Facebook Comments Box

Thursday, August 30, 2012

MBUYU TWITE ATUA DAR

Mbuyu Twite akiongozwa na viongozi wa Yanga kuelekea kwenye gari
Hawa ni washabiki wa Yanga waliofika kumpokea Mbuyu Twite


Mbuyu Twite akiwa amevaa Jezi namba 4 Iliyoandikwa Rage akihojiwa na waandishi wa habari

Mmoja wa washabiki wa Yanga akiwa na jezi namba 4 iliyo andikwa Rage
Wakati huo huo kocha wa Yanga Tom amefanya kikao na waandishi wa habari na kukanusha habari iliyo andikwa katika website ya super sports kuwa hafurahii mazingira ya kazi nani ya ya klabu hiyo ya Yanga.
Amesema anavutiwa na mazingira yake ya kazi na ushirikiano anaopata kwa viongozi wa mabingwa hao wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati.

KIZUNGU CHA OYSTER-BAY.




HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA

Marehemu Hawa Ngurume akitoa maelezo ya ugonjwa wake kwa mwandishi wa habari

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbalali, Bagamoyo na Kinondoni na Mkoani Iringa Hawa Ngurume. Amefariki leo Asubuhi. Mama huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo.
Ugonjwa huo ulimsumbua kwa muda ambapo ilifanya atibiwe katika Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali nyingi za binafsi.
Marehemu atakumbukwa kwa uchapa kazi na uongozi wake mzuri na usikivu na uunganishaji wa wananchi na uhamasishaji wa maendeleo.
Sote ni wa Mungu na kwake tutarejea.

MAGAZETI YA LEO AGOSTI 30















TUSIPO LIKEMEA HILI TUTARAJIE AJALI MBAYA UBUNGO




MH KIKWETE NDANI YA BBC SWAHILI TV




ANGALIA MAGOLI YA MADRID WALIPO ICHAPA BARCELONA NA KUCHUKUA KOMBE


Real Madrid 2-1 Barcelona - Highlights by simaotvgolo12

MESSI NA C.RONALDO HAWAKUPEANA MIKONO BAADA YA MECHI




Wednesday, August 29, 2012

MBUYU TWITE KUWASILI KESHO

Mchezaji alieleta mtafaruku mkubwa katika usajili wake atawasili kesho majira ya saa tisa alasiri. Msemaji wa Young Africans Sports Club Luis Sendeu ameomba washabiki na wapenzi waote wa yanga kujitokeza kumpokea mchezaji huyo. Sendeu pia amehabarisha kuwa suala la Mbuyu kukamatwa wao wanaona ni kama porojo tu.Wakati huo huo timu ya Young Africans Sports Club inatarajiwa kujitupa uwanjani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kupambana na Coast Union ya Tanga.
Mbuyu Twite akiitumikia Yanga huko Rwanda

Mbuyu Twite akisaini Yanga mbele ya Bin Kleb



AKUFFOR NA NGASSA WAING`ARISHA SIMBA ARUSHA

Daniel Akuffor akikabidhiwa jezi ya simba wakati wa usajili
Simba wameibuka kidedea baada ya kutoka kifua mbele kwa mabao mawili kwa moja. Mabao ya Simba yalifugwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Ghana Daniel Akuffor na mshambuliaji aliehamia hapo ktoka Azam FC Mrisho Khalfan Ngassa. Goli la Ngassa lilifungwa kwa tictak.

BABA LEVO,LINEX NA SUMA LEE WAPATA AJALI KIGOMA

Wasanii wa bongo fleva Baba levo Linex na Suma lee wamepata ajali wakati wakielekea katika show yao kigoma. Ajali hiyo ilitokana na basi lililokuwa limepaki katikati ya barabara kwenye kona. Gari la wasanii hao lilikuwa linaendeshwa na Suma lee ambae ndio mmiliki wa gari hilo. mtu mmoja tu ambae ni dancer wa suma lee yeye ndio alie umia mguu tu. Suma lee alijaribu kulikwepa gari hilo ndipo akashindwa kulimudu gari vizuri kitu kilichosababisha kutoka nje ya barabara na kugonga mti. Linex anasema kitu kilichosababisha kusiwe na majeruhi ni mwendo ambao dereva alikuwa akiendesha ulikuwa sio mkali sana. Wasanii hao watakuwa na show kigoma Jumamosi na Jumapili baada ya hapo wataenda Bujumbura kwa shows mbalimbali.
Kitongoni tunawapa pole na safari njema
Linex

Baba Levo



 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU