![]()  | 
| Amis Joselyn Tambwe akishangilia goli lake pamoja na Simon Happygod Msuva | 
YANGA
 Leo ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam imeichapa Klabu ya 
Botswana BDF XI Bao 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya 
Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
 
Bao zote za Yanga zilifungwa na Straika wao Amisi Tambwe anaetoka Burundi moja katika kila Kipindi.
| Tambwe akishangilia goli lake na Mrisho Ngassa na Msuva ambao ndio wapishi wa magoli yake. | 
Tambwe
 alifunga Bao la Kwanza Dakika ya Kwanza tu ya Mchezo alipounganisha kwa
 Kichwa Krosi ya Simon Msuva na kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 55 
pia kwa Kichwa baada ya Krosi safi ya Mrisho Ngassa.
![]()  | 
| Mrisho Ngassa akichanja mbuga | 
Timu 
hizi zitarudiana huko Botswana Wiki mbili baadae na Mshindi wake 
atatinga Raundi ya Kwanza kucheza na Mshindi kati ya Sofapaka ya Kenya 
na FC Platinum ya Zimbabwe.
Hapo 
Kesho Jumapili, Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watakuwa kwao Azam 
Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kuivaa El 
Merreikh ya Sudan katika Mechi ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Timu 
nyingine mbili za Tanzania ambazo pia zimo michuano ya CAF Barani Afrika
 ni KMKM na Polisi, zote za toka Zanzibar, Wikiendi hii zinaanzia 
Ugenini kwa KMKM kucheza Sudan na Al Hilal kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI  na
 Polisi kucheza Nchini Gabon na CF Mounana kwenye Kombe la Shirikisho
![]()  | 
| Mchezaji wa BDF akimfanyia rafu Haruna Niyonzima | 



