Lady Jay Dee
  East  African popular musician  Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo 
Clouds fm  kupitia Twitter kutokana na  wimbo wake mpya uliotoka 
hivi karibuni  Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo.  Jay dee 
ameandika kuwa radio  ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila  
wasanii wao tu. Angalia  tweet za Queen of Bongofleva huyo.
"Radio ya watu  isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu.
"Anaedai kuianzisha  bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na  Bongo flava! Damn !!"
Jay  Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini  kuonyesha kuwa yupo kwa
  lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena  "Kill me if u 
 can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba  sumu,
  lakini hainidhuru. Nakunywa maziwa daily, I will survive".
 "Hee!   Kuna watu wanadhani nili tweet nikiwa nimelewa, nilimaanisha
 na  msimamo ni  huo. Sitasema oooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo its 
me"
"  Kuna DJ flani  alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika 
sehemu  nilioimba mimi anakata  verse yangu nimtaje?? Sa hivi anakat ya 
Prof J"
 Hata hivyo si Jay Dee  pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao  kutokupigwa.
SOURCE:JAMII FORUM 
