Pages

Saturday, June 1, 2013

FALCAO ATUA RASMI MONACO


KLABU ya Monaco usiku wa jana imethibitisha kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kutoka klabu ya Atletico Madrid.
Mabingwa hao wa Ligi Daraja la Kwanza Ufaransa, wamepania kuipindua Paris St Germain katika matawi ya juu ya Ligi Kuu Ufaransa.
New surroundings: Atletico Madrid's Radamel Falcao has joined Monaco
Monaco imesema katika tuvuti yake kwamba: "Monaco imefikia makubaiano na  Atletico Madrid na mchezani mwenyewe (Radamel Falcao) kwa uhamisho wa msimu  wa 2013-14.