Kocha
 wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 
mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za 
Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini 
Afrika Kusini.
Taifa
 Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo 
(Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C 
Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka 
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kim
 amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi 
sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini
 Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe 
Englebert.
Wachezaji
 hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally 
Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, 
Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba,
 Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri 
Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
Mechi
 hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es 
Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano 
itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole 
nje kidogo ya Jiji la Kampala.
SOURSE: SHAFFIH DAUDA 
