Spika
 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Anna Makinda 
ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati ya uongozi ya 
Bunge iendelee  kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu vurugu za 
Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na 
uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za viongozi wa
 serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC.
