Pages
▼
Sunday, March 31, 2013
LADY JAY DEE: CLOUDS FM NI WANAFIKI WANATAKA WAHONGWE NDIPO WAPIGE NYIMBO ZA WASANII
Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.
"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. "Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!"
Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhuru. Nakunywa maziwa daily, I will survive".
"Hee! Kuna watu wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its me"
" Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya Prof J"
Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa.
SOURCE:JAMII FORUM

YANGA WAKAMATWA NA POLISI HUKO MKOANI MOROGORO
UHURU KENYATA AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMANI BAADA YA MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUWA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA HAKI
MAHAKAMA:
Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili 9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.
uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nne walichaguliwa kwa
haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi huu, akimaanisha Kenyatta na
mgombea mwenza na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.
Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa
kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta
binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani,
utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya
asilimia 43,28 za Odinga.

Saturday, March 30, 2013
MAKAMU WA RAIS DK. GHARIB BILAL ALIPOTEMBELEA ENEO LILIPODONDOKA GHOROFA JANA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dk. Gharib Bilal akiwa eneo la tukio ili kujionea mwenyewe pamoja na kupata maelezo kutoka kwa mashuhuda wa ajali ya kudondoka kwa Jengo la Ghorofa 16 jana asubuhi katikati ya Jiji.
Makamu wa Raisi Dk. Gharib Bilal akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa JWT kama anavyoonkana katika picha.
Askari wa JWTZ wakisaidiana na Wananchi kusukuma Jenereta kubwa kulisogeza eneo la tukio ili eneo hilo liwe na mwanga wakati wa usiku na kuwezesha uokoaji kuendelea hadi jana usiku.
Friday, March 29, 2013
DIAMOND NA WEMA WATAMBIANA KATIKA PESA
Wakati WEMA ISACK SEPETU akifungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, aliyekuwa Mpenzi wake Nasibu Abdul 'DIAMOND PLATNUM' amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliomgharimu takriban Shilingi za Kitanzania Milioni 260 hivyo kwa pamoja kuonesha jeuri ya pesa walizo nazo.
WEMA alifanya uzinduzi wa ofisi yake hiyo bila kumpa taarifa Mama yake mzazi MARIAM SEPETU ili iwe bonge la Surprise kwake pamoja na watu mbalimbali kama vile Diamond Platnumz mwenyewe siku ya Jumatano iliyopita, Jina la Ofisi hiyo ni ENDLESS FAME FILMS iliyopo Mwananyamala- Komakoma Jijini Dar es Salaam.
Wema akiwa Nyumbani kwake.
Wema akitoka kwake na gari yake aina ya Audi Q7.
Pamoja na Diamond kutoalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Ofisi hiyo ya Wema lakini chanzo cha habari kinasema alikuwa katika harakati za kumalizia Mjengo wake ulioko Tegeta ili nae afanye uzinduzi rasmi. Akizungumza na kitongoni blog akiwa
kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa ‘finishing’,
Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260 ni
zawadi kwa mama yake SANURA KASSIM ‘SANDRA’.
“Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo,” alisema Diamond.
Diamond alimzungusha paparazi
wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote
ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya
kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la
kuogelea ‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya
kufanyia mazoezi (gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu
kila kitu kitakuwa kimekamilika.
Hii ndiyo Nyumba ya Diamond anayojenga huko Tegeta na gari linalo onekana hapa ndilo gari lake anlotumia ukiachilia mbali Altezza aliyo mnunulia Mama yake.Ukiachana na ukubwa wa nyumba
hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine
ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo zitakuwa zikipangishwa.
Diamond akiwa Nyumbani kwake Sinza Mori anapoishi sasahivi.MHANDISI MKUU NA MHANDISI WA WILAYA YA ILALA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16
Bango linaloonesha Ujenzi wa Ghorofa lililoporomoka leo Jijini Dar es Salaam, Jengo ambalo Mhandisi Mkuu na Mhandisi wa Wilaya ya Ilala wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa Uchunguzi zaidi.
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akipatiwa Maelezo na Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Dar es Salaam Suleiman Kova wakati alipofika eneo la tukio ambapo Jengo la ghorofa 16 liliporomoka leo katika makutano ya Mitaa ya INDIRA GANDHI na ASIA.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia kwa pamoja MHANDISI MKUU WA JENGO na MHANDISI WA WILAYA YA ILALA kutokana na kuporomoka kwa Jengo la ghorofa 16 leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.
