  | 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush  
 
 (Bush Presidential Library) sehemu ambayo imejengwa kwa mfano wa Ikulu 
ya Marekani, White House, hususan katika bustani y a Waziri (Rose 
Garden) pamoja na ofisi ya Rais wa Marekani, Oval office | 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)
 na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais
 Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa
 Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa 
kabisa ya habari na mawasiliano.
Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda
 Houston, jimbo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara
 wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo hapa 
Tanzania. 
Rais Kikwete amekuwa Marekani kwa ziara ya 
kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria 
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake 
jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika 
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
  | 
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma 
Kikwete wakitembelea na kujionea vitu mbalimbali ambavyo Rais mstaafu 
George W. Bush alipewa kama zawadi kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa
 katika Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) | 
  | 
| Rais Jakaya 
Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea na kujionea vitu 
mbalimbali ambavyo Rais mstaafu George W. Bush alipewa kama zawadi 
kutoka Tanzania ambavyo vimehifadhiwa katika Maktaba ya Kirais ya Rais 
Bush (Bush Presidential Library) | 
  | 
|  Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea sehemu ya 
mfano wa ofisi ya kupangia mikakati ya Ikulu ya Marekani iliyotumika na 
Rais MStaafu George W. Bush kwenye Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library) | 
CHANZO:WAVUTI