Rais wa Jamhuri ya Muungano 
wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikweteamemteua Mheshimiwa 
Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini. Kwa
 mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue  amesema 
uteuzi wa Mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili, 2013. Mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
