu wengine saba.
Waziri huyo wa mambo ya nje alikwenda Somalia kumwakilisha Rais Mwai Kibaki kutoa pongezi kwa rais mpya wa Somalia
Wednesday, September 12, 2012
RAIS KIKWETE AKIWA KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI NCHINI KENYA
SIMBA WACHUKUA NGAO YA HISANI
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Mkongoro Mahanga akimkabidhi Ngao ya Hisani
nahodha wa Simba, Juma Kaseja baada ya kuifunga Azam FC 3-2 katika
mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam
| Add caption |
Mshambuliaji
wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Azam FC, Aggrey Morris katika
mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam. Simba imeshinda 3-2. Mapato ya mchezo huo yataelekezwa katika
shughuli za kijamii Hospitali ya Temeke.
Mashabiki wa Simba
![]() |
| Akuffo akijaribu kuleta simanzi kwenye lango la Azam |
Heka heka katika lango la Azama FC
SIMBA KUJIONDOA LIGI KUU
Mwandishi wa habari za michezo Shaffih Dauda ameripoti kwamba Siku moja baada ya kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF kutoa maamuzi juu ya mapingamzi ya Simba dhidi ya wachezaji Kelvin Yondani na Mbuyu Twitte kuichezea klabu Yanga – kwa kuwaidhinisha wachezaji hao kuichezea Yanga. Leo hii klabu ya Simba imesema inafikiria hatua za kuchukua juu ya uamuzi huo wa kamati ya Alex Mgongolwa.
Kwa taarifa za kuaminika alizozipata Shaffih kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kwamba kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakutana usiku wa leo (sept 11) kujadili hatua za kuchukua huku baadhi ya wajumbe wakisema kutokana na uonevu wanaotendewa na TFF itabidi wajitoe kushiriki kwenye ligi kuu kwa sababu hawana imani na shirikisho hilo.
Simba inalalamika kwamba wachezaji wote wawili Mbuyu Twitte na Kelvin Yondan wamesajiliwa na Yanga isivyo halali. Kwa upande wa Twitte walitaka walipwe fedha zao $32,000 walizompa mchezaji huyo na akasaini nao mkataba kabla ya Yanga kuwazidi kete na kumsainisha mkataba mpya beki huyo aliyekuwa akiichezea APR ya Rwanda, na pia walitaka Twitte afungiwe kwa sababu alisaini mkataba na kalbu zote mbili kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kwa upande wa Yondani Simba wanadai mchezaji huyo ni halali yao kwa sababu bado ana mkataba na klabu hiyo, pia wakataka Yanga iadhibiwe kwa kitendo cha kufanya mazungumzo na mchezaji ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya zamani lakini jana kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF ikatoa maamuzi ya kuwaidhinisha Twite na Kelvin Yondan kwenda Yanga, maamuzi ambayo Simba wamesema sio sahihi.
Subscribe to:
Posts (Atom)





