| Klabu
 ya Simba imekamilisha rasmi usajili wa beki wa kati Gilbert Kaze kutoka
 Vital O ya Burundi. Gilbert aka Demunga ni mmoja wa mabeki bora 
walionyesha kiwango kizuri hasa kwenye michuano ya Cecafa iliyopita. 
Amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba. Gilbert Kaze pia 
ni nahodha wa timu ya taifa ya Burundi - na alikuwa mmoja wa wachezaji 
muhimu wa timu hiyo walioiwezesha Burundi kufuzu kucheza CHAN mwakani 
nchini South Africa. |