Mbunge wa
 Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo
 wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 
835KJ kilichopo Mkoani Tanga.
Pichani 
juu ni Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha 
chini akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah 
haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.

Aidha 
Zitto Kabwe amesema anafuraha isiyo na kifani kumaliza mafunzo hayo na 
ameweka historia kubwa katika maisha yake leo hii. Anapasha zaidi 
katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 
akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama.  
