Kwa baadhi ya watu simu ya mkononi ni kifaa tu 
cha mawasIliano ilihali kwa wengine ni kifa ambacho kinaweza kukuweka 
katika hali ya kufa kupona.
Mfungwa mmoja nchini Kenya amewaacha 
wengi vinywa wazi, baada ya simu tatu za mkononi kutolewa mwilini mwake.
 Inaarifia aliziingiza simu hizo mwilini mwake kupitia sehemu yake nyeti
 ya nyuma.
Mfungwa huyo wa gereza la King'ong'o katika jimbo la 
Nyeri alifanyiwa upasuaji Jumanne kutolewa simu hizo ambazo alikuwa 
amezificha mwilini mwake kupitia sehemu yake ya nyuma.
Tatizo la kuingiza bidhaa kimagendo ndani ya magereza ni kero kubwa kwa maafisa wakuu wa magereza.Wamekuwa
 kwa miaka mingi wakijaribu kulikomesha tatizo hilo bila mafanikio.Kwa 
njia yoyote ile wafungwa huingiza bidhaa kama simu katika magereza 
nchini Kenya kinyume na sheria za magereza.
Maafisa wa magereza 
wanakiri kwamba wafungwa hawa wakati mwingine hushirikiana na walinzi wa
 magereza kuingiza bidhaa katika magereza kimagendo.
Chanzo:Bbc 
