Diamond akimkiss Penny kuonesha mapenzi yao
Katika siku za hivi karibuni katika magazeti mbali mbali ya hapa Bongo pamoja na mitandaoni kumekuwa na habari inayosema kuwa Naseeb Abdulmalik "Diamond" amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye aliachana nae kutokana na mwana dada huyo Wema  Sepetu kukosa uaminifu katika mapenzi yao.
Taarifa zaidi zilisema kuwa Wema na Diamond walikutana Dubai wakati Diamond akienda Indonessia na Wema akielekea Hong kong na kula bata sana tu na kuashiria kuwa wamerudiana.
Lakini Diamond ameeleza kwenye Blog yake This is Diamond habari yote kama ifuatavyo:-
"Kumekuwa na Uvumi na Habari nyingi sana 
Mitandaoni na
 Kwenye Media tofauti... kwamba mimi na Mwanadada Wema Sepetu tuna 
mahusiano ya Kimapenzi, kitu
 ambacho Sikweli na taarifa hizo ni za 
uongo.. uvumi huu ulianza kisa tu yeye kucomment kwenye Account yangu ya
 Instagram?..
Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu 
mkiwa hamko kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze  ama Kushiriki  kwa 
chochote? Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana
Mnapenda kuona watu 
wanauadui... nimuda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la 
Tanzania na si kuwekeana chuki zisizo na faida.." alisema Diamond.
Diamond akiwa na Penny
Chanzo:http://wasafii.blogspot.com