Mwanadada Wema Sepetu ametia maguu kwenye ofisi za Mult Choice Tanzania na kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki shindano la Big Brother Africa katika mchakato huu wa awali
Pages
▼
Friday, February 1, 2013
PAKITI YA VODKA YAKUTWA NDANI YA TONIC WATER YA COCA COLA
BAADHI
 ya wananchi ambao ni watumiaji wa vinywaji baridi Jijini Mbeya 
wameyalalamikia baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji wa 
bidhaa hizo kwa kutozingatia usalama wa watumiaji.
Malalamiko hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni mwananchi mmoja aliyoomba kuhifadhiwa jina lake kununua soda aina ya Tonic Water inayotengenezwa na kampuni ya Coke kukutwa ikiwa na karatasi la pombe kali aina ya Vodka.
Soda hiyo ikiwa mpya bila kufunguliwa ilikutwa katika duka moja eneo la Simike baada ya mteja huyo kuuiwa kwa lengo la kiutuimia lakini kabla ya kuifungua ndipo laipogundua uchafu huo.
Kufuatia hali hiyo, Mwandishi wa habari hii alipewa taarifa na mhusika ambapo walienda moja kwa moja hadi kiwandani Coke eneo la Iyunga Jijini Mbeya na kupokelea na Meneja mauzo wa wilaya (Area Sales Manager). Baada ya kupokelewa na kuelezwa hali iliyotokea, Meneja huyo aliwapeleka waandishi kwa kitengo cha ubora wa bidhaa ambao bila woga walisema tuwaachie soda hiyo baada ya kuridhishwa kuwa ni mpya na inatoka kiwandani hapo.
Walidai waachiwe soda hiyo ili kuifanyia uchunguzi wa kimaabara katika uchunguzi utakafanyika kwa wiki moja hali iliyoleta wasiwasi kwa walalamikaji huku wakihoji, “uchunguzi gani ufanyike ili hali uchafu unaonekana?”
Aidha, walidai kuwa pamoja na kukataliwa kubakishwa kwa soda hiyo, walisema mlalamikaji hatanufaika na chochote ikiwa na kiwanda kutoathirika na tatizo hilo licha ya kuhusika na kuzalisha bidhaa yenye uchafu.
Hali kama hizo zimekuwa zikiwaathiri watumiaji wa vinywaji hivyo hasa wanaotumia nyakati za usiku muda ambao si rahisi kwa mteja kugundua hali ya uchafu katika vinywaji.
Hata hivyo, mhusika aliyepatwa na janga la soda hiyo kutoka kiwanda cha Coke aliiomba mamlaka zinazohusika kufuatilia hali ya usafi wa vifaa vya kubebea vinywaji hivyo kabla ya kupelekwa sokoni kwa watumiaji ili kunusuru afya za wananchi.

DR MIGIRO AFUNGUA MSHINDANO YA MPIRA WA PETE MKOANI KIGOMA
HUU NI MUONEKANO WA MJI WA KIGOMA NA ZIWA TANGANYIKA.
 Huu ndiyo muonekano wa Mji wa Kigoma sambamba na Ziwa Tanganyika, na Ghorofa linaloonekana ni la Shirika la Nyumba ambalo linataraji kuzinduliwa rasmi hivi karibuni na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Picha zifuatazo zinaonesha baadhi ya Taswira za Wilaya mpya ya BUHIGWE, Mkoani Kigoma kama zinavyoonekana hapa chini.
PUNGUZO LA GHARAMA ZA KUPIGA SIMU KUANZA KUTUMIKA MWEZI MACHI 2013.

Mamlaka
 ya mawasiliano Tanzania TCRA imeyataka makampuni ya simu za mkononi 
Tanzania kuhakikisha yanaanza rasmi mpango wa punguzo la bei ya kupiga 
simu katika mitandao mingine kutoka bei inayotumika sasa hivi ya 
shilingi 113 kwa dakika mpaka shilingi 34 na senti 92 ikiwa ni bei mpya 
inayotakiwa kuanza kutumika kuanzia siku ya kwanza ya mwezi March 2013.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa TCRA Profesa John Nkoma amesema uamuzi wa kufanya hivyo ni 
kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ambapo makampuni hayo 
yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo na hatua za kisheria 
zitachukuliwa kwa kampuni yeyote ambayo itafanya kinyume na hayo 
maagizo.
Namkariri
 akisema “bei itaendelea kushuka kadri miaka inavyokwenda, tarehe 1 
january 2014 bei itatakiwa kuwa sh 32 na senti 40, tarehe 1 january 2015 sh
 30 na senti 58, tarehe 1 january 2016 itatakiwa kuwa sh 28 na senti 57,
 hizi bei ni za juu kabisa na Kampuni za simu ni ruksa kwao kuzungumza 
na wakatumia bei ya chini kabisa”
TUNDA LA STAFELI LAGUNDULIKA KUTIBU SARATANI

 Tunda aina la Stafeli.
TUNDA
 la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa 
karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo 
vya afya, utafiti umebaini.Utafiti 
huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani, 
umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya 
matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu 
ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani 
pasipo kusababisha madhara katika mwili kama zinavyofanya dawa nyingine 
za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa 
kwa mara ya kwanza katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini Marekani, 
mwaka 2010.
Taasisi ya  utafiti  wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya  utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976. Katika 
utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina 
uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa 
kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani.
Inaelezwa
 kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia  jina la kibiashara
 la ‘Triamazon’  na kimepigwa marufuku kutumika nchini Uingereza na 
Marekani  kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba.Utafiti 
mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na 
kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia  ulibaini kuwa stafeli lina 
uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti 
wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga 
seli za saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo 
tiba ya mionzi ifanyavyo.
Tunda la 
Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho 
ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya saratani. Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na
 kutibu saratani, kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia 
huweza kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya 
mfumo wa fahamu na sukari.Utafiti  
huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo kinaweza  
kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa na 
madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito na 
kunyonyoka nywele.