Jacky Wolper a.k.a 
'Wolper Gambe' na ndinga yake mpya “Mini 
Cooper”. Jambo la
 kufurahisha kuhusu gari hili ni kwamba, kwa nyuma chini 
ya plate number mwanadada katupia maandishi ya steel kabisa kama 
yametoka kiwandani na gari lenyewe..yanasomeka “WOLPER GAMBE” ambalo ni 
jina analotumia kwenye mitandao mingi ya kijamii.
Upande wa pili nilipomuuliza Wolper ni pesa kiasi gani zimemtoka kuvuta ndinga 
hiyo akasema siri yake..nikatafute kwenye internet. Basi sawa.mtandao wa
 mini.co.za ambao ndio dealers wa Mini Cooper kusini mwa jangwa la 
Sahara wameonesha price ya R233,462 
kwa Mini Cooper yenye muonekano kama hii ya Wolper tukizingatia version ya 
gari husika..ambapo kwa pesa za Tanzania ni Tsh 42,012,236. 






