Tizi kali likiendelea wakati Simba wakijiandaa kwa mechi  dhidi 
ya mabingwa wa Angola, C.R.Libolo kwenye mchezo wa awali na endapo 
watafuzu basi watakutana na El Merrikh ya Sudan  kwenye hatua ya 16 bora
 hapo mwezi Machi 15, 16, 17.
| Tizi likindelea | 
| Kocha msaidizi Jamhuri Kihwelu Julio akisimamia tizi | 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi 
akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya 
kukutana jana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Short alisema ushawishi wa Malkia wa Nyuki umechangia yeye kutoa mwaliko huo na anaamini timu zote zitafaidika.
"Mazungumzo yetu na Rahma yalikuwa mazuri sana, nimefarijika na ninaamini mwaliko niliotoa utakuwa mwanzo wa uhusiano mzuri kwa kuwa mwanamama huyu amenishawishi," alisema.
Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu.
Awali Simba, ilijulikana kwa jina la Sunderland.