Baadhi
 ya wanasheria wameunga mkono utaratibu wa  Rais kutia saini Muswada wa 
 Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, 
uliopitishwa hivi karibuni na Bunge kwa hoja kwamba umepitia   mchakato 
sahihi na halali wa Kikatiba.
Wanasheria hao wakaeleza kumshangaa
 mwanasheria mwenzao na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu 
(CHADEMA), kwa ushauri wake alioutangaza kwa umma, kumtaka Rais asisaini
 muswada huo, kwamba ushauri huo ni wa 
 
 
kisiasa zaidi, usio na tija kwa uongozi wala unaofuata utaratibu na sheria.
Wamenukuliwa
 wakizungumza na mwandishi kwa nyakati tofauti jana, wakisema kuwa 
muswada huo kama ilivyo miswada mingine ya sheria, una nafasi ya 
kusainiwa na yakiwepo marekebisho, unarudishwa bungeni kujadiliwa na 
kurekebishwa.
Wakili wa kujitegemea, John Mapinduzi alisema: "Lazima
 muswada huo usainiwe ndipo urudishwe bungeni kwa marekebisho, Lissu ni 
mwanasiasa tu anapotosha umma… sasa utarudishwaje bungeni wakati 
ulishapita?" Alihoji Mapinduzi.
Mwanasheria mwingine wa kujitegemea, Jerome Msemwa alisema kusainiwa muswada huo ni njia sahihi na inafanyika mara nyingi (??) na kama kuna marekebisho, yanafanyika baadaye: "Wabunge
 kama Lissu waliamua kutoka wenyewe bungeni wakati muswada unajadiliwa… 
hakuna aliyewafukuza, sasa iweje leo watake usisainiwe? Haina maana leo 
hii kumshauri Rais kutosaini. Ushauri wa Lissu, kisheria hauna maana 
yoyote, hawezi kumshauri Rais leo asisaini wakati anafahamu kuwa hata 
baada ya kusainiwa, kuna nafasi ya kurudishwa bungeni na kujadiliwa kwa 
marekebisho yoyote," alisema Msemwa.
Msemwa alisema Rais
 asiposaini muswada huo na kuurudisha bungeni, maana yake vikao vya 
wabunge vilivyokaa Dodoma  kujadili muswada huo, vilipoteza muda na 
fedha za wananchi bure.  --- via HabariLeo