DEGE ECO - VILLAGE YAANZA UJENZI WA NYUMBA ZA NSSF KIGAMBONI
Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya
Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki maonyesho ya nyumba
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam umeanza hivi karibuni.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na
Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi
unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zitakuwa tayari
ifikapo Januari 2015. Mradi
huo unajengwa kwenye eneo la eka 300 na kampuni hiyo imewekeza
zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na
apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment
zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.