Kwani Mhandisi wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyetoa kibali cha kujengwa jengo hilo na Mhandisi Mkuu kuwa yeye ndiye msimamizi mkuu wa Ujenzi katika jengo hilo. Lakini pia MKUU WA MKOA wa Dar es Salaam amesitisha ujenzi wa jengo lingine lililopo pembezoni mwa Jengo lililoporomoka ambalo pia linasimamiwa na Mhandisi huyo huyo anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi.
Kwa Habari zaidi juu ya Tukio hilo endelea kufuatilia kwa karibu kitongoni blog
BREAKING NEWS: JENGO LA GHOROFA 16 LAPOROMOKA KATIKATI YA JIJI LEO HII
Taarifa iliyotufikia hivi punde inasema:
Jengo la ghorofa 16 limeporomoka asubuhi ya leo katikati ya Jiji la Dar es Salaam katika mtaa wa INDIRA GHAND karibu kabisa na Msikiti wa SHIA na Kuua watu watatu(3) na Kujeruhi kadhaa, ila inasemekana idadi ya watu wanao kadiriwa kuwa wamefunikwa na kifusi ni 60 lakini 17 kati yao tayari wameokolewa na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda KOVA amesema Uokoaji unaendelea japo vifaa muhimu vya kuokolea bado havipo lakini wataalamu mbali mbali kutoka Manispaa wapo pale kuhakikisha hali inafanikiwa na kuwaokoa watu zaidi walioko ndani.
Mtoto Maisamali Kareem (6) ambaye ameokolewa kutoka katika madrasa ya Msikiti wa Shia ulioangukiwa na Jengo hilo
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda Suleiman Kova na Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Marietha Minangi.
Kamanda Kova akizungumza na James Mbatia (Mbunge, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi)

Thursday, March 28, 2013
MBUNGE WA CHAMBANI SALIM HEMED KHAMIS AMEFARIKI DUNIA
Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,amefariki dunia muda mfupi
uliopita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za
kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.
INNA LI LAHI WA INNA ILAIHI RAJIUUN
INNA LI LAHI WA INNA ILAIHI RAJIUUN
HUYU NDIO BINTI WA MIAKA 16 ALIEFANYIWA UKATILI WA KUTISHA
Vituko
mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja
kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16
mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na
hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
Tukio lilikuwa hivi:
Zawadi
kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu
huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake
mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa
mshindo.
Baada
ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na
kuingia ndani na ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake
mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali
kutoka kwa mama yake mdogo.
Katika
kipigo hicho Zawadi alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa
mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake
Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia
hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.
MSANII HUYU KAMTELEKEZA MTOTO WAKE KAHAMA NA KUJA DSM KULA RAHA
Naitwa sakina mimi ni mtangazaji wa radio hapa kahama. kuna habari nyingi ninazozipata huku nimeona nianze na hii...
huyu jamaa ambae nimeambatanisha picha zake ni msanii ambae anajiona maarufu anaetokea hukuhuku kahama ila kwa sasa yuko dar. anafanya kzi yake ya sanaa kwenye kampuni ya tuesday film entaiteinment. jamaa huyu ambae amewahi kucheza filamu ya ''BEAUTIFUL'' kama mpenzi wake ray c aliyekuwa anaishi porini na ambae anajulikana sana kwa jina la 'TONY WA RAY C' anadaiwa kutelekeza mtoto wa kike wa miaka sita kwa maelezo yafuatayo...
ENDELEA KUISOMA HAPA

HUYU NDIYE MSANII ALIYEKIMBILIA DSM NA KAUCHA MTOTO |
juzi asubuhi alikuja dada mmoja hapa ofisini kwetu nikamkaribisha na
akaanza kunielezea kwamba ye anaitwa 'JUSTINA IKOMBE' alikuwa mchumba
wa msanii huyo ambae jina lake kamili ni 'JANUARY NYANDA' , na hata
wakafikia kuzaa nae mtoto mmoja wa kike anaejulikana kwa jina la
'TUNDA' lakini baada ya dada huyu kujifungua jamaa huyo aliaga
anakwenda dar. kufanya shughuri zake za sanaa na tangu hapo hana
mawasiliano nae wala hajui binti huyu anaishije na mtoto. na mbaya zaidi
ni kwamba mama wa mtoto anapojitahidi kumtafuta jamaa humkatia simu
akionyesha kutokuwa na shida kabisa ya kuongea nae na mpaka hivi sasa
mtoto amekua na anahitaji kwenda shule lakini hakuna msaada
wowote...binti huyo alikuwa akiongea kwa uchungu kiasi cha kunihuzunisha
hata mimi pia kama mwanamke mwenzake...nilimuomba namba za msanii huyo
ambazo ni 0756 570907 na nilipopiga na kujitamburisha jamaa alinijibu
matusi kama hana wazazi akidai kuwa hamfahamu huyo binti na wala yeye
hana mtoto anaeishi kahama na wala yeye mwenyewe hajawahi kuishi kahama,
na wakati amezaliwa kahama katika kijiji kinachoitwa 'kagongwa' na
amesoma shule ya msingi 'KISHIMA' na secondary 'ISAGEHE' na mpaka sasa
wazazi wake wote wanaishi hapa kijijini 'kagongwa'
MTOTO WA MSANII | |||||||||||||
ENDELEA KUISOMA HAPA
RAIS AZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VISAHIRIA VYA UKIMWI NA MALARIA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti
wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia
kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri
Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.
