Jana msanii Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz alitua mjini Bukoba, 
Kagera kuendelea na ziara yake ya kutumbuiza mikoa ya kaskazini 
magharibi. Kama
 inavyoonekana kwenye picha, umati mkubwa wa watu ulijitokeza kumlaki 
Diamond, kitu ambacho kilimpelekea msanii huyo kuchomoza juu ya gari 
kuwasalimia.
Kwa mujibu wa Diamond’s official website, kitendo cha
 Diamond kujichomoza juu ya gari kilisababisha msongamano mkubwa zaidi, 
na kusababisha barabara kufungwa, na baadhi ya kazi kusimama kwa muda.
“Juzi….Tarehe
 30 march niliwasili salama salimini mjini bukoba Mkoani Kagera….Pili 
niwashukuru Mashabiki zangu wote Mkoani Humu kwa kunipokea kwa hali na 
mali ,Hii inaonyesha jinsi gani watanzania wanathamini na wana mapenzi 
na wasanii wao…..!!” aandika Diamond.
Aliongeza “Nililazimika 
kutoka Juu ya Gari kuwasalimu kabla sijaelekea hotelini…. Nilivotokeza 
hali ilizidi kuwa mbaya zaidi….Polisi walilazimika kufunga barabara 
kadhaa mjini bukoba na hata kazi zingine kusimama kwa muda kutokana na 
watu kuzingira Gari nilokuwepo kila kona nilipokuwa napita”. 
SOURCE:Diamond 

