
Mwenyekiti
 wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),Juma Pinto 
akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii nje ya Ukumbi wa Mikutano 
wa Water Front,kunakofanyika Uchaguzi wa Rais na viongozi mbali mbali wa
 Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambapo hadi sasa hakuna Mwandishi 
yeyote alieruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi huo kwa madai kwamba Waandishi
 hawausiki na Uchaguzi huo,kwani waandishi jukumu lao ni kusubiria 
kupewa matokeo tu ya uchaguzi huo,kauli iliyotolea na Mwenyekiti wa 
Kamati ya Uchaguzi,Ndg. Hamidu Mbwezeleni.Jambo hilo liezua tafrani 
kidogo kwenye Eneo hilo hasa pale Watu wa Usalama (Polisi) walipowataka 
Waandishi kuondoka kwenye Eneo hilo la Uchaguzi.Mwenyekiti wa TASWA,Juma
 Pinto amewataka Waandishi wa Habari kuachana na Uchaguzi huo na 
kutoripoti chochote,kwani kilichoonyeshwa ni dharau kubwa kwa waandishi 
wa Habari na watanzania wote nchini wanaopenda Michezo