Kevin McGill 
Mwendesha
 lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la 
Georgia nchini Kevin McGill Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni 
kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na 
kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.
Kervin McGill 
yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba 
anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua 
usumbufu kwa 
wengine na 
majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini 
wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye
 na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.
Kesi
 hiyo imewashtua watu wengi na kuwa gumzo kwenye vyombo vya 
habari huku wengi wao wakiwa wamepigwa na butwaa kwa mtu kwenda jela 
kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. 
Mtu kama huyu alistahili kupata 
onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa 
anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.

Rais 
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa 
Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje 
ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi
 wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es 
salaam.

Rais 
Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati 
alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo 
iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.

Rais 
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, 
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na 
baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa 
studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam.



