
Mamlaka
 ya mawasiliano Tanzania TCRA imeyataka makampuni ya simu za mkononi 
Tanzania kuhakikisha yanaanza rasmi mpango wa punguzo la bei ya kupiga 
simu katika mitandao mingine kutoka bei inayotumika sasa hivi ya 
shilingi 113 kwa dakika mpaka shilingi 34 na senti 92 ikiwa ni bei mpya 
inayotakiwa kuanza kutumika kuanzia siku ya kwanza ya mwezi March 2013.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa TCRA Profesa John Nkoma amesema uamuzi wa kufanya hivyo ni 
kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ambapo makampuni hayo 
yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo na hatua za kisheria 
zitachukuliwa kwa kampuni yeyote ambayo itafanya kinyume na hayo 
maagizo.
Namkariri
 akisema “bei itaendelea kushuka kadri miaka inavyokwenda, tarehe 1 
january 2014 bei itatakiwa kuwa sh 32 na senti 40, tarehe 1 january 2015 sh
 30 na senti 58, tarehe 1 january 2016 itatakiwa kuwa sh 28 na senti 57,
 hizi bei ni za juu kabisa na Kampuni za simu ni ruksa kwao kuzungumza 
na wakatumia bei ya chini kabisa”