(PICHA NA IKULU)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu baada ya taarifa ya utafiti wa
viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia
kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda’, Kushoto kwake ni Mkurugenzi
wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi taarifa ya
utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27,
2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.
Kulia
kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William
Mgimwa.
MBUNGE WA CUF SALIM HEMED KHAMIS AANGUKA GHAFLA
Mbunge
wa chambani (CUF) Visiwani zanzibar Salim Hemed Hamisi ameanguka ghafla
akiwa katika kikao cha kamati ya mambo ya nje na ushirikiano wa
kimataifa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es salaam wakati kamati
hiyo ikiendelea na kikao chake
Mbunge
huyo ambaye siku za hivi karibuni ametoka nje ya nchi kwa matibabu ya
afya yake amefikwa na dhahama hiyo na kubebwa na baadhi ya wabunge kwa
kushirikiana na baadhi ya wandishi wa habari kutolewa nje ya chumba cha
mkutano na kupelekwa hospital ya taifa ya Mhimbili kwa uchunguzi na
matibabu zaidi.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Edward Lowasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
AZAM YAZIDI KUIKARIBIA YANGA YAITANDIKA PRISONS TATU BILA
Pichani juu, nahodha John Bocco, Khamis Mcha na Humphrey Mieno wakimpongeza Kipre Tchetche baada ya kufunga goli la tatu
Timu ya Azam FC imezidi kusonga mbele kwenye ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Tanzania Prisons 3-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Azam FC imepata ushindi huo wa nyumbani huku mshambuliaji wake Kipre Tchetche akijiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kufikisha magoli 12 tofauti na wafungaji wengine kwenye ligi kuu.
Katika mchezo huo Azam FC walipata goli la kwanza katika dakika ya 17 kupitia kwa Kipre Tchteche aliyecheza vizuri crosi iliyopigwa na Khamis Mcha, shuti la Kipre lilimbabatiza kipa wa Prisons David Burhan na kutinga wavuni, matokeo yakawa Azam FC 1-0 Prisons.
Goli hilo lilidumu hadi mapumziko huku Azam FC wakiwa wameutawala mchezo kwa kutengeneza nafasi nyingi dk 23 John Bocco alishindwa kumalizia krosi ya Tchetche na mpira ukatoka nje, dk 34 Tchetche alipiga shuti likatoka nje na kupeleka timu zote mapumziko Azam FC ikiwa mbele kwa 1-0 dhidi ya Prisons.
Kipindi cha pili timu zilirejea uwanjani kwa kasi kila moja ikisaka bao la kumalizia mchezo, Kipre tena alipiga shuti likadakwa na kipa David wa Prisons, Humphrey Mieno naye alipiga shuti likaenda nje, huku Prisons dk 58 Elias Maguli alijaribu kufunga lakini shuti lake likatoka nje.
Wakipata nafasi nyingi na kukosa magoli ya wazi, dk 75 mshambuliaji mahiri wa Azam FC, John Bocco aliandika bao la pili kwa timu yake baada ya kuachia shuti la mbali lililongonga mwamba wa chini na kutinga wavuni, Bocco alibadili matokeo na kuwa Azam FC 2-0 Prisons.
Tchetche alizidi kulisakama lango la Prisons na dakika ya 84 alihitimisha kalamu ya magoli kwa kuandika bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Seif Abdalah ‘Karihe’, na kuipa Azam FC ushindi wa 3-0 dhidi ya TZ Prisons.
