Huduma ya
 M-PAWA inayotolewa na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) imetoa mikopo 
ya shilingi milioni 200 katika kipindi cha miezi mitatu tangu ianzishwe.
Pamoja na
 fedha hizo huduma hiyo imewezesha kuwepo na amana za shilingi bilioni 6
 kutoka kwa wateja laki 7 ambao wanapata huduma ya M-Pawa,Taarifa 
hiyo ya mafanikio imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Julius 
Mcharo akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa Wateja 
iliyofanyika Kariakoo.
Mcharo 
alisema huduma hiyo inayotolewa kwa ushirikiano kati ya benki hiyo na 
Vodacom imepata muitikio kutokana na watanzania kuweza kufungua akaunti 
za huduma hiyo mahali popote pale walipo kwa kutumia mtandao.
Alisema 
huduma hiyo ambayo pia inawezesha kupatikana kwa mikopo na kupokea na 
kulipa huduma mbalimbali kwa m-pesa imerahisisha maisha ya wananchi 
wengi na kusema kwamba itaendelea kuboreshwa na kutanuliwa.
Akizungumzia
 wiki ya huduma kwa wateja alisema kwamba watendaji wote wa benki hiyo 
wanakwenda katika matawi yapatayo 11 nchini kote kutoa huduma kwa karibu
 zaidi na wateja wao kwa lengo la kufahamu changamoto zao.
Alisema changamoto hizo zitawawezesha kutambua mahitaji halisi ya wateja na kutengeneza bidhaa zinazolingana na mahitaji yao.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo watatu kutoka kushoto akiwa na wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la k.koo


