Mwanadada Elizabeth Michael 'Lulu' ametembelea
 hospitali ya Ocean Road Iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa
 zawadi za fedha kwa wagonjwa wa saratani hospitalini hapo.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Lulu ameandika "Naamini Mimi sio mwema sana mpaka Mungu akaniwezesha kuona mwezi 
huu nikiwa mzima na mwenye afya...! kwa kutambua Hilo nimeanza mwezi huu 
kwa kupita ktk hospital ya Ocean Road na kutoa mchango ili kuwasaidia 
wagonjwa wa Saratani.
Tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa 
chochote tulichonacho! Nawatakia mwezi wenye Baraka na mafanikio!...
Kumbuka kutoa ni moyo na sio utajiri mtu yeyote anaweza kutoa kwa kadri alivyo jaaliwa na M/Mungu lakini halazimishwi na mtu ni wewe mwenyewe ukijiona unaweza unatoa na sio Ocean Road peke yake, kwani wahitaji wapo wengi sehemu nyingi iwe hospitali, vituo vya yatima na kwingineko.