
William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319.
William Zelothe Stepehen akiwa na marubani wa ndege ya Fastjet.
William
 Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmaasai aliyepewa ithibati ya 
kuiongoza ndege aina ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya
 urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo
 hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi 
nchini Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha 
ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.
William
 anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati 
akiwa katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya 
Airbus A319 kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya 
usalama. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda 
kweli kweli, kama unaifahamu vyema”
William
 amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani 
kwa mara ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka 
2006 ambapo alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege. Ingawa ana 
umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.
Kumwajiri
 rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za 
fastjet za kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa 
waliobobea katika fani hiyo hapa nchini. Mikakati yao ya kuajiri pia ni 
mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kila 
rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa 
shilingi 49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za 
kimarekani.
fastjet
 ni shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki
 wa FLY540 na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri 
wa ndege ambalo linazingatia bajeti. Fastjet, ambayo inaungwa mkono na 
mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana Stelios Haji Ioannou, 
imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi kiasi cha Tsh32,000 bila 
kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni  ya watu ambao walikuwa 
wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria ndege kwa mara ya 
kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara. Tangu kuzinduliwa kwake
 mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet limewasafirisha zaidi ya 
watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege zikisafiri katika muda 
uliopangwa.

