Thursday, August 30, 2012
HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA
![]() |
| Marehemu Hawa Ngurume akitoa maelezo ya ugonjwa wake kwa mwandishi wa habari |
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbalali, Bagamoyo na Kinondoni na Mkoani Iringa Hawa Ngurume. Amefariki leo Asubuhi. Mama huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo.
Ugonjwa huo ulimsumbua kwa muda ambapo ilifanya atibiwe katika Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali nyingi za binafsi.
Marehemu atakumbukwa kwa uchapa kazi na uongozi wake mzuri na usikivu na uunganishaji wa wananchi na uhamasishaji wa maendeleo.
Sote ni wa Mungu na kwake tutarejea.
Wednesday, August 29, 2012
MBUYU TWITE KUWASILI KESHO
Mchezaji alieleta mtafaruku mkubwa katika usajili wake atawasili kesho majira ya saa tisa alasiri. Msemaji wa Young Africans Sports Club Luis Sendeu ameomba washabiki na wapenzi waote wa yanga kujitokeza kumpokea mchezaji huyo. Sendeu pia amehabarisha kuwa suala la Mbuyu kukamatwa wao wanaona ni kama porojo tu.Wakati huo huo timu ya Young Africans Sports Club inatarajiwa kujitupa
uwanjani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kupambana na Coast
Union ya Tanga.
![]() |
| Mbuyu Twite akiitumikia Yanga huko Rwanda |
![]() |
| Mbuyu Twite akisaini Yanga mbele ya Bin Kleb |
AKUFFOR NA NGASSA WAING`ARISHA SIMBA ARUSHA
![]() |
| Daniel Akuffor akikabidhiwa jezi ya simba wakati wa usajili |
BABA LEVO,LINEX NA SUMA LEE WAPATA AJALI KIGOMA
Wasanii wa bongo fleva Baba levo Linex na Suma lee wamepata ajali wakati wakielekea katika show yao kigoma. Ajali hiyo ilitokana na basi lililokuwa limepaki katikati ya barabara kwenye kona. Gari la wasanii hao lilikuwa linaendeshwa na Suma lee ambae ndio mmiliki wa gari hilo. mtu mmoja tu ambae ni dancer wa suma lee yeye ndio alie umia mguu tu. Suma lee alijaribu kulikwepa gari hilo ndipo akashindwa kulimudu gari vizuri kitu kilichosababisha kutoka nje ya barabara na kugonga mti. Linex anasema kitu kilichosababisha kusiwe na majeruhi ni mwendo ambao dereva alikuwa akiendesha ulikuwa sio mkali sana. Wasanii hao watakuwa na show kigoma Jumamosi na Jumapili baada ya hapo wataenda Bujumbura kwa shows mbalimbali.
Kitongoni tunawapa pole na safari njema
Kitongoni tunawapa pole na safari njema
![]() |
| Linex |
![]() |
| Baba Levo |
Tuesday, August 28, 2012
CHADEMA YASEMA POLISI HAIWEZI KUKWEPA LAWAMA YA MAUAJI
Chadema imesema kuwa polisi haiwezi kukwepa lawama juu ya kifo cha kijana Ally Zona mwenye umri wa miaka 38 kilichotokea huko Morogoro. Vilevile CHADEMA kimesitisha maandamano katika Mkoa wa Iringa kupisha zoezi la sensa. akizungumza na waaandishi wa habari katibu mkuu wa cha hicho Dr. Slaa amesema baada ya zoezi hilo kuisha wataendelea na maandamano na kampeni yao maarufu kwa jina la Movement for Change (M4C). Wakati huhuo chama cha chadema kimesema kitagharamia mazishi ya kijana huyo aliefariki huku ikisubiri ripoti kutoka kwa Daktari na mwanasheria wao ili kujua hatua gani ya kuchukua
| Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa akiongea na waandishi kwenye hoteli ya Mount Uluguru |
Subscribe to:
Posts (Atom)


















