Pages

Thursday, June 12, 2014

TAHADHARI YA PICHA: ASKARI AUAWA KINYAMA KWA KUKATWA NA MAPANGA KIMANZICHANA




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi (SACP) Ulrich Mtei


Marehemu Joseph Ngonyani:
 huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzichana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.

Jambo la kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye
silaha ambaye amefahamika kwa jina la Joseph Ngonyani na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30.

Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. 

Askari Ngonyani alifariki alipokuwa anapatiwa matibabu
kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye Venance amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.

Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye Veronica Musime, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.