Kushoto ni Ney wamitego, Diamond Platnum, na Dancer wa Diamond wakiwa katika jukwaa la Fiesta hivi karibuni wakiwa wamevalia mavazi ya Jeshi.
MSANII wa
 muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond', amekiri kuhojiwa na 
polisi baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa mavazi yanayoaminika kuwa ni 
sare ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hata hivyo
msanii huyo alidai kwamba mavazi hayo hayakuwa sare za jeshi hilo na 
kwamba yeye aliyanunua alipokuwa Ujerumani ingawa baada ya kuhojiwa 
aliyasalimisha.
Diamond 
alipanda jukwaani Jumamosi iliyopita katika onyesho la Fiesta jijini Dar
 es Salaam akiwa na mavazi hayo jambo ambalo liliibua mjadala kwa watu walio wengi.
Diamond alikiri kupata ujumbe uliomtaka kufika Kituo cha
 Oysterbay, Dar es Salaam na madansa wake akiwa na nguo hizo,
        
 "Awali 
Meneja wangu alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile 
nguo nikiwa na madansa wangu ambao pia walizivaa, nilifanya hivyo na 
kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika," alisema.
"Nisingeweza
 kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa 
kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana tu na ya jeshi na hayakuwa 
sare rasmi za jeshi, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo," alisema.