
Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji 
Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa 
sana kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama 
watoto wake mtarajiwa.
Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari 
la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.
Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu 
anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari 
gani 
anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja kwa hiyo sasa hivi 
anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”
Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond 
amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza 
ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema 
chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “