Raia wa Msumbiji walipiga kura kumchagua rais
mpya na vile vile wabunge. Chama cha Frelimo, ambacho kimeiongoza nchi
hiyo tangu ilipojinyakulia uhuru mwaka 1975, kimeshindana na chama cha
upinzani, Renamo.
Kulingana na matokeo
chama tawala kimeshinda uchaguzi huo ingawa upinzani Renamo unasema
haukubali matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika Jumatano. Ulikuwa
uchaguzi wa Rais na wabunge.
Msemaji wa Renamo anasema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na visa vya udagngayifu huku wapiga kura wakitishwa.
AFONSO DHLAKAMA
Kiongozi
wa Renamo, Afonso Dhlakama, alijitokeza kutoka mafichoni mwezi
uliopita, na kuamua kuwania urais, baada ya mapatano ya amani kati ya
chama chake na serikali.
FILIPE NYUSI
Mgombea wa chama kilicho madarakani ni Filipe Nyusi, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa ulinzi.