Katika mchezo huo Azam FC walifanya mabadiliko dk 65 alitoka Khamis Mcha akaingia Seif Abdalah ‘Karihe’, dk 70 akaingia Abdi Kassim ‘Babi’ kuchukua nafasi ya Humphrey Mieno na dk 73 Salum Abubakar ‘Sure Boy’ alipumzika nafasi yake ikachukuliwa na Ibrahim Mwaipopo, mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kucheza kandanda safi muda wote wa mchezo.
Prisons waliwatoa Nurdin Iss na Aziz Sibo nafasi zao zikachukuliwa na Peter Kazengele na Henry Mwalugala, mabadiliko yaliimarisha safu ya ushambuliaji lakini hayakuweza kubadilisha matokeo ya mchezo huo na kuicha Azam FC kupata ushindi huo mnono wa 3-0.
Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amefurahishwa na matokeo hayo na kiwango cha timu yake, amesema kilichopo sasa ni kuhakikisha hawapotezi hata mechi moja katika michezo iliyobaki ya ligi kuu.
Azam FC kesho itaingia kambini kwa maandalizi ya kucheza dhidi ya Ruvu Shooting, mechi itakayopigwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Azam FC, Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, Michael Bolou, Tchetche Kipre, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ibrahim Mwaipopo 73’, John Bocco, Khamis Mcha/Seif Abdalah ‘Karihe’ 65’ na Humphrey Mieno/Abdi Kassim ‘Babi’ 70’.
SOURCE:AZAMFC.CO.TZ
HUMUD KUELEKEA JOMO COSMOS WIKI HII
Kiungo mwenye mapafu ya mbwa Abdulhalim Humud Gaucho huenda akasafiri kuelekea bondeni Afrika ya Kusini wikiendi hii kufuatia kupata nafasi ya majaribio kwenye timu ya Jomo Cosmos aliyowahi kuchezea watanzania mengine Nteze John na Ally Shah siku za nyuma.
Cosmos inayomilikiwa na kocha wa zamani wa Bafana Bafana Jomo Sono imempa nafasi hiyo humudi baada ya kufanyiwa mipango na uongozi wa Azam FCkatika kutekeleza sera yake ya kutengeneza uwanja mkubwa kwa wachezaji wa kitanzania kwenye ligi mbalimbali zinazoendeshwa kisasa.
Cosmos ambao wapo kwenye kampeni ya kurejea PSL watahitaji huduma ya Humud msimu ujao ambao Jomo Sono ameahidi kuwa watakuwa wakicheza PSL
SOURCE:AZAMFC.CO.TZ
SOURCE:AZAMFC.CO.TZ
Wednesday, March 27, 2013
MAHAKAMA YAAMURU MATOKEO YA URAIS KENYA YAHESABIWE UPYA KATIKA VITUO 22 KATI YA 33
Nairobi.
Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchini Kenya imeagiza kuchunguzwa
kwa fomu 34 za matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka katika vituo vyote
34,400, vilivyotumika kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo
uliofanyika Machi 4, mwaka huu.
Kadhalika
mahakama hiyo jana iliagiza kuhesabiwa upya kwa kura za urais katika
vituo vya kupigia kura 22 kati ya elfu 33 vilivyolalamikiwa na aliyekuwa
mgombea urais wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.
Katika
malalamiko yake yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo kupinga Uhuru
Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika
Machi 4, Odinga alidai kuwa vituo hivyo 22 kura zilizopigwa zinazidi
idadi ya wapigakura walioandikishwa.
Akisoma
uamuzi huo kwa niaba ya majaji wenzake watano, Jaji Smokin Wanjala
alisema kwamba uhesabuji kura wa vituo hivyo utafanyika leo kuanzia saa
2.00 asubuhi kwa lengo la kubaini ukweli kuhusu madai hayo.
“Matokeo
ya kura zitakazohesabiwa katika vituo hivyo 22 yawasilishwe katika
mahakama hii Jumatano, saa 10.00 jioni,” alisema Jaji Wanjala.
Kikao hicho, ambacho Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amealikwa kama mwangalizi, ni cha awali kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa rasmi keshokutwa (Alhamisi) na kuendelea kwa mfululizo hadi kufikia uamuzi ikiwa madhumuni yake.
Lengo ni kupitia madai yaliyowasilishwa mahakamani hapo na pande zote zinazohusika na kuamua mwenendo wa kesi utakavyofanyika.
Ukiachilia
mbali kesi iliyofunguliwa na Odinga kupinga Kenyatta kutangazwa mshindi
wa uchaguzi huo wa tano tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa
Kenya, kuna kesi nyingine ambayo imefunguliwa na muungano wa mashirika
yasio ya kiserikali, `The African Centre for Open Governance’ (Africog).
