Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa Francis Cheka amehukumiwa 
kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1
 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko 
Morogoro.
 Meneja huyo ajulikanaye kwa jina la Bahati inaelezwa 
alienda kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati 
akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo ndipo Bondia huyo alikataa
 kumlipa na kumshushia kipigo.
 Francis Cheka akiwa amevaa mkanda wa ubingwa katika moja ya mapambano yake aliyo wahi kucheza na kushinda.
 Francis Cheka hapa akiwa anafanya mazoezi kabla ya mpambano.

