Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini
 Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani 
Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya 
leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 
The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa 
nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake 
Mangwea. “Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P 
nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili 
Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi 
changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea 
asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, 
asanteni,” alisema. Msikilize hapa