MAPAMBANO
 kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara umefika
 katika hatua mbaya,kiasi cha mtu mmoja kudaiwa  kujeruhiwa vibaya baada
 ya kurushiwa bomu wakati wa mashambulizi hayo katika eneo la Magomeni. 
Mbali na kujeruhiwa kwa mtu huyo aliyekuwa katika maandamano ya kupinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia imechomwa moto.
Taarifa zilizonaswa na Fahari ya Kusini hivi punde zinadai kwamba wananchi wa Mkoa wa Mtwara wamefungiwa majumbani tangu asubuhi, huku Jeshi la Polisi likifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwanasa watuhumiwa wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo kwa njia ya vipeperushi.

Shuhuda wa wa tukio hilo ameitaarifu Fahari ya kusini 
 kwamba waandamanaji hao wameapa kufa endepo serikali itaendelea na 
mipango yake ya kusafirisha gesi hiyo hadi Jijini Dar es Salaam. "Hali 
hapa ni mbaya, tangu asubuhi wananchi wote wamefungiwa ndani ya majumba 
yao, hakuna anayeruhusiwa kutoka nje, Polisi wanapiga mabomu ya machozi 
kila mtaa huku wakiwasaka watuhumiwa waliosambaza vipeperushi na 
kuwatawanya wandamanaji waliozagaa katika mitaa  mbalimbali, mpaka hivi 
sasa kuna mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya
 raia na Asakari Polisi wanaotumia mabomu ya machozi na silaha zigine za
 moto"alisema shuhuda wa tukio hilo. 
Hata
 hivyo imedaiwa kuwa hali hiyo imesababisha barabara zote kufungwa kiasi
 cha kuzuia mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, 
kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU 
yametanda kila kona za mji, huku taarifa zidi ikifafanua kwamba hakuna 
mawasiliano, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio 
ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi
 ya nyumba maeneno ya Shangani zimechoma moto.