
SAKATA
 la wizi wa fedha katika akaunti za wateja wa benki, sasa limeingia 
katika sura mpya baada ya Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk Gervas 
Mbasa (Chadema) naye kuibuka na kudai kuwa ameibiwa Sh6 milioni kutoka 
kwenye akaunti yake. Akizungumzia
 wizi huo, mbunge huyo alisema fedha zake ziliibwa kwa nyakati tofauti 
kati ya Desemba 20 mwaka jana na Januari 3, mwaka huu. 
Alisema
 kitendo hicho kilifanywa na mtu mmoja aliyempigia simu na mtu mmoja 
aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa Makao Makuu ya Kampuni ya Airtel
 na kwamba alikuwa katika zoezi la kuhakiki namba zote za zamani.
“Alinieleza
 kwamba kwa niaba ya Airtel yupo katika zoezi la kuhakiki namba zote 
zilizosajiliwa zamani na yangu ilikuwa ni ya miaka 10 na akaniuliza 
namba ya mwisho kuwasiliana na mtu kupitia simu yangu. Nilimtajia namba 
ya mke wangu na baada ya maelezo hayo aliniomba nisizime simu yangu 
wakati wakiwa wanashughulika na kuisajili na kwamba muda wowote 
nitapatiwa maelekezo,” alieleza mbunge huyo.













