KIKOSI CHA TIMU YA SIMBA.
 WACHEZAJI WA SIMBA WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO PATRICK PHIRI.
 KIKOSI CHA TIMU YA YANGA.
WACHEZAJI WA YANGA WAKISHANGILIA MOJA YA BAO LAO.
kitongoni blog:
Mpaka  kwenye  miaka 
ya  90  kulekea  mpambano  wa 
watani  wa  jadi 
kulikuwa  na  imani 
za  kishirikiana za mvua  zikichukua 
nafasi  kuliko  hivi 
sasa, itakumbumbukwa  kwamba  ilifikia 
hatua  timu  ya 
Yanga  wanapoona  mvua 
imenyesha  wao  walikuwa 
wakiingiwa  na  hofu 
zaidi  ya  kuupoteza mchezo  huo 
huku  upande  wa 
pili  wa  Simba nao 
wakichekelea  kunyesha  kwa 
mvua   wakimaanisha  kuwa 
lazima  wataibuka  washindi.
Ama 
kwa  hakika  tukio hilo 
lilikuwa  lina  nafasi 
kubwa  kwa  kuwa 
kweli  siku  ya 
mpambano  huo  kama 
mvua  haikunyesha  Simba 
walifungwa  au  kutoka 
sare  na  pale 
iliponyesha  mvua  tu  ni  lazima 
Yanga  wangefungwa.
Lakini 
kunako  miaka  hii  ya
 2000 
mambo   sasa  yamebadilika 
na  yeyeto  Yule 
anaweza  kupata  ushindi 
katika  hali  yoyote  ile liwake 
jua  ainyeshe  mvua, 
na  hili  ndiyo 
miongoni  mwa  mambo 
yanayozidi  kuupa  ladha 
mchezo  huu  kuwa 
vigumu  kupata  utabiri 
wa  nani  mshindi. 
Jambo lingine  ni 
zile  kambi  zao 
ambazo  kama  Yanga 
wakitokea  Pemba  au 
Bagamoyo   Mbegani  huwa 
wana  uhakika  zaidi 
wa  kupata    ushindi 
kuliko   kuweka  kambi 
yao  Jijini  Dar 
es  salaam,  wakati 
Simba  wao  huwa 
wana  uhakika  zaidi 
wa  kupata  ushindi 
kama  tu  wametokea 
Unguja  au  Dar 
es  salaam  maeneo 
ya  Bamba  Beach. 
Katika 
mechi  hii  kambi 
za  timu  zote 
hizo  hazikuwa  kwenye 
sehemu  zile  zilizo zoeleka 
na hali  hiyo  imefanya 
kuwa  na  tambo 
nyingi  kutoka  kwa 
mashabiki  wake  na kila 
upande  kuamini  kuwa 
wataibuka  washindi.
Jicho  la 
kitongoni blog litakuwepo  kukujuza 
kila  kitu  ambacho 
kitatokea  ikiwa  ni 
pamoja  na  visa na 
vibweka  vyote  vitakavyojiri 
uwanja  wa  Taifa 
tarehe  18/10/2014, Jumamosi. 

