| Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu. | 
![]()  | 
| Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar. | 
Wema Sepetu akibubujikwa na machozi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi. 
 | 
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado 
yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa
 kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki 
asubuhi ya leo.
 Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori 
jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema 
wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya 
familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na 
mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti 
asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti 
yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.