Katika
kesi hiyo inayorushwa moja kwa moja na vituo kadhaa vya televisheni
nchini Kenya, Africog inahoji uhalali wa uchaguzi huo.
“Kesi yetu haihusiani na nani ameshinda au kushindwa bali jinsi umma ulivyoshindwa, tumepoteza ahadi ya uchaguzi uliowazi,” alisema Gladwell Otieno, Mkurugenzi Mtendaji wa Africog.
Kesi
ya tatu ambayo imefunguliwa na wajumbe wa timu ya kampeni ya Kenyatta,
mwanaharakati katika mitandao ya kijamii Dennis Itumbi na Moses Kuria
wanaopinga uamuzi wa Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya
kujumuisha kura zilizoharibika wakati wa kujumlisha kura za wagombea
urais.
Katika
uamuzi wake, mahakama iliamua kwamba kesi zote tatu zitaunganishwa kuwa
moja, huku ile iliyowasilishwa na Odinga ikiwa ndiyo kinara wa kesi
zote.
Pia
mahakama iliamuru Muungano wa Vyama vya Siasa wa Cord na Jubilee kuteua
mawakala 10 kila mmoja ambao watakula kiapo mahakamani hapo kabla ya
kuanza kuhesabu upya kura hizo.
Katika
uamuzi wake jana jioni, mahakama hiyo ilikubali ombi la Mwanasheria
Mkuu wa Kenya, kushiriki katika kesi hiyo kama rafiki wa mahakama na
siyo mdaiwa kama ilivyokuwa awali. Wakili wa Cord, George Oraro
alikubali uamuzi huo licha ya kuupinga awali.
ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA NA KUMUUA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Jackson Simbo anayedaiwa kumgonga kwa gari
marehemu trafiki Elikiza Nko wiki iliyopita katika taa za kuongozea magari za Bamaga-Mwenge
jijini Dar ss Salaam amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni.
Mshitakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena Aprili 15 mwaka huu.
Mshitakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena Aprili 15 mwaka huu.
MWANAFUNZI WA KITIVO CHA SHERIA UDSM AJINYONGA
Picha hii kwa hisani ya Maktaba:
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo cha Sheria,
Joseph Bernadina (25), amejinyonga kwa kutumia kamba na kukutwa
ameifunga juu ya mti, katika eneo la Yombo chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.
Aliongeza kuwa Jumamosi iliyopita alipokea simu kutoka kituo cha polisi cha chuo hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi alitishia kujiua, lakini aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka kitengo maalum cha washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa Jumapili.
“Nilikuja tena kushituka leo asubuhi napokea simu kutoka kwa mshauri wa wanafunzi kuwa kuna wanausalama wamemkuta mwanafunzi akiwa amejinyonga juu ya mti huku akiwa na karatasi kwenye mfuko wa sharti ikimtambulisha pamoja na ujumbe uliosema, kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote kwani amejiua kwa ridhaa yake --asisumbuliwe mtu yeyote kwani nimefanya hivi kwa maamuzi yangu mwenyewe pia nizikwe kwetu--” alisema.
Profesa Mgaya alisema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na Uongozi wa chuo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu na kwamba Chuo kitagharamia kuusafirisha mwili kama alivyoomba katika ujumbe aliouacha wa kupelekwa wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa.
Naye rafiki wa marehemu, Daniel Mwamlima, alisema marehemu hakuwahi kuzungumza chochote kilichoashiria kuwa ana matatizo wala mgogoro na mtu yeyote. Alisema walimuacha hospitalini Jumamosi na kesho yake kumchukua, lakini baadaye aliwatoroka.
“Sasa leo (jana) asubuhi tulipata taarifa za mwanafunzi kujinyonga mbaya zaidi tukakuta ni yeye,” alisema Mwamlima.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Yasini Athumani, alisema wamezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio na alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba marehemu aliwahi kuwa na historia ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu ya ugonjwa wa msongo wa mawazo.

Source: WAVUTI
Tuesday, March 26, 2013
ZITO KABWE, IDD AZAN NAO WAMALIZA MAFUNZO YAO JKT MGAMBO 835KJ - TANGA
Mbunge wa
Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo
wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo
835KJ kilichopo Mkoani Tanga.
Pichani
juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha
chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake Iddi Azan, Abdallah
haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.
Aidha
Zitto Kabwe amesema anafuraha isiyo na kifani kumaliza mafunzo hayo na
ameweka historia kubwa katika maisha yake leo hii. Anapasha zaidi
katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3
akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama.